Mapema leo Jijini Dar es Salaam, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, nimepokea Tuzo ya The GoalKeepers Award inayotolewa na Taasisi ya Gates Foundation.
Tuzo hii ni heshima kubwa kwetu Watanzania kwani mbali na sisi kufurahia matunda ya hatua kubwa tunazoendelea kupiga katika sekta ya afya, inadhihirisha dunia inatambua juhudi zetu katika kuboresha afya ya uzazi na afya ya Mama na Mtoto.
Nchi yetu imefanya kazi kubwa na ya kujivunia, ambapo mpaka sasa tumefanikiwa kupunguza vifo vya uzazi kwa asilimia 80%, kutoka vifo 556 kwa kila vizazi 100,000 hadi 104; na vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka 67 hadi 43 kwa kila vizazi 1,000.
Kazi hii njema inaendelea ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wataalamu wa afya, kutoa huduma za afya bure kwa akina mama na watoto, kuanzisha programu za lishe, kuimarisha mifumo ya rufaa, kuboresha huduma za dharura na kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ya afya mijini na vijijini.
Tuzo hii naielekeza kwa watumishi wa afya kote nchini kwa kazi kubwa wanayofanya usiku na mchana kuwahudumia Watanzania, lakini pia kwa washirika wetu na wadau wa maendeleo katika kazi ya kuboresha afya ya uzazi nchini.
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (@TFSAgency) imetakiwa kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mbegu za miche ya miti ili zifikie wananchi wengi zaidi na hatimaye kushiriki katika kuongoa misitu iliyotoweka. @AngellahKairuki@dossilayo@MNRT_Tanzania
WAZIRI KAIRUKI AWASILI MOROGORO KWA ZIARA YA KIKAZI
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. @AngellahKairuki (Mb) leo Julai 8,2024 amewasili Mkoani Morogoro na kusaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambapo atafanya ziara ya kikazi katika ofisi za TAWA.
TANZANIA, QATAR KUSHIRIKIANA SEKTA YA UTALII
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nchi ya @qatar ziko mbioni kusaini Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding-MOU) kushirikiana katika nyanja mbalimbali za Sekta ya Maliasili na Utalii. #ALT@AngellahKairuki@WTTC
📍Bungeni, Dodoma
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda akiwa akiwa bungeni jijini Dodoma leo Mei 20, 2024.
Jenerali Mkunda ni miongoni mwa wageni waliofika bungeni kushuhudia uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa Fedha 2024-2025.
📸 Credit; Hakingowi
Waziri Mkuu @KassimMajaliwa_ leo Mei 17, 2024 atafunga Mkutano wa 79 wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM), hafla hiyo inafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Johari Rotana Jijini Dar es salaam. @TZWaziriMkuu
MAJALIWA: MICHEZO NI NYENZO MUHIMU INAYODUMISHA AMANI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ushirikiano katika michezo ni nyenzo muhimu katika kudumisha diplomasia na amani miongoni mwa nchi washirika wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM). #ALT@TZWaziriMkuu@tzbranding
📍Arusha
🔹WAZIRI KAIRUKI ATETA NA WAONGOZA WATALII JIJINI ARUSHA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. @AngellahKairuki (Mb.) amekutana na Waongoza Watalii kwa lengo la kusikiliza changamoto zao, maoni na ushauri katika kuboresha Sekta ya Utalii nchini; kikao kilichofanyika katika Jengo la Ngorongoro jijini Arusha, leo Aprili 06, 2024.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. @Abbastz2 pamoja na Watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake.
📸: W/Maliasili na Utalii
📍Buckingham Palace, Uingereza
🇹🇿🇬🇧
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Mbelwa Kairuki amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme Charles katika Kasri la Buckingham Machi 21, 2024.
Mara tu baada ya kuwasilisha Hati hizo, Mfalme Charles amemkaribisha Balozi Kairuki Buckingham katika Kikao cha faragha.
📸:Ubalozi wa Tanzania-Uingereza
🔴TEUZI
Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amemteua Prof Aloys Mvuma kuwa mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliajo Tanzania -TCRA
Kwa viongozi tuliowaapisha leo na kuwapa dhamana adhimu ya kuwatumikia wananchi kwenye maeneo mbalimbali, na wote mnaoendelea na nafasi zenu katika utumishi wa umma, nendeni mkafanye kazi.
Wananchi wanataka kazi na matokeo mazuri na si vinginevyo. Mimi ni Mama, sina kundi, wote ni wangu, wote nalea. Nataka mkafanye kazi. Wanaofanya vizuri nitawapongeza. Wanaofanya vibaya nitaendelea kushughulika nao.
Minister @AngellahKairuki has also met and held talks with the Int'l Advertising Company of @ExpediaGroup as well as a company from Slovakia that sends tourists to the 🌍 for more than 85% from that country and has advertisements on their TV's and discussed how to cooperate.
📍Arusha
🟩 FTI NI CHUO BORA DUNIANI - WAZIRI KAIRUKI
Chuo cha Misitu Olmotonyi (FTI) ni chuo pekee kikubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 1937 na ni moja ya chuo bora kabisa kuwepo Afrika Mashariki, Afrika na Duniani, katika utoaji wa mafunzo ya misitu kwa nadharia na vitendo.
Hayo yamesemwa leo Februari 05,2024 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. @AngellahKairuki (Mb.) alipofanya ziara ya kikazi katika chuo hicho kilichopo jijini Arusha.
Chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo ya misitu katika kozi za Astashahada ya awali ya misitu, Astashahada ya Misitu, Stashahada ya Misitu, Stashahada ya Misitu ya mijini na usanifu wa mandhari, stashahada ya joinfomantiki katika usimamizi wa maliasili (Geoinformatics for Natural Resources and Management) pamoja na mafunzo ya muda mfupi ya misitu na uhifadhi wa mazingira.
Waziri Kairuki amesema ili kukikuza zaidi chuo hicho, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kufanya mapitio ya mitaala yake kuhakikisha kwamba inaendana na mahitaji ya sasa ya kidunia katika taaluma ya ulinzi, usimamizi na uendelezaji wa misitu.
Aidha, amesema Wizara itaendelea kuboresha mazingira ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kuangalia namna ya kuongeza karakana, mashine mpya, majengo maya na maboresho mengine.
“Tunaweka mkazo kuhakikisha kwamba tunaboresha miundombinu ili tuweze kuwa na wanafunzi wengi zaidi, wataalamu wa ndani watakaoenda kufanya kazi katika kulinda na kuendeleza misitu yetu ikizingatiwa kwamba Tanzania ina eneo kubwa sana la misitu inayosimamiwa na Serikali Kuu, Serikali za mitaa kupitia villi na watu binafsi hasa tukitambua umuhimu wa misitu yetu katika utunzaji wa mazingira, uwepo wa vyanzo vya maji na masuala engine kwa ujumla wake” amesisitiza Mhe. Kairuki.
Awali, akizungumza na menejimenti ya chuo hicho, Waziri Kairuki ameitaka kuendelea kukitangaza zaidi chuo hicho.
“Tuendelee kukitangaza chuo kwa kadri inavyowezekana na tujimarishe zaidi katika utoaji wa mafunzo haya ili tuvutie wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi” amesema Mhe. Kairuki.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Misitu Olmotonyi,Dkt. Joseph Makero ameahidi kuwa watumishi wa chuo hicho wanajitahidi kufanya majukumu yao.
📸: W/Maliasili na Utalii