πLUSAIL STADIUM
Uwezo -80, 000.
Dimba Hili Linapatikana Katika Jiji la Lusail, Hapa Ndipo Itapigwa Fainali Ya michuano hii kwa Mwaka Huu.Uwanja sa Kipekee kutokana na Ubora wake na mvuto wa aina Yake.
Zitapigwa Mechi 10 Ikiwepo na Ya Fainali katika Dimba Hili.
π Al JANAUB STADIUM.
Uwezo -40, 000.
Unapatikana katika Jiji la Al Wakrah , Ni Jiji lenye historia nyingi kwa uvuvi , Ubunifu wa uwanja Huu umechochewa na nakshi zilizojaa upepo za Boti za Kitamaduni za Qatar zikionesha asili na heshima kwa wavuvi wa al Wakrah kama Alama .
πKHALIFA INTERNATIONAL STADIUM.
Uwezo -40000.
Ni uwanja wa kipekee uliochezwa Mechi nyingi za Mpira wa Miguu na Hafra za Riadha tangu Kufunguliwa kwake Mnamo 1976.
Ni Uwanja wenye vivutio vingi na Ulifanyiwa Baadhi Ya marekebisho ili Kuweza kutumika katika michuano Hii.
π EDUCATION CITY STADIUM
Uwezo -40, 000
Uwanja Huu umewezeshwa na vyuo vikuu vya jirani , Upo jiji la elimu Ambalo ni kitovu cha Kujifunza na Maarifa.Korido za uwanja Huu zimejaaa Mawazo tafiti za vitu mbali mbali, Ufumbuzi, Muundo wake una sanifu Desturi Mila za Kiislamu.