Baadala ya kukimbilia maji ya upako, mafuta, udongo; tambua Mungu anafanya kazi ya uponyaji kupitia ktk mikono ya madaktari.
Ndio maana kanisa katoliki linajenga hosp, vituo vya afya na kusomesha madaktari na wahudumu wa afya.
Hayo mengine ni uganga, uchawi na nguvu za shetani.
Anaitwa mchungaji Abiud Mishori miongoni mwa waimbaji wakubwa sana wa muziki wa injili hapa nchini huku akiwabariki mamia na maelfu ya watu wengi sana nyimbo zake kama vile ule wa "Lini Utapita Kwangu" , "Nani Atanitazama" zilikuwa zinawafariji watu wengi sana huku wengine wakilia kutokana na namna ya uimbaji wake wa kugusa nyoyo za watu..
Ikumbukwe jamaa alianza huduma ya kichungaji na mke wake mama mishori katika mazingira magumu sana ambayo ameshawahi yasimulia kwenye nyimbo zake.
Nyimbo zake zina upako mwingi sana🫡🙌🏾
Mwaka 2005 niliwahi kufanya kazi kitengo maalumu ndani ya chama cha kupokea, kusoma na kuchakata taarifa za vyama vya upinzani zinazotumwa na watu wa ndani wa vyama vya upinzania. Kila siku iendayo kwa Mungu, kila chama kinatuma ripoti ya kazi, mipango na utendaji ya chama chao.
The EPP Group has nominated lawyer, human rights activist and politician Mr Tundu Lissu as a candidate for the Sakharov Prize.
After surviving a 2017 assassination attempt, Mr Lissu returned to Tanzania to continue advocating democratic reform, only to face arrest, treason charges and exclusion from the 2025 presidential election, while his party was barred from participating.
His case reflects the wider erosion of democratic pluralism and political competition in Tanzania.
For the EPP Group, Mr Lissu represents a powerful combination of personal courage, democratic conviction and geopolitical relevance. His nomination affirms that Europe stands with those defending constitutional democracy and political freedom in Africa and in other partner countries of the EU. Mr Lissu embodies the defence of democracy, political pluralism, the rule of law and fundamental freedoms at extraordinary personal cost.
The Sakharov Prize for Freedom of Thought is the highest tribute paid by the European Union to human rights work.
Serikali Katili ya CCM na wapambe wake wanajisahaulisha kuwa [wananchi] ndio walioathirika zaidi awamu hii baada ya umwagaji damu uliofanywa deliberately Oktoba 29, 2025. Jambo lolote linaloitwa ‘maridhiano’ haliwezi kuwa uamuzi wa wanasiasa tena—wananchi ndio wanastahili kuongoza na kuweka masharti. Baada ya hapo ndipo mchakato wa kuunda Katiba Mpya uweze kuanza. Circumstances have fundamentally changed.
Prof Tibaijuka aliniambia tuna kazi ngumu kuliko ya Mwl Nyerere.
Nyerere alipambana na wakoloni kwanza walikua wanafuata sheria.
Lakini hawa wakoloni weusi hawafuati sheria.
Wakaloni walikua hawatoi rushwa.
Wakoloni weusi wanahonga kila mtu.
Ukweli ni kwamba tutawashinda hata wakitumia nguvu gani.
Vitol yuko na nani?
Nani wamempa tenda ambayo Watanzania wanauziwa mafuta kwa usd 200-260 wakati Uganda anauziwa usd 83 na Msumbiji anauziwa usd 90.
Hawa Namaro waliosajiliwa Dubai mwaka 2023 ni kina nani? Wana uhusiano gani na wizi huu mkubwa unaoumiza Watanzania.
Vyombo vya habari Tanzania kwanini hamfuatilii na kuandika huu ujambazi unaongamiza Nchi kwenye wizi wa mafuta..
TPDC kwanini hawakutoa tenda shindanishi katika suala kubwa kama hili la mafuta.
Baada ya Serikali haramu ya Mama Abduli kushindwa kurubuni Viongozi wetu wa Chama kwa fedha ili waingize CHADEMA kwenye maridhiano sasa wameamua kutumia mbinu mpya ya kuhonga watu fedha ili kutengeneza drama za kipumbavu zenye lengo la kuwachafua haswa wakimlenga Mhe. Heche.
Abduli na mama yake wamemwaga fedha nyingi kwa baadhi ya viongozi wa Chadema na Machawa kwa lengo la kumshambulia Heche, Kuanza leo na siku zijazo tutegemee kusikia Press nyingi kutoka kwa watu kadhaa zikimtuhumu Heche na kumuingiza kwenye kashfa mbalimbali.
Vijana tutapambana na uhuni huu kwa nguvu kubwa, Tutawalinda viongozi wetu kwa wivu mkubwa.
Watanzania @HecheJohn na @TunduALissu wanatuhitaji kupita kiasi.
Heche anapigwa vita sababu kuna viongozi ndani ya Chadema wamefika bei ya maridhiano na CCM so wanajaribu kumuondoa Heche ili waweke mtu ambae atafanya maridhiano..
“Nakutakia upendo mwingi, rafiki yangu—nakukumbuka sana. Bado wewe ni miongoni mwa akili bora kabisa ambazo nchi hii inazo. Ninaendelea kukuombea—Mungu akupe ujasiri, nguvu na ustahimilivu wa kushinda changamoto zote zilizo mbele yako.”
“Much love, my friend—I miss you deeply. You are still one of the finest brains this country has. I’m keeping you in my prayers—may God give you the courage, strength, and resilience to rise above every challenge before you.”
Msimamo wa chama juu ya mauaji uloliofanywa na serikali haramu na dhalimu ya Samia na Chama Cha Mamumiani u wazi.
Bahati nzuri Kamati Kuu ya Chadema itakaa tarehe 28-29 Aprili 2026 na kupokea ripoti ya Wajumbe wa Chadema waliokutana na Mjumbe wa Umoja wa Mataifa na wale waliokutana na Raisi Mstaafu wa Malawi Lazarus Chakwera na kutoa msimamo wake rasmi.
Msimamo wa chama kikuu cha siasa katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania unatokana na vikao rasmi. Hivyo sote tutulie na kusubiri kauli ya Kamati Kuu ya Chadema.
Cha uhakika ni kuwa hiki si chama cha walamba asali au walishwa peremende bali hiki ni chama cha Ukombozi wa Pili wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
MARIDHIANO BILA UKWELI NA UWAJIBIKAJI NI USALITI.
Historia haina huruma kwa watawala katili. Historia inatunza kumbukumbu za sauti zilizopazwa wakati wa mchana kweupe, lakini zikamezwa na giza totoro. Leo watawala wanazungumzia Maridhiano, neno tamu vinywani, lakini lenye makovu makubwa moyoni.
Kumbukumbu hazidanganyi. Humphrey Polepole alisimama, akanyoosha kidole akasema: “Tupatane kwanza kabla ya uchaguzi” Matokeo yake? Akapotezwa. Je, alipotea kwa hiari au alipotezwa kwa lazima? Sauti yake ikawa kama mwangwi uliopotea bondeni.
Mzee Warioba, mbeba maono ya katiba, akapaza sauti: “Tusikimbilie sanduku la kura bila maridhiano.” Badala ya kumsikiliza, mawe yakawa majibu yake. Mzee wa heshima akazuiwa, akawa mfungwa wa mawazo yake mwenyewe ndani ya kuta za nyumbani kwake.
Askofu Josephat Gwajima, akajitokeza, akashauri chama chake na watawala, nchi inahitaji uponyaji, majadiliano kabla ya kwenda katika uchaguzi. Akashauri, uchaguzi huru na haki ni tunda la amani. Hakusikilizwa. Akapuuzwa. Akatukanwa. Akashambuliwa sana.
Vipi kuhusu Captain Tesha? Alisema mengi, akataka maridhiano ya dhati. Akasema mifumo imeharibika na inahitaji marekebisho. Leo, sauti yake imekuwa kama redio iliyozimwa ghafla katikati ya msiba mzito. Tesha na wengine, walioona mvua kabla ya mawingu..
CHADEMA hatuwezi kusahau hata kidogo. Chini ya jua kali na mvua za el nino, kwenye ngurumo nzito na radi, tulipita katika matope tukidai kitu kimoja: Mageuzi ya kimsinhi kabla ya Uchaguzi. Lakini majibu yalikuwa ni kutekwa, magereza, na kuzuiliwa kufanya siasa.
Shingo za watawala zilijawa na kiburi, mioyo ikawa migumu, mkiamini kuwa ushindi ni kuiba kura na si kuchaguliwa na wananchi. Hamkutaka kuchaguliwa. Mliamua kujitangaza washindi kwa ushindi wa kishindo. Watu milioni 32 walishiriki uchaguzi wapi?
Vongozi wa kiroho hawakukaa kimya. TEC, Bagonza, na Gwajima, wote walionya. Walisema maridhiano si chaguo, ni hitaji la lazima ili taifa lipumue. Lakini, shingo zilikuwa ngumu. Mkajiona miungu watu msiohitaji ushauri wa ardhi wala mbingu. Mkasonga mbele.
Fr. Dkt. Charles Kitima, mwanatheolojia, alipojaribu kutoa ushauri wake wa busara kuelekea uchaguzi mkuu akiwa salama ndani ya makazi ya Maaskofu, alivamiwa na maharamia. Alishambuliwa. Akaonewa sana. Akayaona mauti moja kwa moja usoni kwake. Mbaya sana.
Mliamua kushughulika hata na viongozi wa dini. Hakika, mlivuka mipaka. Mdude Nyagali alivamiwa, akatekwa na kupotezwa kabisa. Deusdedith Soka alitekwa na kupotezwa. Dioniz Kipanya alitekwa na kupotezwa. Mamia ya vijana wa CHADEMA, wafuasi wazalendo, watoto wa Tanzania. Walitekwa, wakapotezwa.
Baada ya kuitimiza azma yenu ya kishari; baada ya kuwapoteza wenye sauti na kuwapiga mawe wenye hekima; baada ya kuvuna mlichokusudia kwa nguvu. Mmefikia kile mlichokusudia. Mlichokikinga, mlichokilinda, mlichokitimiza kwa nguvu zote.
Mnataka Maridhiano ya aina gani? Je, ni maridhiano ya kumsafisha aliyetenda makosa bila kutubu? Je, ni maridhiano ya kunyamazisha waliojeruhiwa ili msisikie sauti za maumivu yao? Ni maridhiano ya dhati yanayoanza na KUKIRI MAKOSA na KUWAJIBIKA?
Maridhiano bila haki ni usaliti. HAKI za watu ambao wameuwawa, wamepotezwa, wamefungwa, wamejeruhiwa. Maridhiano bila ya wahusika kukiri makosa ni kiini macho. CHADEMA hatuwezi kutumika katika safari ya wananchi kuelekea kusikojulikana.
Maridhiano ya kweli yanahitaji ujasiri wa kukiri makosa, si ujasiri wa kuficha yaliyopita. Yanahitaji haki, si hila. Yanahitaji sauti zote zisikike, si sauti za wapinzani kuzimwa ili zao pekee zisikike. Wapinzani waseme wapi panavuja. Watawala wakiri makosa yao. Tusonge.
Kama mmetimiza mlichokusudia, angalau kuweni na ujasiri wa kusema: Tulikosea, tuanze upya. Tanzania mpya inawezekana. Lakini huo upya wa Tanzania hauji kwa kufuta kumbukumbu za matukio mabaya yaliyotokea. Unakuja kwa kukabiliana na ukweli.
NB; Hakuna mgao wa kipande cha keki ya maridhiano kwenye sahani yenye damu.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Sijawahi kufanya video kwa ajili ya Chadema hii ndio ya kwanza.
Chadema tunaomba msituangushe kwenye hili. Watanzania tumezika watu kwa ajili ya haki sio kwa ajili ya Lissu kutoka ndani au kwa ajili ya Chadema kufanya siasi.