Karibuni sana kujiunga na sisi katika kugusa maisha ya watanzania wenzetu wenye uhitaji kwa mwezi tunatoa Sadaka kuanzia sh-2000 tuu mawasiliano 0755-559013
Huyu ni Dada Dayati John Kaduga, mwenye ulemavu anaishi mkoani Arusha, Loliondo Sonjo katika nyumba ya kupanga (kodi 5,000.- kwa mwezi) akiwa na mama yake mzazi baada ya kutimuliwa.Karibuni kujiunga na sisi wasiliana na sisi kwa namba 0755-559013
https://t.co/sdch5zM0f4
Jumamosi 22 October 2022 Tunawaletea simulizi nzuri iliyotokea mkoani Arusha, ni kwa yule mama aliyetelekezwa na mumewe sababu eti amezaa mtoto wa ziada (mimba isiyotarajiwa), ni pale kwa Mrefu mkoani Arusha, alikua anaomba Mtaji wa biashara ya kuuza genge
https://t.co/O5TA4eQGDQ
Ndani ya Sadaka Yetu Group tuna Wekahazina ambao wameenea nchi nzima kwa ajili ya kutunza fedha za kusaidia watu wenye uhitaji. Unaweza kuungana nasi popote ulipo ambapo huwa tunatoa kuanzia sh. 2,000/-Karibuni kuungana na sisi mawasiliano 0755-559013
https://t.co/Ve0yMWyDKm
Karibuni sana kujiunga na sisi katika kugusa maisha ya watanzania wenzetu wenye uhitaji ukitaka kujiunga na sisi au unahitaji kujua chochote kuhusu Sadaka Yetu Group au una swali lolote unaweza kuwasiliana na sisi kwa namba 0755559013 .
Sadaka Yetu Group kwa ajili wengine .
Amekuwa akiishi kwa maumivu ya moyo lakini ameniandikia ujumbe kuwa ’SASA MIGUU YANGU IMEREJEA BAADA YA HII BAISKELI’Tulishamnunulia godoro maalum la upepo la sh. 350,000/- maana hawezi kulalia magodoro haya ya kawaida sababu ya vidonda, pia tumeajiri mtu wa kumsaidia kila mwezi
Isdory ana historia mbaya ya kupigwa risasi na Jeshi la Polisi kwenye uti wa mgongo miaka kadhaa iliyopita akiwa na bodaboda yake, hali iliyopelekea kupooza kuanzia kiunoni kushuka chini, Jeshi la Polisi limekanusha kuhusika na hili tukio na halijawahi kumlipa hata sh.100
Baaada ya msamaria mwema mmoja kumnunulia baiskeli ya kisasa Isdory na watu wabaya kumuibia betri hatimaye sisi tulinunua tena hizo betri zenye thamani ya shilingi 80,000/- na ku-replace pale kwenye betri na hatimaye furaha yake imerejea .Ameanza kuendesha baiskeli yake sasa .
Licha ya kwamba bado tuna wagonjwa wawili India, lakini naomba tujipe challenge ya masaa 72 tumsaidie Janan kwenda Afrika kusini kwa matibabu. Kumbuka mfadhili amepatikana bado gharama za usafiri na fedha za kujikimu kwa miezi minne watakayokua huko
Changamoto iliyopo kwa sasa ni gharama za usafiri pamoja na fedha za kujikimu wakiwa huko. Makadirio ni TZS 10M. Niliposikia habari hii kwanza nilimshukuru Mungu, kisha nikaahidi kuwasaidia gharama zilizobakia (usafiri na pesa za kujikimu).
Namshukuru Mungu kwamba Sugu kwa kushirikiana na familia ya mtoto walipambana na wamefanikiwa kupata mfadhili ambaye amekubali kulipia TZS 40M matibabu ya Janan nchini Afrika kusini. Mungu ambariki sana
Wakati ule tulikua na wagonjwa watatu India, mmoja Nairobi na wengine hospitali za ndani ya nchi. Sikuwa na uwezo kuwahudumia wote kwa wakati mmoja. Hivyo nikamuomba awe mvumilivu angalau waliopo nje ya nchi wakirejea, nitakua nimepunguza mzigo na kuweza kumsaidia Janan.
Janan amepitia mateso yote akiwa bado mdogo sana. Sugu aliponikutanisha nae aliniambia "Kamanda, najua una maelfu ya watu wanaokutegemea, lakini tafadhali okoa maisha ya huyu mtoto"
Alishindwa kupumua vizuri, akavimba miguu, maumivu kifuani na kupoteza fahamu. Pia mapafu yalijaa maji na kuwekewa mpira wa kutoa maji. Alishindwa kula kwa njia ya kawaida na hivyo kuwekewa mpira wa chakula (feeding tube).
Janan alizaliwa 17/11/2016, lakini aliumia sehemu ya ubongo na hivyo kuathiri ukuaji wake hasa wa akili. Wakati familia ikihangaika na matibabu, aligundulika na tatizo la moyo kutanuka (Cardiomegaly); yani moyo kuwa mkubwa kupita kawaida na kufanya chemba za moyo nazo kutanuka.
Anaandika @MalisaGJ_ .
Huyu mtoto anaitwa Janan Chomba. Nilitambulishwa kwake na Mhe.Joseph Mbilinyi (Sugu) mwaka jana mwezi November, akiwa kama mnavyomuona. Sugu aliniunganisha na baba yake (Juma Chomba) akanielezea historia ya tatizo la mwanae.
Inaendelea...