Mwanachama wa @ACTwazalendo|
Mwakilishi wa Jimbo la Gando na Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano|
Waziri Kivuli Ofisi ya MakamRais Muungano @ACTBarazaKivuli
Sikiza! Lala nayo hii.👇🏿
Huko nyuma ilikuwa mtu anaweza akaanzisha biashara Tanzania aliyoisajili nje ya nchi. Kisha baada ya miaka mitano ya kupata faida kubwa huku akiwa na msamaha wa kodi(Tax Holiday) anaiuza kampuni na kubadilisha jina. Kampuni mpya inaendelea na biashara ileile huku nayo ikijipatia miaka yake mitano ya msamaha wa kodi. Nchi haipati chochote!😭
Mfano👇🏿
Celtel=>Zain=>Airtel
KC Mstaafu @zittokabwe akabadilisha mchezo huu mwaka 2012 akiwa bungeni Dodoma.
Nimekuwekea video. Msikilize yeye mwenyewe uone akisimulia jinsi mchakato wa kutunga sheria ulivyokuwa kwenye bunge lililotawaliwa na CCM. Tangu sheria hiyo itungwe, nchi yetu inafaidika.💪🏿
@ACTwazalendo
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
@KakaMkuu94@ACTwazalendo Hili nimelipokea kijana! Kubana na kubinya mtandao huu si sawa! Huku ni kupora haki ya raia kupata habari. Pia natambua vijana wengi hii mitandao ni fursa kwenu lakini CCM hilo hawalioni.
Sehemu ya mchango wangu katika bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani bungeni Dodoma.
Pamoja na mambo mengine nimetaka Jeshi la Polisi lisafishwe. Liwe na uhusiano mwema na raia ili hata polisi wetu wakija kustaafu wasije kutengwa uraiani.
#TaifaLaWote#MaslahiYaWote@ACTwazalendo
DKT. NASRA AIBUA MAZITO ZANZIBAR: AFICHUA YATIMA KULALA NJAA. AHOJI ZILIKO BILIONI ZA MRADI WA ‘PAMOJA’
Mwakilishi wa Viti Maalumu wa @ACTwazalendo, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi, Mhe. Dkt. @drnasranassor amelipua bomu zito linaloanika uzembe na viashiria vya ufisadi katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Katika hotuba yake Dkt. Nasra amefichua kashfa katika kituo cha kulelea yatima Mazizini, ambapo watoto wanalala njaa wakati stoo imejaa shehena ya chakula kutokana na usimamizi mbovu. Pia, amesema jengo la kituo halijafanyiwa ukarabati tangu mwezi Machi lilipoungua moto.
Kuhusu mradi wa jinsia wa PAMOJA, Dkt. Nasra amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha wa 2025/2026 Serikali iliweka Sh bilioni 6.512 kwenye mradi wa PAMOJA, walakini ni Sh milioni 685 tu (10%) ndio zilizotumika hadi mwaka wa fedha unamalizika. Hapa Dkt. Nasra akahoji, ziko wapi asilimia 90 ya fedha zilizotengwa?
Kwenye mradi wa Nyumba za Limbani (Sh bilioni 2.2), Dkt. Nasra ameeleza kuwa kamati yao ilibaini njama za watendaji waliotaka kumfukuza mkandarasi aliyebakiza hatua za mwisho (finishing) na ambaye tayari ameshalipwa 93% ya fedha, kwa lengo la kuingiza mkandarasi mpya.
Kufuatia msimamo huo wa Dkt. Nasra, Wizara imetakiwa kutoa majibu ya kina mbele ya Baraza kabla ya bajeti mpya kuidhinishwa.
#ZanzibarMpya #ZanzibarMoja #MamlakaKamili
Nilipokuwa nikichangia bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Pili Rais. Nilizungumzia Tume ya Uchaguzi na jinsi inavyoendelea kuwa kikwazo kikubwa cha demokrasia yetu ya Zanzibar.
#ZanzibarMpya#ZanzibarMoja#MamlakaKamili