@azamtvtz NAITWA SAID MILO WA MBAGALA DAR ES SALAAM.
Matokeo ya leo yanaakisi mechi yenye ushindani wa hali kwa maana simba na yanga msimu huu wana timu nzuri zilizojitosheleza kimbinu. Karata yangu naitupa kwa SIMBA machi 8. UBAYA UBWELA
i. Kuna kizazi kilioa wanawake bikra.
ii.Kikaja kizazi kikawa kinaoa wanawake wasio bikra.
iii. Kikaja kizazi kikawa kinaoa wanawake waliotoa mimba.
iv. Kukaja kizazi kikawa kinaoa wanawake wenye watoto.
v. kizazi kikawa kinaoa wanawake wasio bikra, waliotoa mimba na wenye watoto kwa pamoja.
Unaweza kuona upumbavu wa wanaume wa sasa ukowapi, hatuna standards tena wakati wanawake hawatokukubali kama hauna kakitu unaweka mezani.
Men now hatuna standard, tunajibebea yeyote Provided that ana WetCrack.
KWAHERI UJAMBAZINI (PART 2)
Ndani ya selo namba 2,special wing sikuwahi kuwa na huzuni, majuto wala upweke.Tuliishi kwa amani na furaha sana kama ndugu wa damu
Segerea maji ya "NUA" ni dili. Haya maji ya DAWASCO ndiyo wanaita maji ya "NUA". Mtu kukuruhusu utumie maji yake ya akiba kwenye madumu ya njano, ujue amekuheshimu sana.
Lakini mimi nilibahatika siku ya kwanza Jamaa wa selo namba 2 wakanionyesha madumu ya maji mengi sana kama 15 kisha wakaniambia ukihitaji kuoga au kufua maji chukua hapa kwa kuwa huna vyombo kiongozi wetu.
Nyie nyie nyieeeeee si mnakumbuka 19 September nilitoka mahakamani Kisutu usiku na kupelekwa gerezani usiku kwa mara ya kwanza? Mheshimiwa Hakimu akahairisha kesi hadi Jumatatu ya 23 September 2024 ambapo ilikuwa siku ya maandamano
Kule Jela siku hiyo mapema sana tuliambiwa kuwa hatutokwenda Mahakamani kwa sababu ya Maandamano yaliyotangazwa na CHADEMA.Siku hiyo hakuna Mahabusu gerezani alitoka kwenda Mahakama ya aina yeyote ile.
Hapo nje ya Jela siku hiyo Difenda za Manjagu zilikuwa Kibwena na Mamwela shazi mpaka jau,ulinzi na doria ni kama ikulu ya Marekani (white house)
Basi Jamaa zangu wa Segerea walikuwa wanashangilia sana wakisikia siondoki siku hiyo kwenda kupata dhamana Mahakamani.
Watu wa Ujambazini au Special Wing walitaka niendelee Kubakia nipige nao story na kilatu anielezee kuhusu kesi yake na namna ninavyoweza kumsaidia.muda ndiyo tatizo sasa.
Siku zile chache waliona hazitoshi kumaliza foleni yote kumskiliza kila mtu .
Siku ambayo siku pelekwa Mahakamani ndiyo kesi lilihairishwa kutoka 23 September hadi 26 September 2024 ambapo โremoval orderโ ilikuja gerezani nifikishwe Mahakamani Kisutu kusikiliza Uamuzi mdogo kuhusu dhamana yangu.
Binafsi nakumbuka siku hiyo nilifika uwanjani pamoja na Mahabusu wengine,tayari kwa ajili ya upekuzi na kuitika majina kisha mnasubiri majina ya mahakama mnayopelekwa kila mahabusu mmoja.
Niliposikia wanaitwa mahabusu wa kwenda Mahakama ya Kisutu, Kivukoni, Kinondoni, Ilala na mimi nilisogea nikijua ni safari moja na wenzangu.
Askari waliniambia mimi sipo kwenye safari ile bali nitafuatwa na askari maalum wa KM (Kikosi Maalum).Hivyo, sitopanda gari pamoja na wenzangu,baada ya muda wenzangu wote wakiwa wameshapelekwa katika Mahakama zao na mimi nikiwa nimebakia pekee yangu chini ya mti,ghafla niliona kundi la askaribhao wa KM linaingia lango Kuu la gereza.
Jamaa walikuwa Ntu za Mazoezi,wameshiba,warefu alafu wapo serious muda wote.
Kisha nikaitwa Boniyai.. Boniyai.. Boniyaiโฆ Twende sasa. Jamaa walionifuata walikuwa serious sana, kila mmoja nikimtizama usoni naona kabisa kuna maneno atakuwa kapewa kwamba mimi ni mtu mbaya sana
Kwanza mikononi nikala pingu yangu, Doh! kwa mara ya kwanza nikajiona nilivyokuwa napendeza na bangili za silver nzito mikononi mwangu ambazo zilikiwa zimekutanisha mikono yangu mbele ya uso wangu kama Jambazi au gaidi
Rohoni nikasema no sweat, yote maisha tu na Wahenga walisema ukiwa ngariba usiogope mkojo.
Siku hiyo Kisutu tulifika mapema sana. Saa 4 nilikuwa pale,kama kawaida yangu,ndani ya Mahabusu ya Mahakama za Kisutu nikiwa naendelea kupiga story na watu (mahabusu) waliokuja Mahakamani Kisutu kutokea Magereza Mengine ya Keko na Ukonga na kuwapa vituko vya Jela zao wakati naishi huko zamani.
Kushtuka ni saa 10 : 00 Jioni na bado sijaitwa Mahakamani kusikiliza uamuzi, machale yakanicheza hapa leo narudi tena Segerea. Nilipokwenda chumba namba moja cha Mahakama ya Kisutu baada ya mpambano wa hoja na vifungu vya kisheria, nilitakiwa kurudi tena Segerea kusubiri uamuzi kusomwa tena siku ya 01 October 2024.
Wakati mzuri sana Selo namba 2, Special Wing..! (GOOD MOMENT)
Ni hiyo siku ya 26 September 2024, akili yangu yote ilijua siku hiyo nitapewa dhamana kwa uamuzi wa Mahakama, Kisutu kwa hiyo asubuhi sikunywa uji wala sikubeba "paseli" kama wengine wanavyobeba chapati, bagia au maandazi kuja kula katika chumba cha mahabusu ya Mahakama pale Kisutu, Si unajua Watuhumiwa tukitoka gerezani haturuhusiwi kununua chakula cha kutoka nje pale Kisutu
Basi nishapangiwa zangu tarehe 01 October ndiyo ning'ae tena mbele ya Hakimu mfawidhi Mahakama ya Kisutu. Narudishwa zangu na Kikosi Maalum (KM) kama kawa ,kikosi kutoka Keko kinachokuja kunichukua Segerea na Basi langu moja likiwa na watu kama 20 hivi wote wapo serious na kazi na Mijegejo ya maana mkononi.
Si mlikuwa mnawaona nyie wenyewe?
Wengine wanapanda juu ya Jengo la Mahakama ya Kisutu. Wengine wamevaa soksi usoni, wamepiga groves mikononi na bunduki nzito mikononi ,basi miye taratibu njiani narudishwa zangu ktk makazi ya muda Segerea.
Siku hiyo ya 26 September 2024 nilirudishwa zangu gerezani muda ukiwa umeenda sana. Ni saa 2 usiku ndiyo tunatoka Mahakama ya Kisutu na tumboni sijaweka kitu tangu asubuhi
Basi kwa ujinga wangu wakufikiri ningeruhusiwa kwa dhamana siku hiyo sikula kitu, sasa ngoma imedunda na nina njaa kama Mama aliyetoka Kujifungua leba.
Jamaa wale wa Kikosi Maalum (KM) wamenifikisha salama. Wamenifungua pingu zao. Wamenikabidhi Ngome kisha wao wakasepa zao.Sasa Askari wa Segerea wananipeleka selo namba 2. Muda unaenda saa 3 usiku, siku hiyo.
Nakumbuka siku hiyo walikuwa wanamsisitiza Dereva awahi kuwarudisha Keko wawahi mechi ya Simba SC na Azam FC ambayo ilkuwa inachezwa Zanzibar
Pale selo namba 2 Jamaa zangu akina Chi, Lee, Sam ,Aboubakar, Kimaro na Njau ile naingia mlangoni kitu cha kwanza naona kila mmoja anakoroma. Duh! pozi lote hata la Kuulizia mkate na soda likaniisha.
Nikaingia kuoga chap na njaa yangu.Narudi kwenye kigodoro changu najisema wameshalala hawa wanakoroma, siyo vizuri kuwasumbua watu kwa kuwaamsha na huwaharibia usingizi wao.
Ukizingatia najua thamani ya Usingizi wa gerezani. Unaweza kuamshwa usiupate tena hadi asubuhi, kwa kujikuta unawaza familia yako au biashara zako nje zinaendaje.
Basi kinyonge sana, nikiwa na njaa kali sana, nikajilaza na kujifunika shuka langu. Kumbe washenzi
wale hawakuwa wamelala kweli aiseee.
Walinisikia tangu geti kubwa linafunguliwa na nikiwa naulizwa kwa sauti na Askari, Je nalala selo namba ngapi ..? na yule askari wa kutunza funguo.
Ghafla Jamaa zangu wakaamka kwa lelele wakisema kwa pamoja โWelcome Boniyaiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiโ
Kumbe walikuwa wanaigiza wamelala tu wahuni wale,lakini kwa sura zao na lile shangwe lao niliona kabisa Jamaa zangu walivyofurahi Mimi kunyimwa dhamana yangu ili kuendelea kuishi nao pale gerezani.
Daaaaaaaaah wananikubali na kunipenda sawa,Sasa ndiyo watake niendeleee kuwa gerezani?
Surprise kubwa kwangu ,kumbe Jamaa walibakisha chakula aiseeee,nasikia Aboubakar aliwaambia wenzie kuwa anahisi siachiwi kwa dhamana siku ile,
Jamaa wakaniwekea chakula aiseeee,chapati na kuku makange na Pepsi ya Take away. Upendo uliwoje..?
Jamaa wanafuraha kuniona kama vile nimeishi nao miaka 10, kumbe wiki kadhaa tu ndani ya Jela.
Mwingine ananifungulia soda na mwingine anatoa chapati, huku mwingine kaenda kunichukulia maji ya kunawa kwenye jagi na ndoo ya kunawia.
Kwa njaa yangu,nakula chapati na makange rosti huku nawasilimulia kilichotokea Mahakamani. Chi ananichekesha anasema, kuna watu walitaka kuchukua godoro langu mchana wakijua sirudi, yeye akawakataza kwa sababu alijua nitarudi tu.
Ukiwa selo namba 2,special wing huwezi kumuwaza anayekukomoa asikupe dhamana wala aliyekuleta gerezani , yani ni utani, furaha,vicheko na upendo tu.
Sasa mimi niliposhiba fadhila zangu ilikuwa nikuwaburudisha na utani wangu kama walionizoea nao,wasione nimerudi kinyonge. Kwanza nikasimama kisha nikapandisha bukta yangu juu (mayenu)
Si nikaanza kuporomosha show kwa kuimba wimbo wa DDC Mlimani Park Orchestra "nawashukuru wazazi wangu"
"Nawashukuru wazazi wangu wakati wowote
Ushauri wao umeniletea mafanikio mema
Sasa naishi na watu vizuri, eh
Sasa naishi na watu vizuri, eh-eh
Huku niliko wazazi wangu sina ndugu
Lakini kutokana na husia wenu wazazi wangu
Najiona kama niko nyumbani, eh
Najiona kama niko nyumbani, eh, mama
Nawashukuru wazazi wangu wakati wowote
Ushauri wao umeniletea mafanikio mema
Sasa naishi na watu vizuri, eh
Sasa naishi na watu vizuri, eh-eh
Huku niliko wazazi wangu sina ndugu
Lakini kutokana na husia wenu wazazi wangu
Najiona kama niko nyumbani, eh
Najiona kama niko nyumbani, eh, mama.."
Basi waswahili wenzagu wanaujua na wao wakajikuta tunaimba wote kwa furaha na kelele wimbo huo huku pembeni wale Wachina wanapiga ndoo na Bakuli kama "Drums", bila kujali muda wa kulala saa 3 : 00 Usiku ulikuwa umeshafika.
Unafanya mchezo nini? Uishi na watu mpaka wakumbuke jamaa kaondoka bila chakula, anaweza kurudi na njaa wakununulie chakula tena bila ya kuwa na mawasiliano nao kuwa utarudishwa tena.
Kwanini usijikute unawakumbuka wazazi wako kwa malezi mazuri ya kukufunza kuishi na watu vizuri na ukajikuta unaishi popote na mtu yeyote kama upo nyumbani ingali upo mbali ..?
Itaendeleaaaaa...!