VIDEO:
Serikali kupitia Wizara ya Afya imetangaza mpango wa kuhakikisha kuwa mifumo yote ya tiba asili nchini inajumuishwa rasmi katika mfumo wa afya ya msingi pamoja na Bima ya Afya kwa Wote ifikapo mwaka 2030.
Hatua hiyo imetangazwa leo, Alhamisi Novemba 19, 2026, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya dhifa ya uwekezaji katika dawa za tiba asili maarufu kama Asili Investment Gala.
Waziri Mchengerwa ameeleza kuwa miongoni mwa harakati kubwa zinazoendelea sasa hivi ni kuhakikisha kuwa tiba asili zilizofanyiwa tafiti na kudhibitishwa zinatambuliwa na mifumo yote ya afya na kujumuishwa kwenye bima ya afya ili wananchi waweze kuzipata bila vikwazo.
“Lakini pia serikali imekusudia katika hili ifikapo mwaka 2030 mifumo yote ya tiba asili iwe imejumuishwa katika afya ya msingi. Kwa hiyo moja ya harakati kubwa ambazo tunaendelea nazo ni sasa ni pamoja na kuijumuisha pia katika bima ya afya kwa wote lakini kuhakikisha kwamba mifumo yetu yote ya afya inaitambua tiba asili”, ameeleza.
Waziri Mchengerwa ametoa wito kwa wataalamu wa tiba asili ambao bado hawajasajili dawa zao kujitokeza mara moja ili zifanyiwe utafiti wa kisayansi na kudhibitishwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Bohari ya Dawa (MSD) na taasisi zingine zinazosimamiwa na Wizara ya Afya.
Akiangazia maandalizi ya Asili Investment Gala, Mchengerwa amebainisha kuwa dhifa hiyo sasa inatarajiwa kufanyika mwezi Aprili 2027 ikiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki 1,000 kutoka sekta mbalimbali za ndani na kimataifa.
Rais Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Arusha kupitia Uwanja wa ndege wa Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Katika ziara yake, Rais Samia anatarajiwa kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jeshi la Polisi Tanzania kwenye shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro, pamoja na kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Ushindi wa jasho kwenye mbio za magari! 🏎️🏆
Dereva wa timu ya Asas, Birdi, ametwaa taji la NRC na kukiri haikuwa rahisi. Mashabiki wa motorsport mnasemaje? 👇🏽 #BongoX
Tanzania inaendelea kushangaza dunia kwa utajiri wa maliasili! 🐒🌿
Wanasayansi wamegundua sokwe mtu (chimpanzees) wanaotumia zana za kazi kusini zaidi barani Afrika katika Hifadhi ya Msitu wa Loasi hapa Tanzania. Hii ni rekodi mpya ya kihistoria! Unafahamu hifadhi hii? 👇🏽
Kwa vipindi tofauti, watendaji kutoka Tanzania na Uganda wamekuwa wakijadili utekelezaji wa makubaliano yetu. Leo, nikiwa katika ziara nchini Uganda, nimekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wangu, Rais wa Uganda, Mheshimiwa Yoweri Museveni. Tumefarijika kuona hatua zilizopigwa katika utekelezaji wa makubaliano hayo, hususan katika sekta za biashara, miundombinu, nishati na usafirishaji.
Nimemweleza na kuikaribisha Uganda kuungana na Tanzania katika juhudi za kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, ikiwemo upanuzi wa bandari, ujenzi wa meli, barabara, reli ya kisasa na usafiri wa anga, ili kurahisisha upatikanaji wa masoko ya kikanda na kimataifa.
Aidha, nimempongeza Rais Museveni kwa hatua ya Uganda kuwa nchi ya kwanza kuanza ujenzi wa Ofisi za Ubalozi wake katika Mji wa Serikali wa Mtumba, jijini Dodoma, hatua inayotarajiwa kuhamasisha mataifa mengine kuwekeza katika eneo hilo.
Meli ya MV Mwanza ya Jijini Mwanza imeripotiwa kupoteza mwelekeo na kugonga miamba ya Bismarck wakati Nahodha akifanya jitihada za kutia nanga.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, baada ya Meli kugonga miamba hiyo, moshi mwingi ulianza kufuka na kusababisha hali ya taharuki.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa zilizoripotiwa kuhusu watu kujeruhiwa kutokana na tukio hilo. Taarifa zaidi kuhusu chanzo cha tukio na hali ya Meli hiyo zinatarajiwa kufahamika baadaye.
#KitengeUpdates
Sasa ni wakati wa kuokoa maisha! 🙏💔 Msanii Edu Boy anaomba msaada wa Tsh Milioni 30 kwa matibabu nchini India kutokana na uvimbe tumboni. 🇹🇿🇮🇳
Msaidie kupitia:
📱 Voda: 0752577415
🏦 CRDB: 0152782838500
Tushiriki kumsaidia! 👇
#EduBoy#Tanzania
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetoa miezi mitatu kwa wananchi wanaotumia namba za NIDA kuchukua vitambulisho vyao, ikieleza kuwa baada ya muda huo kumalizika, matumizi ya namba yatafutwa.
Shtuko la shule nzima kufaulu wanafunzi wawili tu darasa la saba: Mjadala mzito kuhusu sababu za matokeo hayo na ubora wa elimu. #ElimuTZ#Tanzania#BongoX
Kampuni ya Mawasiliano ya Yas Tanzania imezindua kampeni maalum ya miezi mitatu inayojulikana kama ‘Magifti ya Viwango’, itakayowapa Wateja wake kote nchini fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu, simu janja pamoja na gari jipya aina ya Jetour lenye thamani ya shilingi milioni 100.
Kampeni hiyo imezinduliwa leo, Novemba 17, 2026, Jijini Dar es salaam, huku ikilenga kuwashukuru Wateja wa Yas kwa kuendelea kuiamini kampuni hiyo na kuchangia ukuaji wake, huku ikiwapa nafasi ya kushinda zawadi kupitia ununuzi wa vifurushi, malipo ya huduma ya intaneti ya Fiber pamoja na marejesho ya mikopo ya vifaa vinavyotolewa na kampuni hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas Tanzania, Pierre Canton-Bacara amesema kampeni hiyo ni sehemu ya utamaduni wa kampuni wa kuthamini Wateja wake na kuwarudishia fadhila kutokana na uaminifu wao, akisisitiza kuwa mafanikio yaliyopatikana mwaka huu yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na Wateja.
Kampeni ya ‘Magifti ya Viwango’ inatarajiwa kuendelea katika kipindi cha mwisho wa mwaka 2026 hadi mwanzoni mwa mwaka 2027, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Yas za kuwathamini Wateja na kuimarisha uhusiano nao.
#MillardAyoUPDATES
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amefafanua kauli yake aliyowahi kuitoa miezi kadhaa iliyopita kuhusu namna anavyotamani kuzikwa pindi atakapofariki dunia, akisema baadhi ya Watu waliitafsiri vibaya kwa kudhani alimaanisha azikwe kwa taratibu za dini ya Kiislamu.
Akizungumza na AyoTV, Chalamila amesema yeye ni Mkristo Mkatoliki na kwamba alichomaanisha ni kutamani kuzikwa kwa haraka kama wanavyofanya Waislamu, ili kuepusha gharama kubwa za misiba zinazoweza kuziacha Familia katika hali ngumu kiuchumi.
Chalamila ameeleza kuwa msimamo huo ulitokana na tukio la kufiwa na Rafiki yake ambaye msiba wake ulidumu kwa wiki nzima na kutumia fedha nyingi, lakini baada ya maziko, Mtoto wa Marehemu alimtafuta akiomba msaada wa ada ya shule, jambo lililomuumiza na kumfanya kuhoji umuhimu wa kutumia gharama kubwa kwenye maziko huku Watoto wa Marehemu wakiachwa bila msaada.
Amesema jamii inapaswa kubadili mtazamo kuhusu matumizi ya fedha kwenye misiba, akieleza kuwa si busara kutumia mamilioni ya fedha kununua majeneza ya gharama kubwa na kuandaa maziko ya kifahari wakati Marehemu ameacha Watoto wanaohitaji elimu na mahitaji mengine muhimu.
#MillardAyoUPDATES
Umoja na maridhiano ndiyo nguzo yetu! 🇹🇿🤝🏽
Rais Samia ametangaza mpango wa kuunda Tume ya Maridhiano itakayoratibu mchakato wa Katiba kwa kushirikisha wadau wote. Njia ya mazungumzo ni bora zaidi! Mnaonaje? 👇🏽✨ #KatibaMpya#BongoX
Familia ya Mtoto aitwaye Faith Fredy mwenye umri wa miaka 13 ambaye ni Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Mkazi wa Makumbusho Jijini Dar es salaam, inatangaza kumtafuta Mtoto wao Faith baada ya kupotea tangu Novemba 10, 2026.
Taarifa ya Familia imeeleza kuwa Faith ambaye hana tatizo la kiafya, alitoweka nyumbani tangu Novemba 10 2026 alipotumwa Dukani kwenda kununua mahitaji mbalimbali ya nyumbani ambapo mara ya mwisho alikuwa amevaa gauni jeupe lenye vidoti vyeusi na sweta.
Familia yake imeomba Mtu yeyote atakayemuona atoe taarifa katika Kituo chochote cha Polisi au apige simu namba 0786782582 au 0773739499.
VIDEO:
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetangaza mpango wa muda mrefu wa kutumia maji ya bahari kupitia mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ili kukabili changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji wa DAWASA, Mhandisi Ndele Mengo, wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo, menejimenti ya DAWASA pamoja na wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa wilaya hiyo.
Mhandisi Mengo ameeleza kuwa katika mipango ya muda mrefu, DAWASA inalenga kuwashirikisha wawekezaji binafsi wenye nia na teknolojia ya kuchuja na kusafisha maji ya bahari na kisha kuiuzia DAWASA ili itawanyie wananchi maji hayo.
Mbali na mpango wa maji ya bahari, Mhandisi Mengo amebainisha kuwa DAWASA pia ipo katika hatua za mwisho za upembuzi yakinifu wa mradi mwingine mkubwa wa kutoa maji kutoka Mto Rufiji. Mradi huo, ambao mshauri elekezi ameshakamilisha takribani asilimia 90 ya kazi, utatekelezwa kwa awamu nne, ambapo awamu ya kwanza pekee itazalisha lita milioni 375 kwa siku na kuondoa karibu upungufu wote wa sasa.
Mvua zikianza kunyesha tu, baadhi ya mitaa yetu inageuka kuwa mito! 🌧️🌊
Wakati huu wa mvua za ngurumo, tahadhari ni muhimu sana hasa kwa wanaotumia barabara za mabondeni. Huko kwenu mvua zimeshaanza kunyesha au bado jua linawaka? 👇🏽☔ #Tanzania#BongoX
Watu wa Kahama zamu yenu imefika! Wakongwe wa Bongo Fleva wanatua Malex Hall Novemba 27 kwenye sherehe za miaka 30 ya muziki wetu! 🎶🔥
Viingilio vinaanzia elfu 50 tu. Wana Kahama mko tayari kuujaza ukumbi na kula burudani ya nguvu? 👇🏽🇹🇿 #BongoFleva#Kahama#BongoX