Katika kile kinachoonekana kuwa ni mkakati wake wa kuachana na kashkash za wanamuziki, mkurugenzi wa Twanga Pepeta Asha Baraka, ameamua kuja na mpango kazi ambao hakuwahi kuutumia hapo kabla.
BOFYA LINK KUSOMA ZAIDI https://t.co/M3aX4Xq3PP
Baada ya miaka 18 mfululizo ya kutamba na bendi za Dar es Salaam, hatimaye Ally Chocky ameamua kwenda Mwanza na kujiunga na bendi ya Super Kamanyola yenye maskani yake Villa Park Resort. https://t.co/6jT5j5zj1v
Mkurugenzi na mwimbaji wa Mapacha Wawatu Original, Khalid Chokoraa , amesema Ally Chocky ni dhahabu ambayo watu hawajui kuitumia. https://t.co/X8iIDa65fJ
Naam ile show Isha Mashauzi na nyota wake wa Mashauzi Classic pale Mombasa, Kenya katika sherehe za Eid el Fitr itakayofanyika ndani ya Talentos Beach Resort, imekaa mkao wa kula ambapo Idd Pili Jumamosi ya Juni 16 ni mlipuko wa burudani kwa kwenda... https://t.co/edR71kcgji
Kutakuwa na kimbembe cha kukabana koo mjini Tanga kati ya bendi za Msondo Ngoma, Malaika Band chini ya Christian Bella pamoja na msanii wa bongo fleva katika maonyesho matatu yatakayofanyika Idd Mosi na Idd Pili. https://t.co/tuihG1p3im
Adam Mbombole (pichani) wa waimbaji safi kabisa kwenye dansi la kizazi kipya, amezitaja dosari tano za rais wa Smart Band ya Tabora – J Four Sukari. https://t.co/VLbSMco7SB
Rapa pekee wa FM Academia HILTER amezushiwa kifo cha ajali ya piki piki wakati ukweli ni kwamba msanii huyo yu hai – mzima wa afya.
#FMACADEMIA#hitler https://t.co/KR3OkSk7so
Wasanii sita miongoni mwa wanamuziki waliokwenda kuasisi Smart Band mapema mwaka huu, wameachana na bendi hiyo ya mjini Tabora.
Baadhi ya wasanii waliotajwa ni Frank Kabatano, Adam Mbombole na mpiga bass Evans.
#jfoursukari#smartband https://t.co/aBVOAKsVfh
Inaweza ikakuwia vigumu kuamini, lakini ndiyo hivyo tena, akiwa anatimiza umri wa miaka 68, miaka 36 ya kuwepo kwenye fani za michezo na burudani, hatimaye Mzee Juma Mbizo ameamua kuingia studio kwa mara kwanza na kufanya ‘kolabo’ na mwanae H-Mbizo. https://t.co/OJmyHs9C9Q
Mwimbaji mwenye sauti tamu na mwenye tungo bora kabisa katika muziki wa dansi, Chaz Baba amesema safari yake kurejea Twanga Pepeta bado haijaiva. https://t.co/xSecotz5RR
Cristiano Ronaldo amezidi kumfagilia kinda wa Manchester United Marcus Rashford na kusema huyo ni staa ajaye baada ya ufalme wa Ronaldo na Messi. https://t.co/Z2ha945bgg
Jimmy Gola si jina geni kwa mashabiki wa muziki wa dansi la kizazi kipya ambapo kwa miaka mingi amekuwa nguzo ya safu ya uimbaji ya Mapacha Music Band inayoongozwa na Jose Mara. https://t.co/px0aPJCZXX