Mwenyezi Mungu mponye Fr #Kitima
Watu wasiojulikana wananguvu sana, wanaua na kuumiza wa vyama vya upinzani,sasa wameingia kwa viongozi wa Dini,huko mlikoingia, sasa mtajulikana tu na ndio mwisho wenu!
Hatuwezi kuendelea kuishi #Tanzania kwa woga, eti watu wasiojulikana
Kwa Hali ilivyo, mtawala ameshindwa hoja za upinzani na hivyo kutumia madaraka vibaya kuwaumiza!
Kwakuwa ni mbabe, vifute vyama vingi vya siasa, futa uchaguzi, endelea kutawala milele, ili tuepushe watu kuumia na kukosa raha katika nchi yao!
Ipo siku si nyingi,Miti itaongea!
Nawaza kwa sauti!
Je ni sababu zipi zinakupa Uhaini?
Je ukiwa na mashtaka ya uhaini, hairuhusiwi watu kufika Mahakamani?
Je ni nani mwenye haki ya kuzuia watu kuingia Mahakamani?
Je anayeharibu Amani ni aliyepiga mtu asiye na silaha Au yule anayedai haki?!
Je Uhuru ni nini?
Kutumia Police kuumiza RAIA wanaodai haki, ipo siku kibao kitakugeukia na utakosa wa kumlaumu!
Polisi ni Taasisi ya kitaalam na inapaswa kuheshimika, kuitumia kulinda maslahi binafsi ya mtawala ni matumizi mabaya ya madaraka, RAIA watachoka!
Acheni kuharibu Police!
Acha ubabe!
Ukiwa na Bunduki unaweza kujihisi ni mbabe sana kila kiumbe kinakuogopa, unasahau ipo siku risasi inagoma kutoka Au risasi zimeisha, jitu lipo tu!
Risasi 16 mwilini, bado yupo tu!
Nenda kwa tahadhali, utajeruhiwa, Bunduki sio fimbo!!
Kuna Giza mbele!
Chama cha siasa kinatekeleza majukumu yake kufanya mkutano wa hadhara, unatumia nguvu kuwazuia mbele ya umati wa watu wasiongee;
Je, hapo unalinda amani?!
Je, umma ukiamua vinginevyo, utabeba madhara?!
Amani ni Tenda la Haki
Hoja za siasa hazipigwi rungu!
Swali la kizushi..
Mvua inanyesha, anakukaribisha kwao ujikinge, Jamaa ni mbakaji mzoefu 2019, 2020, 2024 na zote amelalamikiwa, lakini hajakoma na wanaobakwa wamekuwa wakiamini labda amejirekebisha, wakiingia kwake, imekula kwao!
Je, utakwenda kwake??!
Mbakaji (unamjua)..
Good Friday!
Leo watawala wanampa mashtaka ya uongo Yesu Kristo na kuhukumiwa kuteswa hadi kufa!
Kwa kifo chake Msalabani, binaadam tumekombolewa!
Waliomhukumu wao walikufa, Ila Yesu bado anaishi!
Watakupa mashtaka ya uongo Leo ili uawe, hautakufa Bali wao ndio watakufa!
Magari yaliyopo Barabarani yanaonekana ya kifahari na mazima!
Huwa mkinunua mapya, ya zamani yanakwenda wapi?!
Je, haya mapya yanaumuhimu gani kulinganisha na mahitaji ya pesa Huduma za jamiii?!
Vijana #Tanzania mnalifahamu hili?!
@bunge_tz
@ortamisemitz
@ukaguziTanzania
Hizi Akili ndizo wanaongoza #Tanzania !! 😇
Usiseme ni mawazo yake, Lahasha! Ni za @ccm_tanzania kwakuwa anaongea kwa mamlaka ya chama na usishangae kesho akalamba uteuzi, ndio zao hizo!!
@tanpol wale watu wasiojulikana wanaopoteza wengine, wameanza kujitaja, msikae kimya!
Pasaka njema huku ukitafakari kuwa makini, usichague Mwizi maana walio wengi wanaendelea kufanya makosa ya kuchagua wezi!
#Tanzania kuwa makini na wezi, hujifanya bora wakati wa uchaguzi!!
Chini kushoto ni BenjaminMkapa Stadium Viti 60,000 Ujenzi US$56million,ulizinduliwa Mwaka 2007.
19/03/2024 Serikali imesaini kujenga uwanjaArusha Viti 30,000 kwa Tshd286bn (US$112million)
Sijaelewa hizi hesabu!
@NdumbaroDamas@TZMsemajiMkuu@ukaguziTanzania@Tanfootball
Rais alisema ‘wakati mwingine DPP anapigiwa simu na kwa Mamlaka Kikatiba, anafuta Kesi!’
Leo DPP amefuta Kesi ambayo yeye hakupeleka Mahakamani hadi aliyetendewa ukatili kuamua kushtaki, lakini DPP amefuta!
Ubaguzi kati ya watawala na wananchi!
@TZMsemajiMkuu tunahitaji maelezo
Tumefurahi kumuona VP na afya njema.
VP ni wa wananchi, wanahaki kuhoji alipo,Serikali iwe inatoa Ratiba mapema.
Maelezo ya VP yanaacha wazi mjadala..
Kazi za VP zipo Kikatiba, KAZI MAALUM ni ipi na wapi?!
Je inalipwa na Serikali?!
Mama Leo Kanisani hakuwapo!!
@TZMsemajiMkuu
Hizi cinema Mjengoni Dodoma ni sawa na kikao cha Nyani kumlalamikia mwizi wa Ndizi na kudai akamatwe!
Kuweni makini;anayelalamikiwa kikaoni sio Nyani,yeye anajiona ni Mmiliki waShamba!
Tamthilia ijayo mtanielewa vizuri!
#Tanzania ni yetu sote, punguzeni Tamthilia Mjengoni!
Ameongea Askofu mmoja tu kumuita Mama wa Taifa, wote wanafurahi na kuiita ni sauti ya Wananchi na sauti ya Mungu!
Wameongeza Maaskofu wote wa TEC kutahadhalisha Uwekezaji wa Bandari, wameambiwa wasichanganye Dini na siasa, hiyo ni sauti yao binafsi, waache!
Cheap popularity!
Baba wa Taifa hakuombwa akiwa Rais!
Kumuomba Rais aliyepo Madarakani akubali kuitwa Mama wa Taifa, inatafsiri mbali zaidi!
Inawezekana wanapendekeza kiuchawa ili waonekane wanampenda sana, lakini ndio wanamfikishia ujumbe wa kumtaka Apumzike!
mtego huo!!
Nimemaliza!
@Tanfootball Mjifunze promo toka @SimbaSCTanzania na @Yanga1935.
Haiwezekani #TaifaStars inacheza leo,Watu hawajui!
Mechi haionyeshwi Tv yoyote!
Ingekuwa ni hizo timu zetu, promo yake tu, Tvs leo zingegombea haki ya matangazo!
Taifa Stars ni yetu sote na Sio TFF Pekee!