RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIZUNGUMZA TANGANYIKA PACKERS
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi CCM, katika Viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar leo Agosti 28.2025.
Katika kazi, Ikulu, Chamwino leo nilipata pia wasaa wa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Anyisile Mwabukusi.
Simba SC imetangaza kumsajili Selemani Mwalimu kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Wydad Casablanca ya nchini Morocco.
Kabla ya kujiunga na Wydad Mwalimu alikuwa akiichezea Fountain Gate.
Maelfu ya wanachama, wafuasi na mashabiki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwa katika shamrashamra za uzinduzi wa kampeni za mgombea wa Urais wa chama hicho, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, zinazofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi, Agosti 28, 2025.
Leo nimepata heshima kubwa ya kutunukiwa Tuzo Maalum ya Heshima na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama njia ya kutambua kazi kubwa inayoendelea kufanywa kuimarisha ustawi wa wananchi na maendeleo ya Taifa. Sauti ya Bunge ni sauti ya wananchi. Ahsanteni sana.
Hakika, kidole kimoja hakivunji chawa. Mafanikio tunayojivunia leo si nguvu, uhodari au maarifa yangu pekee, bali ni matokeo ya mipango mbalimbali ya nchi yetu na maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025. Aidha, ni matunda ya kazi kubwa inayofanywa na Bunge letu ya kuisimamia na kuishauri Serikali.
Nimepokea tuzo hii kwa niaba ya Watanzania wote. Ninawashukuru nyote kwa kazi kubwa tunayoendelea kuifanya kwa pamoja kuleta maendeleo kwa Taifa letu, huku tukibaki kuwa wamoja, wenye amani na mshikamano.