@bbcswahili Nchi iliyo barikiwa kila kitu hapa duniani ni TANZANIA
ardhi nzuri,rutuba na yakutosha
Bahari
Maziwa
Milima
Mito
Mabwawa asili
Hewa nzuri
Good Location
Lugha moja kiswahili
Umoja
Nchi yetu ni baraka kwa Mungu
🇹🇿🇹🇿🇹🇿
Mayele🗣
"Nimeona club ya yanga wamenipost kwenye page yao, leo hii wakionyesha vile wapo proud na mimi, ndio hivi dunia ilivyo, club ambayo nilitoka kwa uchungu na matatizo ya kujaa miguu kama vile hakuna jema niliwahi kufanya, sitawahi kupona kwenye hili💔"
#PICHA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Matukio tofauti ya picha alipowasili katika Uwanja wa Ndege Mkoani Iringa ambapo anatarajiwa kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yatakayofanyika Mkoani Njombe Leo Mei 1, 2026. #MillardAyoUPDATES
Kheri ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Leo nimeungana na wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi mkoani Njombe katika maadhimisho ya siku hii kitaifa, ambayo mwaka huu imefungamanishwa na utekelezaji wa Dira ya 2050 unaoanza Julai 1. Hii ni hatua ya kimkakati inayolenga kuelekeza nguvu kazi ya Taifa katika kujenga uchumi shindani, jumuishi na endelevu.
Ninampongeza kila mfanyakazi kwani mafanikio tunayojivunia leo ni matokeo ya juhudi za pamoja katika sekta zote. Serikali yenu itaendelea kuimarisha fursa za ajira, kupanua fursa za kiuchumi, kuboresha mazingira na maslahi ya wafanyakazi, pamoja na kurasimisha sekta isiyo rasmi ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata kazi yenye staha, inayozingatia haki, usalama na ustawi.
Ili kufikia malengo hayo tunahitaji dhamira ya pamoja, kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na weledi wa hali ya juu, huku tukidumisha amani, umoja na mshikamano wa Taifa letu.
Faith does not separate the spiritual from the social. It gives Christians the strength to interact with the world and to respond to the needs of others, especially the weakest. What is needed for the salvation of a community is a communal commitment, which integrates the spiritual and moral dimensions of the Gospel in the heart of local institutions and structures, making them instruments for the common good, not places of conflict, self-interest, or sterile struggles. #ApostolicJourney #Cameroon
When we seem to be sinking, overcome by adverse forces, when everything appears bleak and we feel alone and weak, Jesus is always with us, stronger than any power of evil. In every storm, He comes to us and repeats: “I am here with you: do not be afraid.” With Him, we can get up after every fall and not allow ourselves to be stopped by any tempest. We therefore advance with courage and trust. #ApostolicJourney #Cameroon https://t.co/ANgV1LQAjr
Nchi yetu imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa kwanza barani Afrika wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Shirikisho la Jumuiya ya Madaktari wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (WFNS) ambao leo nimeufungua jijini Dar es Salaam. Uamuzi huu unadhihirisha imani kubwa katika maendeleo yetu na utayari wetu katika kuimarisha zaidi huduma za afya, hususan huduma za kibingwa na ubingwa bobezi.
Matokeo ya kazi kubwa tuliyofanya katika miaka mitano iliyopita katika huduma za afya za kibingwa na ubingwa bobezi yanaonekana ambapo;-
1. Hospitali zinazofanya upasuaji wa kibingwa wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu zimeongezeka kutoka 2 hadi 7.
2. Madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu wameongezeka kutoka 12 hadi 37.
3. Tumeongeza kwa kiasi kikubwa vifaa muhimu kama MRI, CT-Scan na X-ray.
Uwekezaji huu umeifanya Tanzania kuwa moja ya nchi chache Afrika zenye uwezo mkubwa wa kufanya upasuaji huo, na sasa inahudumia wagonjwa kutoka nje ya nchi.
Ninashukuru Chama cha Madaktari wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu Tanzania kwa tuzo mliyonipa, hakika, hii ni heshima yetu sote. Serikali yetu itaendelea kushirikiana na taasisi za kikanda na kimataifa kuimarisha huduma za afya kwa kuzifanya kuwa bora, nafuu na za uhakika ili kuokoa maisha ya wananchi na kurejesha tumaini kwa jamii.
#Peace is not something we must invent: it is something we must embrace by accepting our neighbor as a brother or sister. We do not choose our brothers and sisters: we must simply accept one another! We are one family, inhabiting the same home: this wonderful planet that ancient cultures have cared for over millennia. #ApostolicJourney #Cameroon
Mtoto mdogo ameibua hisia na kuvutia maelfu ya Watu baada ya kuonyesha ujasiri wa kipekee kwa kumkimbilia Papa Leo XIV mara baada ya ibada ya Misa nchini Cameroon.
Katika tukio hilo, mtoto huyo ameonekana kuvuka eneo la usalama bila woga na kumfikia Papa, hatua iliyowashangaza walinzi pamoja na waumini waliokuwepo.
Badala ya taharuki, Papa alionekana kumkaribisha kwa utulivu na upendo, akionesha ishara ya ukarimu na kujali, jambo lililowagusa wengi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo.
Wengi mitandaoni wamesifu ujasiri wa mtoto huyo, wakieleza kuwa kitendo chake kinaonyesha imani ya dhati na moyo wa kumwamini kiongozi huyo wa dini, huku wengine wakivutiwa na namna Papa alivyolipokea tukio hilo kwa upole na busara.
Tukio hilo sasa limegeuka kuwa gumzo, likitafsiriwa kama picha ya uhusiano wa karibu kati ya viongozi wa dini na waumini wao, hasa watoto.
#MillardAyoUPDATES