Serikali itaendelea kutekeleza Programu ya MBT kwa miaka mitano kuanzia 2025/2026 hadi 2029/2030 kwa lengo la kuongeza ushiriki wa wachimbaji wadogo, wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum katika fursa za sekta ya madini.
#BajetiMadini
Tume ya Madini itaendelea kufanya ukaguzi wa afya, usalama na mazingira katika migodi yote, ikiwemo mabwawa ya topetaka, miambataka na maghala ya baruti ili kuhakikisha uchimbaji unakuwa salama na endelevu.
#BajetiMadini
Kupitia Mpango wa MSEAP 2025β2030, Serikali itahakikisha shughuli za madini zinafanyika kwa kuzingatia kanuni za mazingira, jamii na utawala bora ili kulinda mazingira na kukuza uchumi endelevu.
#BajetiMadini
Katika kujenga taifa lenye wataalamu wa madini,Wizara imetenga bajeti maalum ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta ya madini kwa kuwasomesha ndani na nje ya nchi.
#BajetiMadini