Oubin Kramo alikuwa bora sana alipotoka ila amepatwa na majeraha pamoja na kushindwa kudeliver akiwa Msimbazi, anaungana na nyota wengi bora waliotoka kwao wakiwa bora ila wakadrop wakiwa Simba.
Mtazame hata Jean Baleke nyakati za mwisho alishaanza kupoteza makali yake, mkumbuke hata Pape Ousmane Sakho alishaanza kupoteza makali yake mwishoni, Peter Banda alikuwa na majeraha mengi na akashindwa kuperform.
Talent kama Augustine Okrah nae alianza kudrop siku hadi siku tofauti na alivyokuja na akaondoka kwa kigezo cha mambo ya nje ya uwanja ila kwasasa anauwasha ndani ya Yanga na husikii mambo ya nje ya uwanja, Jonas Mkude ni kama amezaliwa upya Jangwani na anaonesha.
Mchezaji anayekaa benchi Simba akipewa dakika siku huoni akikupa mechi bora tofauti na aliyempisha ila ukienda Jangwani Mchezaji anayeketi bench hata mechi 10+ bado akiingia atadeliver kwa ubora mkubwa, kuna maswali hapa.
Maswali ya kujiuliza ni kama yafuatayo.
1- Kwanini kuna changamoto za majeraha sana ndani ya Simba? Na Mchezaji akirejea sio yule tena.
2- Kwanini wachezaji wengi wakija Simba na ubora wao, wengi wanaondoka wakiwa wamefeli kabisa?
3- Mchezaji akikaa bench Simba bila kucheza, akipewa nafasi ni kama hakuwahi kucheza mpira maishani mwake?
Nadhani hili suala linaumiza sana kichwa.
Shamrashamra za uzinduzi wa hamasa zimeanzia kwenye Tawi la Karume Unstoppable tukisoma magazeti yenye habari za Simba.
ππππ ππ ππππππ: ππππππππ ππππππ. #VitaYaKisasi#WenyeNchi#NguvuMoja
"Uwanja wa Mkapa unahitaji wastani wa taa za LED 300 kufanya kazi zake ipasavyo. Gharama ya taa moja ya LED inakadiriwa kufikia kiasi cha shilingi za Tanzania milioni 12. Kwa sababu hiyo, gharama ya taa peke yake inaweza kufika takribani shilingi milioni 360." @ezekiel_kamwaga