Sense Internationa Tanzania ni shirika lisilokuwa la kiserikali ambalo linalenga kuhakikisha watu wasioona na wenye ulemavu mchanganyiko wanajumuishwa katika shughuli za maendeleo na wanakuwa sehemu ya mipango ya maendeleo bila kuachwa nyuma kutokana na changamoto ya ulemavu.
Leo tunaadhimisha ๐๐ข๐ค๐ฎ ๐ฒ๐ ๐๐๐ฆ๐ kwa kuwapongeza na kuwashukuru kina mama wote kwa upendo, uvumilivu na nguvu kubwa wanazozionesha kila siku katika malezi ya watoto wao. ๐
Kwa kina mama wenye watoto wenye uziwikutoona, tunatambua mchango wenu mkubwa katika kuhakikisha watoto wanapata huduma, malezi na mazingira yanayowawezesha kufikia ndoto zao. Ninyi ni chanzo cha matumaini, faraja na maendeleo kwa watoto wenu.
"Kwa sasa wazazi wanawaleta watoto hospitali kwa ajili ya kufanyiwa ubainishaji, ni vizuri tukaanza utaratibu wa sisi kwenda mtaani ili kuwafikia watoto wengi zaidi"
Dkt. Isabella Ipopo
Mganga Mfawidhi - Zahanati Mbagala Kizuiani.
Siku ya Karume ni fursa ya kukumbuka mchango wa Hayati Abeid Amani Karume katika kujenga jamii yenye usawa na mshikamano.
Sense Tanzania tunaendelea kufanya kazi ya kuwawezesha watoto na watu wenye uziwikutoona kupata haki zao za elimu, afya, na ushiriki katika jamii.
Kupitia mradi wa CADiR, walimu wataendelea kuimarishwa kwa mafunzo na mbinu bora za ufundishaji ili kuhakikisha watoto wenye uziwikutoona wanapata fursa sawa ya kujifunza, kukua na kushiriki kikamilifu katika elimu.
#ElimuJumuishi#CADiR#Deafblindness#UsawaKwenyeElimu
๐๐๐ค๐ฎ๐ง๐ ๐๐ฅ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐ฃ๐ฎ๐ฆ๐ฎ๐ข๐ฌ๐ก๐ข ๐๐ข๐ฅ๐ ๐ฐ๐๐ฅ๐ข๐ฆ๐ฎ ๐ฐ๐๐ฅ๐ข๐จ๐ฐ๐๐ณ๐๐ฌ๐ก๐ฐ๐. ๐ฑ๐
Katika mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa CADiR, maandalizi ya mafunzo kwa walimu kutoka shule 10 zinazoshirikiana kwa karibu na mradi yanaendelea kuimarishwa.
Katika picha hizi, walimu wa Shule ya Msingi Lukuledi Maalum iliyopo Masasi, Mtwara, wanashiriki majadiliano ya kina kuhusu uziwikutoona (Deafblindness), ikiwemo kuelewa viashiria vyake na namna ya kuwabaini watoto wenye hali hii shuleni..
Moja ya mafanikio ya mradi wa Task Order 51 tuliokuwa tunautekeleza kwa mikoa ya Shinyanga na Mwanza ni kuwawezesha wazazi wa watoto wenye ulemavu kiuchumi kwa kuwapatia msaada wa kifedha unaowawezesha kuanzisha biashara ndogondogo ili waweze kumudu gharama za shule za watoto wao
Ili kufikia jukwaa hili, tafadhali bonyeza kiungo (link) kilichopo kwenye wasifu (bio), kisha chagua "Global Deafblindness Resource Hub". Utapelekwa moja kwa moja kwenye mtandao huo.
Karibu kwenye Global Deafblindness Resource Hub, jukwaa maalum lililoundwa mahsusi kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Kupitia mtandao huu, utapata maudhui mbalimbali ya kielimu na kijamii, ikiwemo video na makala za maandishi.
Maudhui haya yameandaliwa kwa lengo la kutoa msaada na mwongozo kwa watu wenye ulemavu, wazazi au walezi wa watoto wenye ulemavu, pamoja na walimu wanaofundisha katika vitengo maalum vya elimu jumuishi.