@EsirEid@TaasisiMoyoJKCI Hawa watu Wana shida, mzee wangu alipata stroke saa 6 usiku akakata kauli lakini daktari alikuja kumuona jioni saa 12,longo longo nyingi mpaka wakamuhamisha mloganzila hakuchukua siku nyingi akafariki,kiufupi alikuwa mzima lakini the point nimempeleka jkci ulikuwa mwisho wake.
Inasikitisha kuona bado kuna viongozi wanaamini siasa za kufuta upinzani badala ya kushindana kwa ideas na sera. Tanzania ni nchi ya vyama vingi na CHADEMA si adui wa taifa bali ni sehemu ya demokrasia ya nchi hii
Kama chama tawala kinaamini kinakubalika kwa wananchi, kishindane kwa hoja na utendaji wake sio kutumia vitisho, kesi na propaganda dhidi ya wapinzani. Ukweli ni mchungu kwa Ccm kadri wanavyojaribu kuibana CHADEMA ndivyo wanavyoonyesha wana hofu na nguvu yake kwa wananchi
Demokrasia haiimarishwi kwa kufuta wanaokukosoa tunatakiwa kuwa ña watu wenye utambuzi wa kwamba vyama vya kisiasa ni kuvumilia tofauti za mawazo na kushindana kwenye hoja na sera
Leo tunaposherehekea Sikukuu za Uhuru, ni muhimu kukumbuka kwamba hatuna nchi nyingine zaidi ya hii. Hii ni nchi yetu, hii ni ardhi yetu, na hii ni haki yetu ya kuzaliwa hapa.
Tumepewa mamlaka ya kupigania na kulinda haki zetu, kuhakikisha kwamba tunanufaika na kila rasilimali inayojaa kwenye nchi hii.
Nchi yetu ni tajiri, imejaa fursa na uwezo mkubwa, na sisi vijana ndio miongoni mwa walio na nguvu ya kuitumia. Tunapoishi na kufanya kazi hapa, tunastahili haki ya kupata kila kilicho bora, Hatufai kuwa maskini kwenye nchi yenye rasilimali tele.
mwendokasi ni kielelezo kimoja kati ya vingi kwamba walioko madarakani hawana nia, uwezo wala mbinu za kutatua matatizo yanayowakabili w'nchi. these people want power for its own sake. their sole preoccupation ni kujitajirisha. hawawezi kuongoza, ufisadi tu ndiyo kitu wanaweza!
“Tujenge utamaduni wa kudhibiti viongozi wetu kama wanavunja sheria ya nchi (Katiba) tusiogope, mkianza, mkiwa na woga, I’m, I promise you, mtatawaliwa na dictators, (huku anacheka), I promise you, mkiogopa ogopa namna hii, nyinyi, wabunge, nani, wote mkiogopa ogopa, mkisema mzee wanakuwa wakali, then you are making it absolutely certain, you will be under a dictatorship” - Mwl, Julius k. Nyerere
Kiasi kidogo cha halali chenye amani na uhuru wa kuishi na kuabudu ni bora zaidi kuliko haramu inayokuondolea uhuru huo. Vijana, tuendelee kupambana kwa njia halali; kilichoandikwa, kimeandikwa. Mwisho wa siku, kaburi halina VIP, na maisha ya dunia hayakuwa ila ni pambo la muda mfupi tu.
Ngoja nikuelekeze kitu kimoja ambacho unahitaji kukielewa wewe na CCM wenzako.
Hakuna mtu anaevionea hivi vyama Wivu kwa kushiriki huu Uchaguzi ila kila mtu mwenye kiu ya kuona Taifa hili linasonga mbele alikuwa anatakani vyama vyote visimame na kudai haki ya pamoja kama Taifa.
Kutokushiriki kwao CCM wasingeweza kwenda kwenye Uchaguzi usio na vyama pinzani bali wangelazimika kufanya marekebisho hata pasipo kupenda ili Taifa lisonge mbele.
Kwa sasa vyama vilivyoshiriki maana yake ni kuhalalisha uozo wa muda mrefu kwenye Chaguzi za nchi ambao umekuwa ukionekana wazi wazi kwa mtu yeyote mwenye akili timamu.
Kinachokufanya uone Lema anaona wivu ni Ubinafsi wako wa kuangalia ulipo wewe tu bila kujali ni watu wangapi ambao wamekwama au wanateseka na haya yanayoyalilia.
Tutaendelea kuwa na Taifa Maskini kwa kuwa na aina ya vijana kama wewe ambao kwao maendeleo yao ndip kitu pekee wanachoishi kukitafuta.
Nakukumbusha baada ya wewe kuna watoto na wajukuu zako na nina uhakika hautaweza kuishi nao au kuwa nguvu yao siku zote. Kuna siku utakuwa hauna nguvu na watakuwa wanufaika wa huo mfumo ambao leo unaona unakuchekesha.
Endelea kucheka na kutabasamu hata mifumo ya nchi yako ikiwa mibovu lakini kumbuka hili Taifa limejengwa na watu ambao hawakuwa Wabinafsi na Tanzania ilikuwa kiu yao kuliko Vyama vya siasa.
Wasalimie sana hapo Iringa siku moja nitakuja kukutembelea tuongee zaidi ndugu yangu. 🤙🏾
Amani ni tunda la kutenda HAKI. HAKI itendeke, ionekane inatendeka kwa wote, popote, wakati wote.
Kilichotakiwa kuwa TUNU ya kwanza nchi hii ni HAKI.
Hayo mengine yote tutayapata tena kwa ziada.