Tukio hilo lilitokea Februari 1, 2006 wakati Juventus ilipokutana na Roma kwenye mchezo wa Coppa Italia nchini Italia.
Dakika ya 18 pekee ya mchezo huo, Zlatan pamoja na kiungo wa Roma Olivier Dacourt walitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kutokea kwa mvutano mkali uliowashirikisha wote wawili.
Hapa Zlatan Alizuga kama hakijatokea Kitu😅😅
🚨 UPDATE ⚽
Klabu ya Young Africans imeagizwa na FIFA kulipa jumla ya $43,000 pamoja na riba kwa klabu ya TP Mazembe, kufuatia mzozo uliotokana na dili la usajili wa mshambuliaji Jean Baleke.
FIFA imeongeza faini ya $10,000 pamoja na gharama za kisheria za $5,000.
Kuna riba ya 5% ya kila mwaka kwenye deni hilo.
Ikiwa Yanga itashindwa kulipa kiasi hicho ndani ya siku 45, wanakabiliwa na hatari ya kufungiwa kusajili wachezaji kwa madirisha matatu (3) mfululizo, ndani na nje ya nchi.
Cc @MickyJnr__ African Football Journalist
🚨Tuliwahi kudanganywa kwamba Simba na Yanga hazina faida,ukiwekeza pale unatoa na sio kuingiza na tuliishi kwenye imani hiyo kwa miaka mingi bila kujua ukweli
Kwa bahati nzuri Jayruty amekuja kutuonyesha namna gani hawa matajiri kina GSM na Mo dewj wanapata faida kupitia hizi mbili za Simba
Jayruty amefanya kazi na Simba kwa msimu mmoja tu na bado haujaisha ila amelata mabadiliko makubwa kuliko hawa matajiri wengine ambao wamekaa kwenye hizi timu kwa miaka nenda rudi
Jayruty anawalipa Simba Billion 5.6 kwa mwaka na kwa mujibu wa mkataba tayari fedha hizo ameshazitoa kwasababu zinatakiwa kutolewa kwa mwaka kwanzia posho na fedha ya mkataba wote wa jezi kwa msimu mmoja
Jayruty anatoa hizo Billion 5.6 lakini bado kanunua Irriza ambayo ni tofauti na hiyo Billion 5.6 ambazo anatoa kila mwaka
Jayruty kanunua mchezaji kama ambavyo mkataba wao unasema,yani, kwa mwaka mmoja, Jayruty kanunua bus ambalo litagarimu zaidi ya Billion 1.3 hadi kukamilika na bado kanunua mchezaji na bado ile Billion 5.6 ambazo anatakiwa kulipa kwa msimu mmoja ziko pale pale
Haya yote Jayruty kayafanya kwa msimu mmoja tu na hapa ndio mjue Jayruty hayupo Simba ili kupata peke yake ila yupo Simba kwa ajili ya kuwasaidia Simba waweze kupiga hatua kubwa na kuendana na mazingira ya kisasa duniani
Jayruty amekuja kuiokoa simba,kuitoa kwenye giza na kuipeleka kwenye mwanga,njia pekee ya kumlipa Jayruty ni kumsaport kwa kununua bidhaa original za Simba ambazo anatengeneza yeye kwasababu faida ambayo anaipata,anairudisha hapo hapo Simba ili kuifanya iwe timu ya kisasa zaidi.
🎯🎯🎯⚽Kuna kipindi Mzamiru Yassin aliwahi kusema kuwa wachezaji wa kigeni wanapokuja Simba, hupatiwa darasa maalum la kuwafundisha kuhusu klabu hiyo.
Hupewa maelezo kuhusu utamaduni wa Simba, historia yake, mafanikio yake na mambo mengine mengi yanayoihusu klabu.
Moja ya icon na magwiji wanaotajwa na kuonyeshwa kupitia picha na video ni John Bocco.
Ndiyo maana ukitazama picha za Mpanzu na Kante, utaona walivyokodoa macho wakimtazama mmoja wa manahodha waliofanikiwa zaidi katika historia ya Simba.
Kante na Mpanzu wanawaza na kujiuliza iliwezekana vipi, “Katika misimu yake yote, magoli 155 aliyafungaje?”
Sikushangaa kuona picha nyingine ya Chama akiwa na mwalimu akielezewa kuhusu makubwa aliyoyafanya John Bocco akiwa Simba.
John Raphael Bocco, katika kipindi chake cha soka kuanzia mwaka 2008 hadi 2025, amefunga mabao 155.
Takwimu zinamtaja kama mmoja wa wafungaji bora wa muda wote nchini Tanzania, akiwa ameweka rekodi ya kipekee mbele ya wengi waliomtangulia na wanaocheza kwa sasa.
Katika miaka 17 ya kucheza Ligi Kuu, amezitumikia Azam FC, Simba SC na JKT Tanzania.
Kwa upande mwingine, Mohamed Hussein “Mmachinga” alitumia miaka 12 kufunga mabao 153 kati ya mwaka 1993 na 2005.
Hivyo, John Bocco amemzidi kwa mabao mawili pekee.
*papaa* 🔥
◾️Winga wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Ghana 🇬🇭 Antoine Semenyo ameweka wazi kwanini alichagua kuiwakilisha Ghana taifa la asili yake badala ya England taifa ambalo ndipo alipo zaliwa ,
🗣 Sikuwahi kuwa na majadiliano na England, Ghana walikuja kwangu nikiwa na miaka 19 pekee na haikuwa rahisi kuwakataa , kwa familia yangu ilikuwa ni jambo kubwa sana maana yalikuwa maamuzi yalio tupa furaha na utulivu kati yetu , sikutaka kusubiri chochote maana ilikuwa ndoto yangu ya kuliwakilisha taifa la asili yangu ".
▪️Jambo kubwa sana hili 🙏🙏 kuna wengine wanasubiri mpaka wakataliwe ndo warudi Afrika.