Hakuna cha kuongea zaidi ya kuwapongeza hawa vijana. Kiukweli hata hapa walipofika wametushangaza wengi.
I hope huu ni mwanzo tu. Tutakuwa na mwendelezo mzuri na kushiriki mashindano kama haya mara kwa mara ili kuongeza exposure kwa vijana wetu.
Up Tanzania πΉπΏ
Hongereni Simba Queens kwa kutwaa ubingwa wa ligi kwa mara nyingine tena. π
Kwa mafanikio ya mataji matano ya ligi na kufika hatua ya nusu fainali ya CAF Womenβs Champions League, Simba Queens imeendelea kujidhihirisha kama moja ya timu zilizoweka alama kubwa zaidi katika soka la wanawake nchini Tanzania.
Mafanikio haya yanatupa sababu ya kujivunia, lakini bado tuna malengo makubwa zaidi.
Lengo letu ni kuona Simba Queens ikitwaa ubingwa wa CAF Womenβs Champions League na kuipeperusha bendera ya Tanzania barani Afrika.
Hongereni Simba Queens. Safari bado inaendelea. π¦ #Simba #Nguvumoja