Mungu akikupa nafasi ya pili kamwe usirudie makosa ya zamani. Ni kweli njia ya mafanikio haikosi vikwazo, lakini awamu hii hakikisha unaibuka na ushindi.
@Positivenga1 Binafsi nadhani kinachotofautisha hawa wawekezaji na sisi wengine ni suala la Nidhamu. Mfano nimejaribu kufuatilia founder wa Nala ana discipline ya hali ya juu. Chakushangaza zaidi kipindi anaanza watu walidhani kachanganyikiwa.
Nyakati ambazo unahisi kuchoka, upweke, kukata tamaa au kukosa morali ya kusonga mbele. Huu ndiyo muda sahihi wa kuongeza ukaribu na mwenyezi Mungu, ili kuamsha NGUVU YA NDANI.
Kwenye MAHUSIANO, watu hawavutiwi na wewe kwasababu ya Muonekano, Maumbile au Uzuri wa sura yako.
Kwani vyote huonekana vya kawaida, na huzoeleka ndani ya muda mfupi.
Ukweli ni kwamba, watu wataamua kubaki na wewe kutokana Utu na SIFA ZA KIPEKEE (Personality Traits) ulizonazo.
Kila mwaka Miti hupukutisha majani yake, ili kuruhusu USTAWI MPYA kwa Msimu unaokuja.
Hata kwenye Maisha kuna wakati utapitia magumu, na kupoteza kila chenye thamani. Hii haimanishi ndiyo mwisho wako.
Lahasha, bali ni hatua muhimu ya kuusogelea MWANZO MPYA kwenye Maisha yako.
Wakati ambao unahisi huzuni, majonzi, moyo umeinama na hujisikii kufanya chochote, ndiyo muda sahihi wa kuzungumza na Mungu wako.
Haijalishi ni kwa kiasi gani umeumizwa, Mungu atakufariji na kuiponya upya nafsi yako.
Nakusihi, USIHUZUNIKE Mungu yupo pamoja nawe.
Kwenye Maisha kuna MAJIRA tofauti utapitia.
. Kuna kupata na kukosa
. Kuna huzuni na furaha
. Kuna dhiki na faraja
. Kuna kupendwa na kukataliwa.
Haijalishi utapitia nyakati mbaya kiasi gani, USIKATE TAMAA kwani kila hatua ni muhimu katika kujenga kesho yako.
Kwenye UONGOZI, huitaji Mwili mkubwa, Mavazi au Lugha nzuri ili kudhihirisha uwezo wako.
Kwani ni KARAMA inayohitaji vitendo zaidi kuliko maneno.
Hivyo, Dhamira na Maono uliyonayo kwa watu unaowaongoza vitaamua uwezo ulionao.
Kwenye maisha jitahidi sana kuwatendea WEMA watu waliokuzunguka.
Hakikisha hauwafanyii kiburi, fitina au majivuno.
Kwasababu, MATATIZO yanatabia ya kukurudisha kwa watu uliowadharau na kuwafanyia mabaya.
Kwenye maisha ili ukue unahitaji PONGEZI lakini ili uwe bora zaidi kubali Kukosolewa.
Ni kweli UKOSOAJI unaumiza, lakini ni namna nzuri ya kukuwajibisha ili ufanye vizuri zaidi.
Hata MMEA ili ukue na kustawi unahitaji vyote viwili JUA na MVUA.
Kubali KUKOSOLEWA.