Biashara Asubuhi, Mahesabu Jioni.
Leo, Jumamosi ya tarehe 28 Juni 2025, saa mbili kamili asubuhi, nimekuwa mtia nia wa kwanza kufika katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, kuchukua rasmi fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Siha.
Hatua hii ni ya heshima, lakini pia ni ya dhamira. Nimefika mapema si kwa bahati, bali kama ishara ya namna ninavyochukulia jukumu hili kwa uzito, umakini, na heshima kwa wananchi wa Siha.
Ninakuja si kwa maneno tu, bali na rekodi ya kazi, uwezo wa kushirikisha watu, na maono ya kujenga Siha yenye maendeleo jumuishi, fursa kwa vijana, na huduma bora kwa wananchi wote.
Nimelelewa Siha. Nimepitia changamoto zake, nimeiona thamani yake, na naamini sasa ni wakati wa kizazi kipya kutoa mchango wake.
Leo ni mwanzo wa safari rasmi. Safari ya kusikiliza, kujifunza, na kutumikia kwa moyo wote.
Siha ni nyumbani. Na sasa, ni wakati wa kuijenga pamoja.