@faida_magiyula Uchambuzi wako ungelikuwa sahihi lau tu kama ungefanyika uchaguzi kwa maana ya uchaguzi lakinni si kwa uchafuzi huu wenyesura ya uchaguzi
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 24, 2025
Jana tuliishia part 142 so leo tunaendelea na-;
Part 143
Mhe. Lissu ameingia.
Inapigwa courtttttttttt.
Watu wote wanasimama kwa heshima na nidhamu kubwa sana.
Majaji wanaingia na kutoa heshima.
Tunakaa wote chini.
Karani anasimama anasoma jalada hapa na namba ya kesi ya Uhaini.
Upande wa Jamuhuri anasimama Renatus Mkude anatambulisha jopo na anasema wapo tayari.
Anasimama Mhe. Lissu anasema pia yupo tayari.
Renatus Mkude anaieleza Mahakama kuwa mpaka sasa wameleta mashahidi watatu na ameendelea kueleza kuwa Mashahidi wengine wanatoka mkoani hivyo siku ya leo hawatakuwa na shahidi wanaomba kuahirisha shauri na kutokana na ratiba leo ilikuwa siku ya mwisho ya usikilizwaji mpaka itakapopangwa tena.
Mhe. Lissu anasimama na kusema yafuatayo:
Nimesikiliza maombi yaliyosemwa na wakili wa Serikali na ninaomba niseme yafuatayo:
Kwa kifupi leo wameweka mpira kwapani, naona tafakari yao ya jana haijazaa matunda yoyote, kesi imewashinda hii na imedoda kweli kweli kama tulivyoambiwa na Mh. Lissu jana kwamba kesi ilishaisha labda kama anashikiliwa kwa ajili ya Uchaguzi.
Kama Mashahidi Mapolisi ushahidi wao ndio hao mabodaboda waliowakuta vijiweni na kuwatengeneza kuwa walihamasika na maneno ya Lissu watakuja kusema kipi kipya? ngoja tuwasubiri, nafikiri baada ya tarehe 29 kutakuwa na sura tofauti kabisa ya kesi hii ngoja tuone.
Mh. Lissu sasa anaanza na yeye kutoa maelezo yake kuhusu ombi la Mawakili wa Serikali la kuahirisha kesi hii.
Jambo la kwanza sababu iliyotolewa ya kuomba ahirisho sio sababu ya msingi ya kuahirisha kesi.
Kesi hii yote inategemea vielelezo vilivyokataliwa na Mahakama kuu hakuna shitaka ambalo lipo nje ya hizo flash disk na memory card na yaliyomo, Hakuna.
Mashahidi wale ambao wanadaiwa wapewe ulinzi ushahidi wao ni walichoona mtandaoni, mashahidi wa polisi waliobaki ushahidi wao unatokana na yale yaliyodaiwa kuwa mtandaoni.
Mashahidi pekee na ushahidi wao hauuhusiani na mambo ya mtandaoni ni afisa wa uhamiaji aje aseme kwamba mm ni mtanzania ili iweje?
Mwingine ni yule anaekuja kusema nilienda JKT ili iweje? Ili wathibitishe nini??
Wakati kesi ni mambo yaliyokuwa mtandaoni, Kesi hii ilishaisha Waheshimiwa Majaji, maneno haya ya Mawakili wa Serikali ni maneno ya bure kabisa na kutaka kutupotezea muda tu.
Ombi hili ni la kurefusha shauri hili ili niendelee kukaa gerezani ili Uchaguzi Mkuu upite.
Hawawezi kuthibitisha chochote kwasababu flash disk na memory card vimekataliwa, hawana kesi hapa.
Waheshimiwa Majaji kama mtaona ni sawa sawa kuahirisha shauri hili naombeni nipate dhamana ya mahakama kuu kwa mujibu wa kifungu 302(3) cha CPA.
Mahakama inaweza kumuachia mshtakiwa kwa dhamana, mm siendi popote. Nitakuwepo tu mtaani.
Kwasababu ya maamuzi ya jana na juzi hamna kesi hapa kama mtaaamua kuahirisha nipewe dhamana ili nisiendelee kuteseka kwa kitu ambacho hakiendi popote nitakuwa tayari kesi iahirishwe katika mazingira hayo.
Leo ni siku ya 202 nipo gerezani ni miezi sita na nusu nipo gerezani kwa haya ambayo tumeyaona na kuyasikia kuna kesi gani hapa kama sio umbea na uoga wa Serikali kwa watu wanaowapinga?
Kwahiyo waheshimiwa Majaji Ombi lao likataliwe mkikubali nipewe dhamana ni sawa hilo halitakuwa na shida ya kuahirisha.
Sijawahi kukimbia kesi yoyote na wamenifungulia kesi nyingi tu.
Mimi sio mtu wa kukimbia kesi tena kesi zenyewe za uongo uongo wa hawa Mapolisi, nikimbie kwenda wapi, nitamalizana nao hapa hapa Mahakamani walipoamua kunileta.
Nimeshafanya kazi hiyo vizuri na sitakuja kuacha kuifanya ilimradi watanileta tena.
Ni hayo tu waheshimiwa Majaji kwa sasa.
Waheshimiwa majaji wanaandika na kujadili kidogo kilichosemwa.
Anasimama Renatus Mkude tumesikia reply ya mshtakiwa, hapa anajibu pingamizi la Mhe. Lissu.
Msingi ni kwamba hatuna shahidi kifungu cha 302 CPA
Part 144 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 142
TumerudI Mahakamani.
Mawakili wa Serikali wanasema uwakailishi wao ni kama asubuhi.
Mhe. Lissu yuko tayari pia.
Anaendelea kumfanyia Cross-examination Samuel Elibariki Kaaya
Mhe. Lissu: Je umehesabu maswali uliyoulizwa na Wakili wa Serikali.
Samuel Kaaya : Sijui.
Mhe. Lissu: Maswali 165 umeulizwa unasemaje?
Samuel Kaaya : Sijui.
Mhe. Lissu: Majibu uliyotoa 112 HAYAPO kwenye maelezo yako ya Polisi unasemaje?
Samuel Kaaya : Sina uhakika.
Mhe. Lissu: Mambo ambayo hayapo kwenye maelezo yako polisi ni mengi sana unasemaje?
Samuel Kaaya : Sina la kusema.
Mhe. Lissu: Je ulitoa sababu kwanini hukuandika mambo hayo mengi kule Polisi?
Samuel Kaaya: Maelezo ni summary tu.
Mhe.Lissu: Umeelewa swali ? Nimekuuliza ulitoa sababu kwanini hukuandika mambo hayo Polisi?
Samuel Kaaya : Sikueleza.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji nani aliyeandika haya maelezo yako?
Samuel Kaaya : Nimeandika mimi.
Mhe. Lissu: Nani aliyekukanya kwamba ukisema uongo utashitakiwa?
Samuel Kaaya : Maeelezo ya shahidi hayana onyo.
Mhe. Lissu: Nani aliyekwambia maneno ya kwamba unapaswa kusema ukweli?
Samuel Kaaya : Niliandika Mwenyewe.
Mhe. Lissu: kuna mtu huwa anathibitisha maelezo yakiandikwa?
Samuel Kaaya : ndio.
Mhe.Lissu: Yako nani aliyathibitisha?
Samuel Kaaya : Mimi Mwenyewe.
Mhe. Lissu: Nani ananyewafundisheni Mapolisi namna ya kuandika haya maelezo?
Samuel Kaaya : Polisi wenzetu.
Mhe. Lissu: Unafahamu PGO?
Samuel Kaaya : Ndio nafahamu.
Mhe. Lissu: Mara ya mwisho ulisoma lini PGO?
Samuel Kaaya : Leo asubuhi.
Mhe. Lissu: Je hizi PGO zinakuruhusu wewe kujiandikia maelezo yako ya ushahidi?
Samuel Kaaya : Sijui.
Watu wanacheka.😀😀😀😀
Mhe. Lissu: Umeandika katika maelezo chini ya kifungu cha 10 cha CPA kwamba ndio uliandika hayo maelezo.
Samuel Kaaya : Ndio.
Mhe. Lissu: Hicho kifungu unajua kinasemaje? Je kinakuruhusu kujiandikia?
Samuel Kaaya : Mimi Sijui Sheria.
Mhe. Lissu: Wanasema mimi nilirusha live, nilikuwa mzungumzaji pia siku hiyo na pengine nilishika na camera kujichukua hizo video. Hivi hayo mambo yanawezekana kweli?
Samuel Kaaya : Hayawezekani.
Mhe. Lissu: Naishia hapo Jaji.
Wanaitwa Mawakili wa Serikali kwa ajili ya Rejoinder.
Anasimama Thawabu Issa na kumuuliza shahidi kuwa nina swali moja tu la ufafanuzi.
Kwanini maelezo yako ya Polisi yanatofautiana na ulichosema hapa Mahakamani?
Samuel Kaaya : Mimi sikuandika yote kwenye maelezo yangu kwasababu maelezo ni summary tu.
Mhe. Lissu : anasimama anasema hayo majibu ni mapya na sikusema aseme sababu kwahiyo majibu yake yasiingie.
Jaji anasema basi shahidi tunakuruhusu.
Anasimama Renatus Mkude na kusema tunaomba ahirisho hadi kesho saa tatu asubuhi lakini bado tunatafakari pia ruling za Mahakama.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji naomba wakati wanaendelea na hizo tafakari zao pia wasiache kutafakari kama kweli bado kuna UMUHIMU WA KUENDELEA NA KESI HII baada ya Mahakama kutoa hizo ruling.
Jaji Ndunguru : Tunaahirisha shauri hadi kesho saa 3 asubuhi tukutane kesho basi naomba muwe watulivu wakati mnatoka Mahakamani.
Kwa leo tunaishia hapa so tukutane tena kesho saa tatu asubuhi kama kawaida.
Mungu awabariki sana.🙏🏻
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 141
Mhe. Lissu: Ulisema maneno ya kuwa msimamo wetu unaashiria uasi yaanzia dakika 8 kwenye video. Je hayo nayo yapo kwenye maelezo yako Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema ukitumia Amped Authenticate inaweza kukusaidia ukajua camera iliyotumika kupiga hizo video?
Samuel Kaaya : Sahihi nilisema.
Mhe. Lissu: Je ulieleza hiyo camera uliyoitaja ilikuwa ni mali ya nani?
Samuel Kaaya : Sijaeleza ilikuwa ni mali ya nani?
Mhe. Lissu: Je umeeleza nani alikuwa anaitumia siku hiyo pale Mikocheni Makao makuu ya Chadema?
Samuel Kaaya : Sijui pia.
Mhe. Lissu: kwahiyo hujui aliyekuwa anapiga picha na aliyekuwa anaimiliki hiyo camera.
Samuel Kaaya : Sijui kiukweli.
Renatus Mkude: Anasimama Mh. Imefika saa saba na dakika tunaomba mapumnziko ya lisaa limoja.
Mhe. Lissu: Naomba niulize la mwisho tu halafu tukapumnzike.
Sasa shahidi swali la mwisho mtu ambae hana password wala username anaweza ku upload video kwenye ukurasa wa Jambo TV?
Samuel Kaaya : Akihuck anaweza kuingia.
Mhe. Lissu: Sasa kwenye mazingira ambayo hakuna Hacking tuhuma zinasema mimi ndio nimeupload hizo video kwenye mtandao wa Jambo TV. Tusaidie kwa ufahamu wako unaelewaje?
Samuel Kaaya : Hakuwa mtu anaweza kuingia kwenye mtandao wa mtu kama hana hizo credentials za kuingilia au ku hack ndio unaweza kuingia.
Mhe. Lissu: kwahiyo ni either una password, password creaker au unafanya Hacking?
Samuel Kaaya : Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu ; Je mimi nina password?
Samuel Kaaya : Sijasema unazo na sijui pia.
Mhe. Lissu: Password creaker je?
Samuel Kaaya : Sijui na sijasema unayo..
Mhe. Lissu: Je nilifanya Hacking?
Samuel Kaaya : Hukufanya.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji Tukale sasa.
Jaji anasema tutakutana baada ya lisaa limoja na nusu.
Turudi hapa saa nane na nusu.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 140
Anaendelea Mhe. Lissu na maswali ya Dodoso
Ulisema Wakati wa kuandaa taarifa yako ya Uchunguzi ni lazima ufanye reference kwenye Police Notebook na huku ukiangalia yale uliyokuwa umeandika kwenye Polisi Notebook, ni sahihi ulisema hivi?
Samuel Kaaya : Nilisema.
Mhe. Lissu: Yako wapi sasa kwenye maelezo?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuhusu covering letter na ukaiambatabisha na taarifa ya Uchunguzi, Je hayo nayo yapo kwenye maelezo yako?
Samuel Kaaya : Ni kweli nilisema lakini hayapo kwenye maelezo yangu yale ya Polisi.
Mhe. Lissu: Hiyo covering letter umeleta?
Samuel Kaaya : sijaleta kwasababu ni internal communication.
Mhe. Lissu: Kwahiyo haiwahusu Majaji?
Samuel Kaaya : Ni kweli haiwahusu.
Mhe. Lissu: Sasa kama haiwahusu uliisema hapa Mahakamani ili iweje?
Samuel Kaaya : Mimi Sijui.
Shahidi hapa amepiga ile tunaita CHAKUFIA NINI?😀😀😀
Mhe. Lissu: Je barua uliyoandikiwa ya kukuomba ufanye uchunguzi umeiwasilisha kwenye kesi hii?
Samuel Kaaya : Hii haina uhusiano na kesi hii.
Mhe. Lissu: Je barua ya pili umewasilisha?
Samuel Kaaya : Sijui wanayo Mawakili wa Serikali.
Mhe. Lissu: Unasema ulifungua mafile mawili ya Uchunguzi baada ya kupata hizo barua kutoka requesting authority. Je hayo mafile umewasilisha mahakamani kama kielelezo?
Samuel Kaaya : Sijawasilisha.
Mhe. Lissu: Mahakama sasa itajuaje kama wewe ndio uliombwa kufanya uchunguzi kama hujaleta barua uliyoombwa kufanya uchunguzi na pia hujaleta ripoti wala video itakuaminije?
Samuel Kaaya : Itaniamini kwa maneno yangu hapa Mahakamani na hayo maelezo ya Polisi.
Mhe. Lissu: Umewahi kusikia msemo wa Kiswahili kuwa maneno matupu hayavunji mfupa?
Samuel Kaaya : Sijawahi kuusikia.
Mhe. Lissu ; Je mkono mtupu haulambwi?
Samuel Kaaya : Sijawahi sikia.
Mhe. Lissu: Je Mali bila daftari hupotea bila habari?
Samuel Kaaya : Huo nao sijawahi kuusikia.
Mhe. Lissu: Sasa maneno yako na wewe hapa Mahakamani yamepotea bila habari.
Watu wanacheka 😂
Mhe. Lissu: Ulisema habari ya kitabu cha Laboratory Boom Register, Je nayo umeileta hapa Mahakamani?
Samuel Kaaya: Sijaleta pia.
Mhe. Lissu: Hivi ili uwe assigned kufanya uchaguzi utararatibu ukoje?
Samuel Kaaya : Zipo minutes pale kwenye file la Ofisi ndio anaandika huko.
Mhe.Lissu: Hiyo ndio tunaita kwa lugha za ofisi ni Dokezo 70 kwamba inaandikwa kazi fulani aifanye fulani?
Samuel Kaaya : Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Sasa umeleta hiyo dokezo 70 hapa Mahakamani?
Samuel Kaaya : Sijaleta.
Mhe. Lissu: Nisaidie ulisema kulikuwa na majalada mawili la kwanza ni taarifa za uongo na la pili ni uhaini. Hayo maneno yako wapi kwenye maelezo yako?
Samuel Kaaya : Hayapo sikuandika.
Mhe. Lissu: Katika uchunguzi wako ulisema hiyo video ilikuwa uploaded kwenye channel ya youtube ya JAMBO Tv ni sahihi?
Samuel Kaaya : sio sahih, mimi nilisema video imepatikana kwenye youtube kupitia account ya Jambo Tv.
Mhe. Lissu: Kwahiyo hiyo video ilipatikana kwenye account ya Jambo TV?
Samuel Kaaya : sahihi.
Mhe. Lissu: Sasa waeleze kama uliweza kubaini mtu aliyeiweka video clip kwenye hiyo account ya Jambo Tv?
Samuel Kaaya : Mimi experts sijibu facts najibu kama mtaalamu.
Mhe. Lissu: Sasa mimi ndio nashitakiwa kuwa nimeiweka huko Jambo TV na wewe ni mtaalamu umekuja leo nataka utusaidie, nani aliweka?
Samuel Kaaya : Account ya Jambo Tv ndio iliweka hiyo account.
Jaji Kalyamaahe: Kwahiyo ulibaini mtu au hukubaini mtu aliyeweka hiko youtube?
Samuel Kaaya : Mimi sikubaini mtu.
Mhe. Lissu: Mimi nashitakiwa kwa kuweka hiyo video huko Jambo Tv basi na mimi nitumie fursa kusema Mwenyezi MUNGU akurehemu na kukubariki sana maana kama mtaalamu umesema mimi sijaweka huko hiyo video nani mwingine atakuja kusema mimi niliweka hiyo video. Ahsante sana.
Part 141 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 139
Mhe. Lissu: Kati ya Mwaka 2021 na 2022 ulihudhuria mafunzo ya Assistant Inspector of Police kule Moshi, sasa kwenye maelezo yako Polisi mambo hayo yapo?
Samuel Kaaya : Sikuyasema.
Mhe. Lissu: Ulisema umesomea medani za kivita na masomo mengine mengi hayo nayo umesema kwenye maelezo yako Polisi?
Samuel Kaaya : Sikusema.
Kwa kifupi huyu shahidi amesema mambo mengi sana hapa Mahakamani ambayo siku anaandika maelezo yake Polisi kuhusu kesi hii hakuyaandika ila hapa Mahakamani ameyasema.
Ndio yale maeneo 75 ambayo Mhe. Lissu ameyasema hapo awali na anaendelea kumuuliza.
Kila kitu anachomuuliza shahidi kwamba ulisema hivi hapa Mahakamani je kwenye maelezo yako yapo? JIBU LA SHAHIDI NI HAPANA, HAYAPO NA SIKUANDIKA.
Yataulizwa maswali mengine ya utofauti wa statement mfano alisema hapa Mahakamani hivi na kwenye maelezo alisema tofauti tutafikia pia hatua hiyo.
Lengo la zoezi hili ni kuonesha shahidi ni muongo na hapaswi kuaminika.
Mhe. Lissu: Je ulisema sana hapa Mahakamani kuhusu mafunzo uliyopata South Africa, Je kwenye maelezo yako yapo?
Samuel Kaaya: Sikuandika kwenye maelezo yangu.
Mhe. Lissu : Ulisoma miezi sita chuoni hapo?
Samuel Kaaya : Sikuandika na hilo pia.
Mhe. Lissu: Anauliza kuhusu chuo cha IFM na Masomo aliyosoma ya kuhusu Uhasibu na Data Management anayosema alisomea na kuzawadiwa shahada ya Sayansi ya Tehama kwenye vyuo mbalimbali je yako wapi kwenye maelezo yake?
Samuel Kaaya : Sikusema.
Mhe. Lissu: Mwaka 2024 ulipata mafunzo katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Sayansi ya Jinai. Kule India, Je yako wapi hayo kwenye maelezo yako?
Samuel Kaaya : sikuandika kwenye maelezo yangu, hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema mambo mengi ikiwemo utaratibu wa kuchunguza vielelezo ikiwemo ile kanuni yenu ya first inn first out kama umeuelezea kwenye maelezo yako ya pale Polisi?
Samuel Kaaya : Sikuelezea kabisa.
Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuhusu kuwepo na Police Notebook muda wote ili kila unaloliona unarekodi kwenye Polisi Notebook, je hayo yapo kwenye maelezo yako?
Samuel Kaaya : Hayapo
Mhe. Lissu: Hivi nyie Mapolisi nani huwa anawafundisha kuandika maelezo yenu?
Samuel Kaaya : Tunafundishana wenyewe.
Mhe. Lissu: Neno Confimatory test ulifanya, sasa nionyeshe hapo kwenye maelezo yako hiyo confirmatory test ulipoandika.
Samuel Kaaya : Kiukweli Sijaandika hilo neno, halipo.
Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuwa unafanya Chron analysis ili kugundua kama kuna Deep Fake yaani teknolojia ya AI imetumika katika video husika je hayo yapo kwenye maelezo yako uliyoandika Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo Sikuandika.
Mhe. Lissu: ulisema habari za kuangalia video kama iko compressed or decompressed nao upo kwenye maelezo yako?
Samuel Kaaya : Haupo.
Mhe. Lissu: Ulisema kuhusu censor pattern analysis na non Uniformity je hayo nayo yapo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema habari za kufanya noise analysis kwenye hiyo video sasa tueleze hayo mambo mengi na utaratibu wa kufanya noise analysis na unaweza kuona vichengachenga kwenye video kama yapo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo
Mhe. Lissu: Nitakuwa sahihi nikisema huu ushahidi wa maeneo niliyokupitisha ulikuwa ni wa muhimu kwenye kesi hii?
Samuel Kaaya : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Na ni kweli ni muhimu kwasababu unaonesha maabara yenu inavyofanya kazi kitaalamu?
Samuel Kaaya : Ni kweli
Mhe. Lissu: kuhusu notebook ni muhimu askari awe nayo muda wote wa uchunguzi hilo nalo ni muhimu?
Samuel Kaaya : Ni muhimu.
Part 140 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 138
Mhe. Tundu Antipas Lissu akiwa anaendelea kumsomea Shahidi maelezo yake.
Anasema naomba tuelezane yafuatayo.
Majaji watatu ambao ni Dunstan Ndunguru-Mwenyekiti wa jopo.
James Karayemaha – Jaji mjumbe wa jopo.
Ferdinand Kiwonde – Jaji mwingine wa jopo.
Wameingia kwenye rekodi ya kusikiliza shauri hili la Uhaini linalomkabili Mhe.Tundu Lissu na kwakweli kwa hatua ya sasa ya wao kukataa kupokea hivi vielelezo viwili kwa maana video pamoja na report ya mtaalamu nafikiri hata kama wamefanya kwa mujibu wa sheria na kweli.
Mungu atawabariki kwa hilo kwasababu kwa Mahakama zetu na namna tulivyowazoea hawa Majaji wangeweza kuamua vinginevyo na tusingekuwa na la kusema.
Nafikiri katika hili na sisemi wamefanya kwa nguvu zao ila ninachokisema lolote walilolifanya angalau rekodi zitawatambua kuwa kuna maamuzi ya msingi waliyafanya katikati ya kesi hii.
Kazi kwao huko mbele kama hawatajidharirisha.
Kwa hatua ya sasa nafikiri WATANZANIA hawawadai chochote hawa Majaji.
Wamejitahidi kutenda haki na Mimi binafsi nawaombea kwa Mungu kila la kheri kwasababu tunafahamu wanaafanya kazi kwenye utawala ambao professionalism hakuna kabisa pongezi sana kwao kwa hatua ya sasa.
Mara baada ya pongezi hizo, Mheshimiwa Lissu anamueleza shahidi maeneo ambayo anataka kum contradict shahidi kutokana na kilichopo kwenye maelezo yake Polisi na alichosoma hapa Mahakamani.
Ameshafika eneo la 30 kwa sasa ambayo yanatofautiana na maelezo yake hapa Mahakamani. Ikiwa ni pamoja na Elimu yake ya Upolisi, Masomo aliyosoma nyakati tofauti tofauti, vyuo na course mbalimbali za kipolisi alizosoma South Africa, India na maeneo nengine.
Mhe. Lissu alikuwa anasoma maeneo ambayo amefikisha maeneo 75 anayotaka kwenda kumcontradict shahidi.
Mhe. Lissu amemuuliza Shahidi je ungependa maelezo yako sasa yapokelewe kama ushahidi Mahakamani?
Shahidi: Waheshimiwa Majaji naomba yapokelewe kama ushahidi.
Jaji Ndunguru anasema maelezo hayo yamepokelewa kama kielelezo cha Mshitakiwa na nitayapa alama Exhibit D2 ya upande wa Mshitakiwa.
Kwa kifupi kwa msio elewa hadi sasa Jamhuri hawana kielelezo chochote kilichopokelewa kuunga mkono kesi yao.
Ila upande wa Mshitakiwa Tundu Lissu hadi sasa amefanikiwa kuingiza vielelezo viwili yani Exhibit D1 na Exhibit D2 ambavyo vyote lengo lake ni kuonesha mashahidi wa Jamhuri ni waongo na wanatunga mambo.
Waliyosema hapa Mahakamani ni tofauti na walichokiandika kule Polisi nako ni tofauti kabisa.
Kwahiyo kwenye vielelezo hadi sasa ni mbili bila. 😂
Mhe. Lissu anaanza sasa kuendelea na maswali yake.
Kwenye ushahidi wako ulisema wewe ni mtaalamu wa picha na uliteuliwa kwa kazi hiyo naomba angalia maelezo yako uliyotoa polisi kama ulisema kuwa wewe ni mtaalamu wa picha kwa mujibu wa GN NO. 725/2020.
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: ulisema hapa Mahakamani Kati ya 2003 na 2004 ulihudhuria mafunzo ya Polisi Moshi CCP sasa angalia kwenye maelezo yako kama mambo hayo yapo?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: Hapa Mahakamani ulisema ulisomea Criminal Law, Singe, Judo na Karate na masomo mengine sasa waeleze majaji kama yapo kwenye maelezo yako Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: je kuhusu ulipandishwa cheo na kupata cheti cha umahiri nayo yapo kwenye maelezo yako Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuwa ulifanya mafunzo ya upigaji picha je yapo hayo kwenye maelezo yako Polisi?
Samuel Kaaya : Hayapo.
Part 139 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 23, 2025
Jana tuliishia part 136 so leo tunaendelea na-;
Part 137.
Mh. Lissu ameingia ila leo amekuja na ujumbe anasema kuwa yatakwisha tu.
Majaji wameingia wapo watatu kama kawaida yao.
Karani anasoma namba ya shauri
Wakili wa Serikali Renatus Mkude anatambulisha jopo la Mawakili wa Serikali na anasema yuko tayari kwa ruling kwa upande wao wa Jamhuri.
Mshitakiwa nae anasema yuko tayari.
Anaanza kusoma Jaji Kiwonde kwa niaba ya Majaji watatu.
Mshitakiwa alipinga shahidi Na. 3 kutoa report kwani ilipaswa kuwa ni certificate lakini pia mshitakiwa alisisitiza kuwa shahidi huyu ni mtaalamu wa picha na sio video.
Lakini pia Mr. Job Mrema yeye alijibu pingamizi hilo na kusema pingamizi halina mashiko.
Alisema Mahakama hii haibanwi na maamuzi yake aliyoyatoa siku ya jana kuhusu flash na memory card.
Na mshitakiwa alienda mbali kuingia kwenye content za report wakati Mahakama ya Rufani ilishazuia jambo hilo.
Mr. Mrema anasema kwa mujibu wa kifungu cha 216 cha CPA shahidi anaruhusiwa kutoa hiyo report.
Kwasababu ina uhusiano mkubwa na kesi na hata yeye ndio aliandaa basi ni yeye ndio anaweza kuitoa.
Na katika rejoinder mshitakiwa anasema taarifa hii au report vina uhusiano mkubwa kama hizo device zimekataliwa hivyo hata report haina miguu ya kusimama.
Mahakama inapaswa kuamua kama shahidi Na. 3 yuko competent kutoa hicho kielelezo.
Sisi tunaona shahidi Na. 3 ni mtaalamu na kwa mujibu wa kifungu 216 kimeeleza majukumu ya mtaalamu na GN Na. 799/2020 inasema kinagaubaga wajibu na kazi ya shahidi.
Hakuna ubishi aliteuliwa na DPP na Attorney General na hicho kilichopo hapa Mahakamani ndio kipo kwenye kifungu hicho.
Kwetu sisi tunaona kazi yake ni kuzichunguza zile picha na baada ya kufanya huo uchunguzi yeye analo jukumu la kuandaa certificate.
Hizo ndizo kazi aliteuliwa kufanya.
Tunakubaliana na Mshitakiwa kuwa shahidi alipaswa kuandaa Certificate badala ya kuandaa Report.
Angekuwa ameteuliwa kama Forensic expert basi tungekubaliana na nyaraka yake.
Kwenye kesi hii shahidi Na. 3 aliteuliwa kushughulikia picha mnato ambazo zinapelekwa kwake na hilo tulisema jana pia na mwishoni anaandaa certificate.
Kwa maana hiyo hatukubaliani na Mr. Mrema kuwa kuna mtego na sisi hatuko tayari kuingia kwenye mtego alitupatia Mrema na kumuamini.
Hii taarifa inalenga kwenda kuelezea nini kama tutaipokea?
Hicho kinachoelezewa kwenye taarifa kama hakipo tukiipokea tunaopokea ili kije kutusaidia nini kama Mahakama.
Huyu Shahidi hana uwezo wa kutoa hiyo taarifa bali alipaswa kutoa CERTIFICATE.
Tunaona pingamizi lina Mashiko. Na tunakubaliana na Mshitakiwa na tumeamua hivyo.
Leo tena wamepigwa na kitu kizito hawa ndugu zetu wa Jamhuri. Wamechanganyikiwa tena kwa mara nyingine. 😂😂
Jaji amesema haya sasa muendeleee.
Anasimama Thawabu Issa Wakili wa Serikali anasema Mhe Jaji.
Jaji anamwambia subiri kwanza Wakili,
Shahidi nakuonya upo chini ya kiapo.
Ukiwa unaendelea kutoa ushahidi wako.
Shahidi sawa Mhe. Jaji.
Thawabu Issa anasema Mhe. Jaji hatuna kingine cha zaidi kwa Shahidi huyu.
Tunaomba kuishia hapa
Watu wanacheka.😂😂😂
Anaitwa Lissu kwa ajili ya Maswali ya Dodoso.
Mhe. Lissu: Shahidi uliandika maelezo yako Polisi tarehe 08/04/2025 kwenye ofisi za Polisi Forensic Bureau?
Samweli Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu ; Je ukiyaona hayo maelezo yako utayatambua.
Samweli Kaaya: Ndio nitayatambua. Ni maelezo yangu.
Anasomewa hapa Maelezo yake na anapatiwa.
Mhe. Lissu ananendelea kumsomea Maelezo yake Polisi huyu shahidi ambae ni Samweli Elibariki Kaaya.
Part 138 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 136
Anatoa kesi nyingine ya Maghimbi Mzini Criminal appeal No. 304/2023 Mahakama ya Rufani
Ukurasa wa 21 unasema admissibility of documentary evidence huo ni mtego na Mahakama isiingie hapo.
Kwa kumalizia Mahakama hii naomba isiyazingatie mapingamizi ya Mshitakiwa.
Jaji anasema Mshitakiwa karibu kwa ajili ya Rejoinder.
Mhe. Lissu anaanza.
Waheshimiwa Majaji msishawishiwe na uamuzi wa awali kuhusu admissibility ya flash disk na memory card kwasababu hivi vitu viwili ni tofauti kabisa.
Hivyo msishawishike kusimama na msimamo wenu wa flash disk na memory card.
Wakili wa serikali Mkuu hajaelezea kwanini hizo nyaraka ni tofauti.
Sasa Majaji ni kweli hivi vitu ni tofauti kimoja ni karatasi na kingine ni memory card huo utofauti ni wa kweli hata kama hajaelezea.
Lakini swali la msingi hapa ni hii ripoti ambayo iko tofauti na flash na memory card inahusu nini? Content yake ni nini? Inahusu flash disk na memory card pamoja na kwamba they are different but they are related.
Bila flashdick na memory hakuna report na hayo ndio mahusiano yake kimoja kikianguka kingine hakiwezi kusimama.
Hii report Waheshimiwa Majaji kwasababu ni report ya Vitu vilivyokataliwa na Mahakama haiwezi kusimama yenyewe, kusimama kwake kunategemeana na kile ilichokichunguza.
Waheshimiwa Majaji kama taarifa ikipokelewa haitakuja kuprove chochote Mahakamani.
Wakili wa Serikali Mkuu Mrema amewaalika msiangalie content za hiyo report na anasema mimi nimeenda kwenye content za report.
Wakili wa Serikali Job Mrema anasema the fact kwamba hiki kielelezo hakijaitwa CERTIFICATE kuitwa kwake taarifa hakubadilishi Content.
Hii sio kesi ya kukosewa jina. This is not the case of misnaming this is a case of something being tendered which have never been tendered.
Hii taarifa sio tu taarifa jina ni taarifa kwa content kungekuwa na umaana wa hii taarifa yao wangeambatabisha na kurasa moja ya Certificate kwa mujibu wa sheria.
Sasa wametuletea kurasa 11 za maandishi hiyo tunaita nini kama sio taarifa?
You should not be persuaded kuwa hili jina halina shida, hilo jina linaelezea kilichopo ndani.
Maghimbi Mzini dhidi ya Jamhuri ni kesi nyingine imeletwa na wenzetu pia hii kesi haiwasaidii hata kidogo naomba nisome paragraph mbili kwenye ukurasa wa 21.
Amesoma hiyo kesi.
Anasema hoja hapa hatujajadili uzito wa ushahidi wa hiyo taarifa, My only contention has been hii taarifa is not admissible.
Haijakidhi matakwa ya sheria ya kupokelewa kama kielelezo, sijasema ripoti hii ni ya uongo na ina mambo yasiyo ya ukweli.
Mimi sijafika huko nimeishia kwenye suala la kwamba hayakidhi vigezo.
Kwahiyo with all due respect hii kesi ya Maghimbi Mzini haiwasaidiii kwasababu inasema tusichanganye uzito wa ushahidi na kupokelewa kwa kielelezo.
Ni hayo tu Mhe. Jaji, Mhe. Lissu amemaliza kufanya Rejoinder
Majaji wanaandika kidogo.
Mawakili wa Serikali kwa mara ya kwanza leo wapo na kahali fulani ambako ni kama hawaitaki kesi kabisa.😂
Ukiwaangalia unaona moja haikai na mbili haikai, wapo wapo kama wamerogwa.
Majaji wanamaliza kuteta hapa.
Jaji Ndunguru anawasha kipaza sauti.
Anasema Mahakaman itatoa uamuzi kesho saa tatu asubuhi.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 135
Mahakama imerejea.
Amesimama Renatus Mkude kusema Uwakilishi uko kama asubuhi na tunaomba Job Mrema atoe majibu.
Amesimama Job Mrema sasa kujibu.
Upande wa Jamhuri tumesikia pingamizi lililowasilishwa na mshitakiwa kuhusiana na upokelewaji wa taarifa ya mtaalamu ambae ni PW 3.
Ni msimamo na hoja yetu kwamba tunapinga pingamizi la Mshitakiwa kuhusiana na kielelezo tunataka kukitoa.
Job Mrema huwa anaongea kama anarap anaanza kwa sauti ndogo baadae anaongeza sauti.
Sisi tutajibu kwa kifupi sana ingawa yeye amesema kwa urefu sana.
Anaendelea Job Mrema hapa.
Waheshimiwa Majaji muda mfupi Mahakama ilitoa uamuzi wa kutopokea kielelezo cha flash na memory card.
Ni dhahiri kuwa uamuzi kuhusiana na flash disk na memory card ni tofauti na kielelezo ambacho Mahakama hii imeombwa na Shahidi kukipokea.
Pia Mshitakiwa alikuwa anajaribu kusema wino haujakauka.
Alikuwa anajaribu kuhusianisha hivi vielelezo viwili.
Suala la wino umekauka au haujakauka sio subject matter kwenye hii kesi katika mazingira kama haya Mahakama hii ione hivi vitu ni tofauti.
Ni hoja yetu kwamba katika mazingira ya sasa hoja muhimu ni suala la upokelewaji wa kielelezo.
Mshitakiwa ameanza kusoma maudhui ya kielelezo.
Huko kwenye maudhui hatujafika bado hapa tulipaswa kujadili upokelewaji wa kielelezo tu.
Waheshimiwa Majaji kwenye kueleza hilo Mahakama hii ya Tanzania imedevelop principle zinaisadia Mahakama kufikia kwenye maamuzi yaliyo sahihi.
Katika mazingira tuliyonayo tunaialika Mahakama hii kutizama principle ya admissibility of an exhibit before the Court of law.
The exhibit must be cleared before admission hicho ndio Mahakama inapaswa kuanza nacho.
Utaratibu haujafuatwa, kielelezo kingesomwa na shahidi baada ya hiyo hatua ya kwanza sasa Mshitakiwa ameanza kukisoma yeye mwenyewe.
Labda nichomekee, hivi mnamuelewa kweli hapa Job Mrema anapiga akapela, hasemi kifungu cha Sheria wala hajatoa zile kesi zake nyingi anazotoa, ngoja tumsubiri.
Sasa amekumbuka kutaja kesi anasemaa Kesi ya Robison Mwanjisi Criminal Appeal No. 154/1994. Ukurasa wa 18 unasema katika kufafanua principle ambayo Jamhuri imeisema kwamba before you read out the documentary evidence, it must be cleared first and after admission the witness will read the same.
Pia Mshitakiwa alirejea kifungu cha 216 cha CPA na mtaalamu anayezungumziwa kwenye kifungu hicho ni huyu mtaalamu ambae yuko Mahakamani.
Pia amerejea GN. No. 799/2020 kuwa PW 3 ametangazwa kwenye gazeti la Serikali na sisi tunasema ni kweli ametangazwa na hili ndio jukumu alilokuwa nalo.
Swala la substance ya taarifa hii ni mtego ambao sisi tunautegua upande wa Jamhuri. Tunaialika Mahakama isifike huko.
Anaendelea Job Mrema hapa anasema Kesi ya Sharif Mohamed Mahakama itabaini kuwa wakati wa upokelewaji wa kielelezo mahakama inazingatia vitu vitatu ambavyo ni competence, materiality and relevance.
Katika kipindi hiki Mahakama inazingatia hivyo vitu vitatu.
Mtaona pia vinakuja kuwa qualified kwenye shauri la Robison.
Je vielelezo vinavyopaswa kutolewa na shahidi ni relevant? Jibu ni NDIO ni relevant kabisa.
Pia issue ya materiality na sisi tunasema ile nyaraka ina ushahidi ambao ni material kabisa.
Pia vifungu alivyocite vyote hatuoni kama ni relevant.
Hoja ya msingi hapa ni kwamba baada ya shahidi kufanya kazi vielelezo alivyoletewa nini kilipatikana? Ndio hiki kielelezo.
Halafu kutokuandikwa kuwa hii ni certificate je inafuta content iliyopo ndani ya hiyo taarifa?
Haiwezi kabisa kufuta content ya hiyo nyaraka.
Kwa taarifa yenu tu leo kivuruge wao KATUGA hayupo kabisa Mahakamani. pengine aliona kuna aibu itatokea akaamua kula nyoya so leo ameachiwa msala Job Mrema.
Part 136 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 133
Anaendelea kusoma uamuzi Jaji Nduguru
Kilichotokea hapa Mahakamani shahidi ametender flash disk yenye hizo video na memory card.
Ingawa upande wa Mashitaka uliishawishi Mahakama kuwa hizo flash disk zimebeba picha na video na wakatumia shauri la India.
Mahakama imepitia upande wa Mashitaka na hoja zao walizoleta.
Mahakama imerejea kwenye kifungu cha 216 cha CPA kikirifaa mambo ya picha na hakisemi kuhusu video.
Hivyo vitu viwili vina maana tofauti kuhusu photograph na video na Jamhuri wameshindwa kutofautisha.
Shahidi Na. 3 alichokuwa anataka kukitoa hivyo vitu sio photographic prints wala enlargement.
Kwahiyo huyu shahidi hana uwezo wa kutoa hiyo video na Mahakama imekataa kupokea hizo video.
Wataalamu wa electronic ndio walipaswa kuja kutoa hizo video na tumeona ipo GN inayohusiana na video na mambo ya kielektroniki kwa ujumla.
Baada ya kusema hayo Mahakama inakubaliana na pingamizi la mshitakiwa.
Jaji anasema tuendelee sasa.
Kabla hatujaendelea kwa kifupi ni kwamba VIDEO AMBAYO SASA NDIO USHAHIDI WENYEWE WA KESI IMEKATALIWA. KWAHIYO HAYO WANAYOSEMA YALISEMWA NA LISSU AMBAYO NDIO UHAINI WENYEWE. MAHAKAMA IMEUKATAA. KWA KIFUPI KESI IMEISHIA LEO. HAPA TUNAPOTEZA MUDA KUSUBIRI HUKUMU.
Anasimama Thawabu Issa kuanza kumuongoza Shahidi.
Sasa shahidi ulizungumzia kuhusu taarifa ya uchunguzi.
Ukiiona utaijuaje.
Samwel Elibariki Kaaya: Nitaitambua kwa majina yangu, logo ya Polisi, signature, Muhuri na tarehe.
Thawabu Issa: Naomba Waheshimiwa Majaji naomba nimuonyeshe Nyaraka shahidi.
Jaji: Muonyeshe.
Anapewa shahidi nyaraka kadhaa.
Shahidi anasema hii ndio ripoti ya kitaalamu niliyoiandaa ina majina yangu na vyote nilivyosema awali na niliandaa mwenyewe.
Wakili wa Serikali: Unaiomba nini Mahakama?
Shahidi: Ipokee kama sehemu ya kielelezo.
Jaji: Mpatieni Mshitakiwa.
Mhe. Lissu anaiangalia anasema napinga hiyo taarifa kupokelewa kwa hoja zifuatazo.
Hii inaitwa Mbwa kala Mbwa.😀
Mhe. Lissu anaanza tena.
Waheshimiwa Majaji kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Jinai shahidi anayetakiwa kuwasilisha taarifa za uchunguzi wa kitaalamu, anapaswa kuwa ni shahidi aliyetamkwa kwenye kifungu cha 216, 217, 218 na 220 vya Sheria ya Mwenendo wa Jinai.
Sasa Waheshimiwa Majaji shahidi huyu ni shahidi wa picha za mnato kwa maelezo yake yeye mwenyewe mtayaona kwenye kielelezo anachotaka kukiwasilisha.
Mimi Samweli Kaaya Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la Polisi ambae ni mtaalamu wa picha chini ya kifungu cha 202(1) cha CPA.
Sasa anaendelea Mh. Lissu.
Sasa Waheshimiwa Majaji hicho kifungu cha 202(1) cha CPA ndio kifungu cha 216 cha sheria ya sasa kinazungumzia hati za wataalamu wa picha mnato.
Wao wanakitumia kuleta kielelezo ambacho ni video.
Waheshimiwa Majaji WINO HAUJAKAUKA. toka muamue kuwa huyu shahidi hapaswi kuleta ushahidi wa video hapa Mahakamani maana yeye sio mtaalamu wa video.
Shahidi yeye mwenyewe amejisema kuwa yeye sio shahidi competent, amejisema Mwenyewe.
Tunaanzaje kumkubalia?
Na hawa Mawakili wa Serikali sijui wana akili au wamerogwa maana muda mfupi uliopita Mahakama imewaambia kuwa huyu mtu sio mtaalamu wa video ni mtaalamu wa picha, wao wanataka kutuletea hapa mtaalamu wa picha aliyechunguza video ni kituko.
Kwenye kielelezo chake mwenyewe shahidi anasema pia ameteuliwa na tangazo la serikali 799 lilitolewa na AG Adeladus Kilangi halikutolewa na DPP.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali hakuwa na Mamlaka na hana mamlaka ya kuteua mtaalamu yeyote aliyesemwa kifungu cha 216 hadi 220 cha CPA.
Mawakili wa Serikali wapo na ubaridi mkubwa wamekuwa wadogo sana kama Pilton.
Sect. 216 ya CPA inazungumzia Certificate ambayo ndo ripoti yenyewe ya mtaalamu na kinasema pia uteuzi wa huyo mtaalamu anapaswa kuteuliwa na DPP na sio AG.
Part 134 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 22, 2025
Last time tuliishia part 131 so leo tunaendelea na-;
Part 132
Ameingia Mhe. Lissu akiwa amepiga Tshirt yake Nyeusi ya Chama.
Yuko na vibe kama ilivyo siku zote.
Dakika Chache kabla Mahakama haijaanza Makamu Mwenyekiti John Heche amechukuliwa na Mapolisi na kuondoka nae.
Majaji wameingia hapa Mahakamani.
Watu wote wamesimama.
Kabla Mahakama haijaanza upande wa juu wa Mahakama ameingia mtu amesimama amesema yeye ni Nabii ametumwa na Mungu.
Anasema anaomba Majaji wamsikilize, jana alikuja hapa Mahakamani akaishia hapo Maaskari wamemdaka na kuondoka nae.
Kabla ya kuondoka nae amepiga kelele nyingi akisema YESU YESU YESU, anasema yeye ni Nabii yuko toka jana ametumwa na MUNGU kuwa Tundu Lissu aachiwe.
Leo siku imeanza kwa mambo mengi yakushangaza kama hivyo.
Jaji anaanza kusoma sasa uamuzi mdogo wa yale Mapingamizi ya Mhe. Tundu Lissu.
Wakati shahidi akitaka kutoa vielelezo mshitakiwa aliweka hoja nne kupinga. Ambazo ni;
1. Video haikuchezwa Mahakama ya Kisutu
2. Vielelezo hivyo vinatolewa kabla ya wakati.
3. Shahidi namba 3 hana uwezo wa kutoa vielelezo hivyo.
4. Upande wa mashitaka haujaonyesha mnyororo wa vielelezo katika utunzaji wake.
Upande wa Mashitaka walipinga mapingamizi hayo na Mahakama imejiuliza swali moja je mapingamizi hayo yana mashiko?
Jaji Ndunguru anaendelea kusoma.
Mahakama imeona ianze na pingamizi la tatu. Je Shahidi huyo ni competent au laa?
Mshitakiwa alisema shahidi huyu hana nguvu ya kisheria na hayupo kwenye orodha kwa mujibu wa GN. No. ... kwahiyo huyu sio mtaalamu anayepaswa kuja kutoa ushahidi.
Shahidi huyo hakuteuliwa na DPP kwa ajili ya kushughulikia hizi video na kutoa ushahidi wa namna hii.
Nao upande wa Mashitaka walijibu hoja hiyo ya Mshitakiwa na kuipinga. Wakairejea shauri la Mirzai na kusema shahidi ni mtu ambae alichunguza na kuandaa ripoti. Kwahiyo anaweza kutoa vielelezo hivyo hapa Mahakamani.
Pia Wakili wa Serikali alisema hizo video ni ushahidi wa kielektroniki hivyo unapaswa kupokelewa Mahakamani kwani sheria inaruhusu na kutoa vigezo vitatu ambao ni relevant, material na competent.
Vigezo vyote vimekidhi katika kuhakikisha ushahidi huo unapokelewa.
Pia Wakili wa Serikali alirejea Dictionary kueleza maana ya mtaalamu wa video na picha.
Mshitakiwa katika kujibu hoja za Serikali alisisitiza kuwa shahidi mtaalamu ni lazima awe ameteuliwa na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali kama ambavyo GN. inasema.
Sasa Mahakama imefuatilia na kuchunguza kwa makini na kuamua Shahidi namba 3 ni competent na ananuwezo wa kutoa hiyo flash kwa maana ya video.
Mshitakiwa anasema shahidi hana uwezo wa kisheria kutoa hiyo flash.
Kama tulivyokubaliana vigezo ni vitatu ambavyo ni relevant, material na competent na pia shahidi anapaswa kuwa competent.
Shahidi namba 3 ni shahidi mtaalamu na sheria inasema huyo sio shahidi facts ni shahidi wa utaalamu.
Experts witnesses ni lazima wawe wameteuliwa na DPP na wametangazwa kwenye gazeti la Serikali.
Shahidi namba 3 alitangazwa kwenye gazeti la Serikali wa kuchunguza picha mwaka 2022.
GN hiyo ilitengenezwa kwa mujibu wa kifungu cha 216 cha sasa katika aya ya pili ya gazeti hilo inasema Watu ambao majina yao yameorodheshwa ni wataalamu wa picha.
GN. hiyo iliyotengenezwa kwa mujibu wa kifungu cha 216 ambacho kinampa mamlaka DPP kuteua wataalamu. Kinasema nanukuu, anakisoma hapa.
Ukisoma kifungu hicho kinazungumzia shahidi kuandaa photographic print au photographic enlargement.
GN. no. 745 imetengenezwa kwa mujibu wa kifungu cha 216 pamoja na mambo mengine inahitajika awe na Certificate ambayo itataja majina yake na kuelezea namna alivyopokea kazi ya kuchunguza na alivyofanya.
Hapa tunamaanisha ni report ya mtaalamu.
Hivyo basi kama kifungu ndio kinasema hivyo lazima tafsiri ya kila kitu kiwe kwenye njia hiyo.
Part 133 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 131
Anaendelea Mhe. Lissu kufanya Rejoinder
Anasema kwahiyo Katuga ameleta hicho kifungu cha 70 kwa kutoelewa anazungumza na kuipotezea muda Mahakama akiwa anazungumza jambo gani?
Twende kwenye hoja ya nne.
Hoja ya Chain of Custody ambayo ni hoja ya nne.
Maamuzi yote niliyowasilisha mimi na waliyowasilisha wao Mawakili wa Serikali linalosema shahidi anaweza kuleta ushahidi kutoka mfukoni mwake.
Chain of custody is about paper trail na kesi inayosema hivyo ni Paul Maduka hajaigusia kabisa ukurasa wa 18 na 19 kesi imesema chronological documentation and all paper trail shows the seizure, transfer and disposition must be documented.
Waheshimiwa Majaji ushahidi unaoombwa upokelewe una hiyo chronological documentation uliyosemwa na Mahakama ya Rufani kwenye Paul Maduka?
Je una hiyo paper trail?
Naomba ikumbukwe huyu ni shahidi mtaalaamu na kwenye ushahidi wake aliandikiwa barua na vielelezo vililetwa kwa maandishi afanye uchunguzi wa hivyo vielelezo.
Hizo barua hazijawasilishwa, anasema nikisign dispatch haijaletwa mahakamani.
Anasema alivituma kwa requesting authority na kwamba vimerudije kwake tena hajasema lolote.
Leo ametuletea hivi vielelezo sisi hatujui vimefikaje kwake tena.
Wamefanya mambo kienyeji sana na mambo ya kienyeji hayakubaliwi Mahakamani.
Sasa ushahidi wa namna hii unakubaliwaje Mahakamani?
Nitamkumbusha maneno yake Wakili wa Serikali kuwa alisema Mahakama hii sio ya MAMA YANGU na Mimi namwambia leo kuwa MAHAKAMA HII SIO YA MAMA YAKE KATUGA WALA MAMA YAKE NA HUYU SHAHIDI.
Anasimama Katuga anasema Waheshimiwa Majaji Mahakama hii sio ya Mama yetu wote.
Mhe. Lissu anasema ni sawa KAMA MAHAKAMA SIO YA MAMA YETU WOTE basi na WEWE USIFANYE MAMBO KAMA UNAENDA KWA MAMA YAKO.
Tufuate tu utaratibu hicho ndio ninachokisema na ndo maana naomba vielelezo hivi visipokelewe na Mahakama hii kwa hizo hoja nne nilizosema toka awali na kusisitiza kwa sasa.
Anawaachia Majaji sasa wanaandika.
Kwa kifupi Mh. Lissu amemaliza na gia kubwa sana.
Watoto wa Mjini wanasema amepiga sana kwenye MSHONO kwa hizi nondo majaji sijui watasema tunarudi lini kwa ajili ya uamuzi mdogo wa mapingamizi haya.
Wanaandika pale mbele na kuteta kidogo.
Jaji Ndunguru anasema baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili uamuzi utatolewa siku ya Jumatano tarehe 22/10/2025 saa tatu asubuhi.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 130.
Mhe. Lissu anaendelea kufanya Rejoinder
Anasema Kwenye hoja ya pili bado nasimamia hoja ya pili kwamba video zilipaswa zitamabuliwe na taarifa ya mtaalaamu ambae ni shahidi.
Kesi ya Mirza Katuga anasema ni prosecution plan kuwa prosecution wanapanga nani wakuleta kielelezo.
Hoja nimesema kielelezo kinahusika na utaalamu basi kifuate taratibu za utaalamu.
Hoja ya tatu kuhusu competence ya shahidi vifungu kuanzia vya 216 na kuendelea, kusingekuwa na umuhimu wa sheria kusema wateuliwe.
Kinachofanya wawe wataalaamu sio maneno yao bali ni uteuzi wao.
Katuga anasema shahidi ameonysha utaalamu wake.
Je huyu ni mtaalamu? Ameteuliwa? Kama hajaonesha kuwa ni mtaalamu maneno yake ni kazi bure.
Shahidi huyu amesema kwamba ameteuliwa kwa mujibu kwa gazeti la serikali No. 799/2020 na vilevile amesema ameteuliwa kwa mujibu wa gazeti la serikali no. 745/2020
Hayo magazeti ni Sheria na ni nyaraka za kisheria. Wakili wa Serikali hakusema lolote kuhusu GN. No. 799/2020. Na anasema tusiende huko.
Na mimi nasema lazima twende huko kwasababu ni mtaalamu wa picha na sio mtaalamu wa video.
Wapo wataalamu walioteuliwa na DPP kwa ajili ya video huyu hayupo. The are withholding important information, wanaficha nyaraka muhimu na wakitaka walijibie.
Hii ni sheria ambayo walipaswa kuileta kwenu lakini walikaa kimya ni sheria inayohusiana na ni akina nani ambao ni wataalamu wa kisayansi wa mitandao ambapo wapo kwenye GN. No. 823/2024.
Ukiisoma hii GN wapo 27 hao wataalamu hayupo Samweli Elibariki Kaaya kwenye hiyo orodha.
Majaji wanateta sana hapo kama dakika 10 nadhan wanafikiria Mhe. Lissu aruhusiwe kuitoa hiyo Sheria au haruhusiwi.
Jaji ilikuwa ni haki kwa mshitakiwa kuijibia hoja hiyo maana hata Jamhuri mlituletea maana ya picha mkatuambia kuhusu dictionary.
Kwahiyo mshitakiwa endelelea.
Mhe. Lissu anawasomea hiyo GN hapo juu iliyowataja hao ma experts na anasema kwa kiswahili inaitwa AMRI YA UTEUZI WA WATAALAMU WA KISAYANSI WA MTANDAO aya ya pili ya Tangazo hilo inasema mtu ambae jina lake limetajwa katika jedwali anateuliwa kuwa mtaalamu wa kisayansi wa mtandao katika mashauri yoyote ya jinai na masuala yoyote kama hayo kwa mudhumuni hayo.
Jedwali hilo limeorodhesha watu 27 na huyu shahidi hayumo.
Amesimama Katuga anasema anaanza kutaja majina asifike huko.😂
Katuga hajui kama majina yametajwa kwenye hiyo GN yenyewe.
Huyu mtaalamu wao wamekuja nae mfukoni hayupo kisheria, hajatajwa kwenye tangazo la serikali na hajawahi kuteuliwa.
Jaji anasema hiyo ni sheria sasa kama watu wameandikwa tutaona na tutaona nani yupo na nani hayupo kwahiyo muiachie Mahakama tu.
Waheshimiwa Majaji Sharif Athuman Ukurasa wa 8 Jaji Masatti amesema:
But admissibility of evidence, it is also about the competence of the witness. It is not only about relevance, materiality and...
Jaji amesema competence ya shahidi inaweza kuwa general au specific.
Kwa huyu shahidi ni suala specific kwasababu tunazungumzia mambo ya mitandaoni na shahidi ambae anapaswa kutoa huo ushahidi ni ambae katangazwa kwa kazi hiyo.
Hivyo admissibility ya ushahidi huu inahitaji mtaalamu wa cyber forensic na sio mwingine na nimewapa hapo GN ambayo DPP ameteua watu wake.
Wakili wa Serikali anasema shahidi amesema mengi kuwa yeye ni mtaalamu.
Ni wasilisho langu kuwa kwa vile hayupo kwenye gazeti la Serikali na sio mtaalamu wa chochote huyu shahidi ni wajibu wa Mahakama kujiuliza kwa mujibu wa sheria je huyu ni mtaalamu na ameteuliwa kama nani?
Sayansi ya mtandaoni wameteuliwa yumo?
Kwenye picha za kawaida za makaratasi hilo halibishaniwi hapa, asubiri siku tukiwa na kesi ya makaratasi atakuja.
Haya ya leo ni masuala ya kimtandao.
Kifungu cha 70(1) cha Evidence Act kwamba ushahidi wa kielektroniki unakubalika hata mimi najua hilo ila hoja ni kwamba je anayeleta ushahidi kateuliwa?
Hii ndo hoja ya msingi.
Part 130 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
@swahilitimes Kwa hiyo Sheikh kabeke anataka kutuambia kwamba tz hakuna haki kwa sababu hakuna amani? Na wao wanaubiri amani kwa sababu amani hiyo haipo tz?
Ninyi viongozi wa dini mtaipoteza amani hapa tz kwa kuipuuzia haki
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 129
Anaitwa Mh. Lissu.
Anasimama na kusema naomba na mimi nitoe Rejoinder yangu baada ya kuwasikiliza Mawakili wa Serikali.
Nitafuata utaratibu huo huo ambao wao wameufuata walipokuwa wanajibu mapingamizi yangu.
Kuhusiana na hoja ya kwanza.
Je hizo video zilichezwa Kisutu?
Je nyaraka zingine zote zilisomwa ukiaichia witness statement. Je video zilionyeshwa?
Waheshimiwa majaji mashauri ya Kisutu yalikuwa ni hadhara yalifanyika hadharani members of the public pia walikuwepo.
Amesimama Katuga anasema huko kwingine hatukwenda, tuliishia kwenye Court Records pekeee. Tusimuache aende mbali zaidi.
Lissu Mh. Jaji video hazikuchezwa na kama Wakili wa Serikali anasema hadharani kuwa video zilichezwa maana yake tuna shida kubwa sana.
Waheshimiwa Majaji, je ni kweli kwamba hii rekodi ya Kisutu haikuwa impeached? Wakili anasema kwamba record ya Mahakama haiwezi kuwa impeached?
On the question of record: kuna ruling mbili za Mahakama hii juu ya integrity ya hiyo record mtakumbuka kwamba record hii haikusema chochote juu ya majina ya mashahidi niliowataja.
Anasimama tena Katuga anasema hii ni Rejoinder tunaona anaanza kuingiza vitu vipya tena.
Katuga anaogopa kuna mambo kusemwa. 😂 anasema vitu vipya.
Mhe. Lissu anasema hii rekodi nimeichallenge mara kadhaa.
Hiyo page 92 exhibit zimekuwa listed na page 93 inasema the records has been read out.
Hiyo kuandika hivyo haina maana ukweli wangu unabadilika. It doesn't change my position.
Sitaki kukubali jambo ambalo ni uongo.
Mimi sipendi uongo na ukweli wa kwamba video haikuchezwa kisutu utabaki kuwa hivyo hapa Duniani na hata Mbinguni.
Siwezi jidanganya au kutenda dhambi ya namna hiyo namuachia Katuga pengine yeye amezoea dhambi na kudanganya mambo ambayo sio ya kweli.
Video hazikuonyeshwa anasema zimeonyeshwa tena kwa ujasiri wa kusema hadharani na hapa mahakamani.
Niendelee sasa.
Katuga anasema pia kuwa mimi nilisema kuwa sikatai maneno yangu ya tar. 03/04 pale Makao Makuu ya Chama.
Nilichosema mimi ni kuwa hizi video haziko sahihi kupokelewa kwasababu hazikuonyeshwa Kisutu.
Kwa vile hazikuonyeshwa Kisutu haziwezi kuonyeshwa hapa, zilikuwa listed YES. Hazikuonyeshwa na haziwezi kutolewa hapa Mahakama.
Kuhusu mimi kusema sina shida navyo swali linabaki kuwa haviwezi kupokelewa kama havimeet masharti ya kisheria.
Amerejea mashauri ya Mahakama ya rufani wakati natoa hoja yangu. Shauri la Sharif Mohamed @Athuman, Lemina Omary Abdul na Musa Ramadhani Magai.
Hakuna kesi mbili zinazofanana kwa kila jambo. Kitu muhimu what is the principle ambayo inatokana na mashauri hayo yote matatu.
Principle ni kwamba nyaraka na vitu vyote vinavyotajwa katika mashauri kabidhi kama ni vya kusomwa visomwe na kama ni vya kuonyeshwa lazima vionyeshwe kwahiyo ulitakiwa kuonyeshwa huu ushahidi kule Kisutu.
Mahakama ya rufani ilisema the issue is not authenticity basi issue ni compliance of the law.
Kwenye hoja hii ya kwanza videos ambazo hazikuonyeshwa Kisutu haziwezi kuonyeshwa hapa.
Naomba sasa niende kwenye hoja ya pili.
Kwenye ushahidi wa shahidi ambae anadai yeye ni mtaalamu.
Kitu cha kwanza ni taarifa yake ya kitaalamu na sio alichokifanyia kazi.
Katuga amesema kwamba hakuna sheria mahususi inayolazimisha tuanze na Report badala ya kuanza na video iliyochunguzwa na alisema inantegemea na mazingira ya kesi.
Hajasema mazingira gani ya kesi hii ambayo yanataka ianze report na baadae video.
Sasa katika kesi hii tunayo report ya uchunguzi asa ripoti ndio inayo estabalish genuinely ya hicho kilichofanyiwa uchunguzi.
What is the legal logic ya kutanguliza video na kuacha report ya mtaalamu.
Ukisoma vifungu 216 hadi 223 vya CPA vinasema kuhusu ripoti na sio video na ndio maana ya mfano wangu wa mkokoteni na punda.
Ushahidi wa kitaalamu unahitaji kuletwa na mtaalamu na baada ya ushahidi kuo kuletwa ndio utazingatiwa.
Part 130 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 128
Anaendelea Katuga naomba sasa nihamie kwenye hoja ya nne.
Mshitakiwa anasema vielelezo visipokelewe eti akiwamaambia kwamba vielelezo hivi vimevunja mnyonyoro wa utunzaji.
Watu wanacheka. 😂😂😂
Ni mnyororo kumbe.
Amesema Chain of custody inathibitishwa na paper trail. The gist of chain of custody ni kuifanya mahakama ione kielelezo ni chenyewe au au vipi?
Mshitakiwa anasema kilipita kwa Michael Gyumi, sijui kikaenda kwa nani? Hicho kilichosemwa hakijajionyesha kwenye ushahidi wa shahidi wetu.
Ametajwa Churu, baadae Malugala na kujazwa ile PF No. 145.
The issue of chain of custody can no be established by a single witness. Utunzaji wa kielelezo hauwezi kuthibitishwa na shahidi mmoja.
Kuleta pingamizi la kwamba Chain of custody imevunjwa na kisipokelewe huku ni ku misplace mapingamizi.
Haya ni maneno ya Mahakama ya rufani R vs Charles Abel Gazilabo na wenzake 3 Rufaa ya jinai No. 358/2019.
Ukurasa wa 17 imejitokeza inshu ya chain of custody na kusema itatumika na kuangaliwa baada ya ushahudi wa upande wa Jamhuri ukifungwa. Prosecution case ikiwa closed sio muda huu.
Kwa maamuzi hayo Mahakama itaona hii hoja haijakuwa established kabla ya kupokelewa kwa kielelezo ila imeletwa kwa kubahatisha na kupoteza muda wa Mahakama ni ombi letu muitupilie mbali.
Kwa mapingamizi hayo yote tunaona hayana msingi kabisa na naomba niwarejeshe kwenye maamuzi aliyowaletea kesi ya Musa, Lemina Omary Abdul na Kesi ya DPP VS Sharif Mohamed.
Mashauri hayo yote yalikuwa yanahusu vielelezo ambavyo havikuwa vimesomwa au listed kwenye records.
Hayakuwa mashauri ambayo yanaonesha vielelezo kutosomwa, sisi kwetu hapa kwenye kesi hii vilisomwa na kuonyeshwa pale Kisutu.
Kwa kumalizia wakati wa hoja ya Competence pia Mahakama ilialikwa ikasome taarifa ya PW3 tulishangazwa sema tukakumbuka Mshitakiwa ni mtaalaamu wa kesi za Madai na sio jinai.
Tunaomba submission zetu ziwe considered na naomba kuishia hapo.
Renatus Mkude anamualika Ignas Mwinuka na anaomba aongeze kidogo.
Nitasema kwenye ile ground ya committal. Nitaomba mrejee ukurasa wa 93 wa Mwenendo kabidhi Mahakama imeandika, S. 263 of CPA has been complied with. Hii ni kuonesha kuwa taratibu zote ambazo zipo zilizingatiwa kwa mujibu wa Sheria.
Naomba niwarejeshe kwenye shauri la Mahakama ya rufani Jamhuri Vs Christian Muhaka Criminal Revision no. 7/2017.
Naomba Waheshimiwa Majaji kwenye shauri hilo Mahakama wa rufani wakiquote mwenendo kabidhi na kusema hawakuona mapungufu kwasababu vifungu vikiandikwa na vikishaandikwa maana yake utaratibu ulifuatwa.
Kwahiyo naomba kusisitiza kuwa hoja hiyo isikubaliwe na kuzingatiwa na mapingamizi yake yasizingatiwe na yatupiliwe mbali. Naomba kuishia hapo.
Anasimama Renatus Mkude anasema ni mwisho wa hoja zao na tunaomba kusisitiza kuwa mapingamizi yatupiliwe mbali, wanakaaa.
Tusubiri Rejoinder kutoka kwa Mhe. Lissu sasa.
Atajibu vimbwanga vyao hapa.
Part 129 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 127
Anaendelea Katuga
Shahidi alitambua vielelezo pale kizimbani na ndio maana tunasema vipokelewe, alisema hawezi kutufundisha na sisi tunataka akitufundisha atufundishe kutoka kwenye Sheria.
Naomba niende kwenye hoja ya tatu ambayo inasema shahidi sio competent kutender hii exhibit na kwenye hoja hii aliialika Mahakama kwenye vile vifungu vingi kuanzia 216 hadi 221 vya CPA.
WAKATI KATUGA ANAENDELEA NI KAMA NIMEWAONA HAWA ASKARI MAGEREZA WANAOMLINDA MH. LISSU WAPO WAGENI NA SURA ZAO ZIMEKAA KAMA WALE WENZETU KWELI. WAPO WAGENI NDIO WAMELETWA HAPA. SIJUI WANA MPANGO GANI NA HAWA WALINZI WAO.
Acha tuendelee na Katuga sasa
Anataja vifungu vyote alivyovitaja Mh. Lissu na vinazungumzia nini? Kingereza chake ni kibovu sana. Akisoma mahali ZE ZE ZE ZE ZE ni nyingi sana.
PW 3 amejieleza kama yeye ni mtaalamu na alialikwa kufanyia kazi vielelezo na amejipambanua kuhusiana na umri wake na utaalamu wake. Na alifanyia kazi vielelezo hivi hivyo basi kifungu cha 52 cha Evidence Act Cap. 6 kinasema mtu mwenye uelewa na fingerprints, na ujuzi mwingine basi yanapokelewa.
Kila shahidi yuko entitled kuaminiwa unless Mahakama ije na sababu za kutomuamini.
Kesi ya Goodluck Kyando Vs Jamhuri TLR 2006 Every witness is entitled to credence.
Shahidi wetu anaomba kutoa memory card yenye video, flash yenye video.
Kifungu cha 70 cha Evidence Act Cap. 6 kinasema in any proceedings electronic evidence shall be admissible.
Mahakama ya rufaa imetoa visifa vya vitu inavyotakiwa kuzingatia kabla ya kupokea vielelezo.
Kesi maarufu ya DPP VS Sharif Mohamed, Athumani and 6 others CA 74 2016.
Kesi inasema mtu aliyefanyia kazi kielelezo ni competent ku tender pia kesi ya DPP vs Mirzai inatoa utaratibu huo wa kisheria.
Naomba kesi hizi zote nizitoe kwa Mahakama na mshitakiwa pia.
Amekuwa appointed na gazetted kwa kufanya uchunguzi na kutoa taarifa ndio kazi ya shahidi huyu.
Yeye ni shahidi wa picha mnato na mjongeo Gazeti la serikali no. 745/2022 ndio lilimtangaza kwa ajili ya kufanya uchunguzi na kutoa taarifa.
Tangazo hilo limesainiwa na DPP na kwamba title ya tangazo lile ni amri ya uteuzi wa wataalamu wa picha na mambo mengine.
Mtaalamu wetu anasema yeye ni mtaalamu wa picha mnato na picha mjongeo na mimi naialika mahakama itafute meaning ya picha, is video a picture? Vifungu vya 216 na kuendelea havioneshi mtaalamu wa video, hayupo.
Kifungu cha 220 cha CPA kwamba video ni cyber forensic expert, tafsiri ya CYBER ziko nyingi sana ikiwa ni pamoja na ushahidi wa Computer ndo maana yake.
Anachunguza devices utambuzi wa uhalisia wa picha utabaki kwa mtambuzi wa picha. Is a video a picture? Video ni picha za muendelezo.
Hapa cyber experts na photographic expert wasichanganywe ni watu wawili tofauti.
Kuna definition mbalimbali lakini kuna dictionary ya computer and internet terms ukurasa wa 363 alitafsiri photograph is a picture created by a camera whether digital or video. Ukurasa wa 513
Anasema Jaji unaenda kwa kasi sana hatukuelewi kwakweli hata unakimbilia wapi.
Au Mshitakiwa unasemaje Jaji anamuuliza. Lissu anajibu Mimi namuangalia tu naona anaongea ongea, nimemuacha.
Jaji sasa sisi tunaona ujielekeze vizuri ukiendeleea kujiongelea wewe sisi hatutaandika.
Haya rudia hapo sasa kwenye Dictionary taratibu.
Part 128 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.