AFRIKA NI KWA AJILI YA WAAFRIKA.
β Timu zote zinatolewa katika mazingira yanayofanana.
β Timu zinashindwa hata kukaa na Mpira kwa Dakika 2 tu wakati wanaongoza.
Walichokifanya Misri leo ni zaidi ya kupoteza mchezo, wamedhalilishwa πππ.
Namungo FC wana hali mbaya lakini kwenye kile kikosi chao kuna huyu Abdulkarim Kiswanya, football anayocheza ni kama ana misimu Mitano kwenye ligi, mtulivu, makadirio ya muda na ufasaha wa kupiga pasi, anapiga ile Six ya kisasa, WA KUZINGATIWA HUYU π.
Ederson sio Mtu wa kawaida, ni Allien, kumfananisha na viungo wengine ni sawa na kumtishia Maji ya kwenye Bakuli anaemiliki Bahari, jamaa kawaomba viongozi wa United wamkate Mshahara kila atakapopigwa Chenga, viongozi walikataa kitu ambacho kilimfanya alie mpaka kupoteza fahamu.
Ndugu zangu Arsenal, kufurushi changu cha Dua njema kilikomea pale tu mliposhinda taji la EPL, niwatakie kipigo chema chenye Fedheha, Manyanyaso, Masimango na Udhalili, kwa ufupi tu kitakachowatokea leo itakuwa ni sawa na kuweka kalio kwenye Kichuguu cha Siafu π€£.
James Akaminko yupo Azam FC lakini ni kama hayupo, kuna namna Klabu yake haijapata manufaa kamili ambayo pengine yaliwafanya wamsajili, vs mechi kubwa anauwasha halafu hujui nini kinatokea baadae, anakuwa kimya.
Tukiwa fair kabisa Uwanja wa Mkwakwani umepoteza ubora wa kuchezewa mechi za Ligi Kuu NBC, kinachotokea hapa kwa Coastal v Mashujaa mpira hautulii kabisa, unadunda sana, nadhani kwa mustakabali wa Mpira unahitaji maboresho πππ.
Nelson Munganga, mchezaji senior kuliko wote pale Dodoma Jiji, athari yake inaonekana ndani ya Uwanja, Munganga ni kiungo haswa, anacheza football ambayo kwa vijana wengi huipati πππ.
Swali la Meena na jibu la Rio havikumaliza hata DK 5 katika sehemu ya mahojiano yao waliyoyafanya, Watanzania tumechagua aina yetu ya maisha, silioni kosa pale, Rio ametoa maoni kama mpenda football mwengine wa kawaida, tulitaka aseme NO COMMENT kama wasemavyo watu wa Mpira?.
Pale ambapo alipaswa kukemewa wenye timu walisimama nae licha ya aina ya utovu wa nidhamu aliouonyesha, kawaida kama utashindwa kumkanya mwanao kwa Mdomo amini Jirani atamchoma na Njiti ya Kibiriti, yes anaweza kuwa sababu ya Yanga kupoteza leo, kama mmenielewa lakini.
Chama vs Aziz Ki
Chama vs Pacome
Chama vs Feisal
Chama vs Okello
Bila shaka Chama ndio standard ya Viungo Washambuliaji wanaohitajika kwenye ligi yetu, kama nimeuelewa huu mjadala lakini.
Tatizo huwa tunachukulia poa sana tuhuma ndogondogo, kwa wanaotuhumu ilibidi wazingatiwe kisha uchunguzi ufanyike ili kubaini ni kweli au sikweli, lakini huku kuupuzia madhara yake huwa ni makubwa kisha misemo ya WALISEMA, ALISEMA, WANGEFANYA ianze kutawala kwenye Vinywa vyetu.
Wakati Chama anarejea Simba nilisema kuwa Chama mwenye Mguu mmoja anaweza kuwa bora mbele ya namba Kumi wengi kwenye hii ligi, Chama amechoka tu Mwili sio Akili πππ.
Kama Pedro atakuwa wanalazimika kumtoa Damaro kwa kuhofia Kadi Nyekundu basi hiyo si sawa, Damaro anahitaji kuboresha sana game yake, kwanini anacheza sana faulo? kwa sababu anachelewa kwenye matukio, akiboresha hilo basi atakuwa muhimili zaidi kwa timu yake.