π’ FURSA ZA MASOMO CHINA 2027/2028 π¨π³π
TASAFIC inawatangazia Watanzania fursa za masomo nchini China kwa ngazi za Bachelor, Master na PhD.
π Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti na mitandao rasmi ya TASAFIC.
πΉπΏ TASAFIC β Elimu na Umoja, Tuijenge Tanzania!
πΉπΏπ€ WUTASA WELCOME PARTY 2026 π¨π³
Wanafunzi wa Kitanzania jijini Wuhan, kupitia jumuiya ya WUTASA, wawakaribisha wanafunzi wapya kwa furaha na mshikamano. β€οΈπ
#TASAFIC#WUTASA#TanzaniansInChina#WelcomeParty2026
Katibu Mkuu DITAG akitoa hotuba fupi na salamu za heri wakati wa Mahafali ya TASAFIC 2026 yaliyofanyika jijini Wuhan. DITAG walisisitiza umuhimu wa ushirikiano thabiti na jumuiya ya wanafunzi, huku wakiwasihi wahitimu kutumia vema ubunifu na ujuzi wa kiteknolojia
Wawakilishi kutoka kampuni ya usafirishaji ya FOX Cargo wakitoa neno mbele ya Mgeni Rasmi na hadhara ya Mahafali ya TASAFIC 2026.
Katika salamu zao, FOX Cargo waliwapongeza wahitimu wote na kueleza utayari wao wa kuendelea kutoa huduma bora, salama na za gharama nafuu
Mgeni Rasmi, Mh. Balozi Dk. Suleiman Haji Suleiman, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi/waakilishi kutoka Benki ya NMB (Wadhamini Wakuu wa Mahafali). Uhusiano wa karibu kati ya Serikali kupitia Ubalozi wetu nchini China, Jumuiya ya TASAFIC, na sekta binafsi kama Benki ya NMB
Mgeni Rasmi, Mh. Balozi Dk. Suleiman Haji Suleiman, katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe (Organizing Committee). Nyuma ya pazia la mahafali haya makubwa na ya kuvutia, kuna nguvu, muda, na ubunifu wa vijana hawa waliojitoa usiku na mchana.
Picha ya pamoja yenye tabasamu za ushindi! Mgeni Rasmi, Mh. Balozi Dk. Suleiman Haji Suleiman, akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wote wa TASAFIC wa mwaka 2026. Hii ni taswira ya nguvu kazi mpya, yenye weledi na uzalendo, iliyo tayari kulitumikia Taifa letu. Hongereni sana
SALAMU ZA UONGOZI: Mwenyekiti wa TASAFIC akihutubia hadhara na kuwakaribisha wageni waalikwa katika Mahafali ya TASAFIC 2026 yaliyofanyika jijini Wuhan. Katika hotuba yake, alieleza mafanikio makubwa ambayo shirikisho limeyapata, changamoto zilizovushwa, na kuwashukuru wanafunzi
Mwakilishi kutoka Benki ya NMB akitoa salamu na hotuba maalum mbele ya Mgeni Rasmi na hadhara ya Mahafali ya TASAFIC 2026. Benki ya NMB, kama mshirika na mdhamini mkuu, imedhihirisha kwa vitendo dhamira yake ya kuunga mkono sekta ya elimu.
Mgeni Rasmi, Mh. Balozi Dk. Suleiman Haji Suleiman, akihutubia na kutoa nasaha zake za dhati kwa wahitimu na wanafunzi wote waliohudhuria Mahafali ya TASAFIC 2026. Katika hotuba yake, alisisitiza umuhimu wa kutumia maarifa na teknolojia waliyoipata nchini China kurudi nyumbani.
Kazi ya pamoja ndio siri ya mafanikio yetu! Mgeni Rasmi, Mh. Balozi Dk. Suleiman Haji Suleiman, akigawa tuzo za heshima kwa kamati mbalimbali za TASAFIC zilizofanya vizuri zaidi na kuonyesha utendaji uliotukuka katika kipindi hiki.
#UmojaNiNguvu#TuzoZaUfanisi#NMBBank
Mgeni Rasmi wetu, Mh. Balozi Dk. Suleiman Haji Suleiman, akikabidhi vyeti vya shukrani kwa viongozi wa TASAFIC waliomaliza muda wao wa uongozi.
Uongozi wa TASAFIC unatoa shukrani za dhati kwa viongozi hawa kwa uzalendo, kujitoa, na kuiongoza jumuiya yetu kwa ufanisi mkubwa.
Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Balozi Dk. Suleiman Haji Suleiman, akitunuku vyeti kwa wahitimu wa TASAFIC 2026 katika mahafali yaliyofanyika jijini Wuhan. Huu ni mwanzo wa safari mpya ya kuitumikia na kuijenga Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia taaluma zilizopatikana nchini China.