Tazama mratibu wetu mkoa wa Arusha wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wajane 2026 na hitimisho la Kampeni ya Malezi Chanya, tukishirikiana na Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Fahamu jinsi tunavyopambana kulinda haki za mirathi na kutoa msaada wa kisheria.
Msaada wa Kisheria kwa Wajane: TAWLA Katika Kilele cha Siku ya Wajane Ar... https://t.co/ssjSnKVBik
#HakiHainaJinsia
Kupitia ushirikiano huu wa kimkakati, tunaendelea kuimarisha utetezi wa usawa wa kijinsia, kulinda haki za msingi za wanawake na watoto, na kuchangia kikamilifu katika utekelezaji wa ahadi za kikanda na kimataifa ambazo Tanzania imeridhia chini ya Mkataba wa CEDAW.
#UsawaWaKijinsia
#HakiHainaJinsia
@TawlaTZ kwa kushirikiana na @WiLDAFTz na @scitanzania, tumefanikisha kikao cha kazi cha kupitia Rasimu ya Ripoti Mbadala ya Asasi za Kiraia kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake(CEDAW) nchini Tanzania.
#UsawaWaKijinsia
#HakiHainaJinsia
Kikao hiki kimeleta pamoja wadau muhimu kutoka Wizara mbalimbali za Serikali na Asasi za Kiraia (CSOs) kwa lengo la kuhakiki taarifa, kuboresha mapendekezo, na kuhakikisha ripoti ya mwisho inaakisi kwa usahihi hali halisi, fursa, na changamoto zinazowakabili wanawake na wasichana nchini.
#UsawaWaKijinsia
#HakiHainaJinsia
If a fat solidifies on your plate, imagine what it’s doing to your arteries.
This quick clip is just a teaser. For the full deep-dive explaining industrial trans fatty acids and how they increase the risks of cardiovascular diseases, watch the full video on YouTube: https://t.co/xV8L8nyrSR
#TransFatFreeUG #TransFatFreeEAC
Every shopping trip is a health decision, but only if the information is clear.
Our digital advocates share why Front-of-Pack Warning Labels (FOPWL) matter to every Kenyan. Simple warnings on the front of food packages can make it easier to spot products high in sugar, salt, saturated fat, or total fat before they reach your basket.
#FoodPolicyKE #FoodPolicy #WhatsInMyFoodKE
#SipSmartChallenge26 is the way to start the second half of the year. As we daily share reminders to prioritize health and remind you that #SSBTaxSaves
Wadau walipata fursa ya kubadilishana uzoefu kuhusu mafanikio, changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao, pamoja na kujadili sababu zinazochangia baadhi ya mashauri kucheleweshwa au kukwama katika mnyororo wa utoaji haki na kuja na mbinu za pamoja za kuondokana na changamoto hizo.
Majadiliano hayo yaliibua uelewa wa pamoja kuhusu vikwazo vilivyopo katika mfumo, na yaliimarisha ushirikiano kati ya taasisi mbalimbali za utoaji haki.
#J4S
#HakiHainaJinsia
@TawlaTZ tumeendesha kikao maalum na wadau wa mfumo wa utoaji haki (justice actors) ambacho kilibainika kuwa jukwaa muhimu la kujadili masuala ya kitaaluma na kiutendaji katika mfumo wa haki.
Kikao hicho kilichofanyika mkoani Kigoma kilihusisha Mahakimu, Waendesha Mashtaka, Maafisa Polisi kutoka Dawati la Jinsia na Watoto, Madaktari kutoka One Stop Centres, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii pamoja na Wasaidizi wa Kisheria kutoka maeneo ya mradi ya Kibondo, Kasulu na Kigoma Mjini.
#J4S
#HakiHainaJinsia
Kupitia mafunzo haya, pamoja na kuongezeka kwa uelewa kwa washiriki, @TawlaTZ tumefanikiwa kujenga mtandao wa wanahabari walioko Kigoma ambao itaendelea kushirikiana nao katika kutumia taaluma yao kama nyenzo ya kuelimisha jamii na kuendeleza ajenda ya usawa wa kijinsia.
#WezeshaBinti
#SautiYaHaki
#HakiHainaJinsia
Kwa kutambua nafasi ya waandishi wa habari kama chachu muhimu ya mabadiliko ya kijamii, @TawlaTZ kupitia mradi wa Sauti ya Haki Kigoma chini ya programu ya Wezesha Binti inayofadhiliwa na shirika la Enabel, tumetoa mafunzo maalum kwa waandishi wa habari kuhusu ukatili wa kijinsia (GBV), usawa wa kijinsia, haki za wanawake na watoto wa kike, pamoja na misingi ya uandishi wa habari unaozingatia haki za binadamu na maadili ya taaluma.
#WezeshaBinti
#SautiYaHaki
#HakiHainaJinsia
Mafunzo haya yaliyofanyika mkoani Kigoma yalihusisha waandishi kutoka vyombo mbalimbali vikiwemo redio, televisheni, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii (social media). Ushiriki huu mpana uliwezesha mijadala ya kina kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuelimisha jamii, kuzuia ukatili wa kijinsia, na kuendeleza usawa wa kijinsia.
#WezeshaBinti
#SautiYaHaki
#HakiHainaJinsia
Kadri wanawake wanavyoshiriki zaidi kwenye tasnia ya habari, ndivyo sauti tofauti na mawazo mapya yanavyoongeza ubora wa vyombo vya habari. #WomenInMediaTz@TAMWA_
IJUE KATIBA ya Ijumaa ya leo ni kutoka Ibara ya 111 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,inayosisitiza Jaji wa Mahakama Kuu hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapishwa kwanza kiapo cha uamunifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi
Obesity is not a lifestyle choice; it is the result of an industry that floods our markets with soda and spends billions convincing us to drink it. #SSBTax#SSBTaxSaves
To reduce your salt or sodium intake, embrace a diet garnished with fruits and veggies and eliminate junks from your plate. By doing this, you will not only enhance your health but also improve the quality of your diet.
#SaltReduction#HealthyDiets
Kama wadau wakuu wa msaada wa kisheria na mapambano dhidi ya ukatili, @TawlaTZ tulishiriki uzinduzi wa kampeni ya ushuhuda wa sauti za manusura wa ukatili wa kijinsia na kingono, ulioandaliwa na WATED Tanzania na Tree of Hope kwa udhamini wa GIZ.
Katika kuimarisha uhusiano wetu wa kikazi na wadau, @TawlaTZ tulipata wasaa wa kutoa salamu za taasisi kwa wananchi, tukihimiza jamii kuacha muhali, kupaza sauti, na kudai haki kupitia sheria. Pamoja tunaweza kutokomeza ukatili.
#VunjaUkimya
#PingaUkatiliWaKijinsia
#HakiHainaJinsia