Takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Polisi zinaonesha ukatili wa kingono kwa jinsia zote umeshuka kutoka matukio 12,749 mwaka 2024 hadi 11,625 mwaka 2025. Hayo yameelezwa leo na Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
"Nasisitiza waandishi wa habari kushiriki kuwania Tuzo za Samia Kalamu Awards 2026, kwa kuwa waandishi ndio daraja kati ya serikali na wananchi, tuone umuhimu wa kusemea miradi yetu hatua tunazopiga za kimaendeleo ili zijulikane duniani". Dkt Kannaeli Kaale - Mwenyekiti TAMWA
“Mchakato wa kupokea kazi unaanza rasmi leo 31 Mei 2026 na kuhitimishwa 30Juni 2026 kupitia tovuti rasmi ya Tuzo https://t.co/tpFbY72U4Q. Kazi zitakazopokelewa ni zilizochapishwa na kurushwa kuanzia 1 Julai 2025 hadi 30Juni 2026”. Mhandisi Peter Msalyanda - Mkurungenzi TCRA
TCRA na TAMWA kwa kushirikiana na JAB zimezindua, Msimu wa pili wa Tuzo za uandishi wa habari za maendeleo za "Samia Kalamu Awards 2026" leo May 31, 2026. @ithibati
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania- TAMWA leo kinaungana na watanzania wote katika kuadhimisha Siku ya Malezi kitaifa. TAMWA inaendelea kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa malezi na makuzi salama ya watoto wa kike na wa kiume.
Wawakilishi kutoka Thomson Foundation wameitembelea ofisi ya TAMWA na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa TAMWA, Dk Rose Reuben. Majadiliano hayo yalijikita katika mikakati ya maendeleo, fursa za mashirikiano yanayolenga kuimarisha vyombo vya habari na maendeleo ya jamii.
Tunaamini mdahalo huu wa leo utaleta mawazo chanya, ubunifu, na kutoa suluhu za pamoja katika kutokomeza ukatili wa kijinsia bila kumuacha yeyote nyuma,” Dr. Rose Reuben Mkurugenzi wa TAMWA. #SautiZetu#ZuiaUkatili#GIZ
Leo TAMWA kwa kushirikiana na GIZ wanaendesha mdahalo wa kitaifa wa ushiriki wa wanaume katika kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto #ZuiaUkatili#SautiZetu#GIZ
TAMWA inajivunia kuwa mjumbe wa Kamati kuu ya maadhimisho na kilele cha Sherehe za Uhuru wa Vyombo vya Habari, 2026 yenye kauli mbiu: Kujenga Mustakabali wa Amani- Kukuza Uhuru wa Vyombo Vya Habari kwa ajili ya haki za binadamu, maendeleo na Usalama.
Leo, tarehe 30 Aprili 2026 TAMWA kwa kushirikiana na mradi wa Sauti Zetu unaosimamiwa na GIZ, kimefanya ziara katika Kituo cha Jumuishi cha Mwananyamala. Lengo la ziara hiyo lilikuwa kujifunza na kufahamu kwa kina namna kituo hicho kinavyoshughulikia na kusimamia kesi za ukatili
"Wanahabari tuanze kubadilika kwa kuandika habari za kina zenye uchambuzi, ili kututofautisha na wasio na taaluma ya uandishi wa habari na kujijengea imani kwenye jamii" Dkt Rose Reuben -Mkurugenzi TAMWA
TAMWA leo imeshiriki ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani,yanayofanyika kitaifa, mkoani Arusha. Maadhimisho ya WPF kwa mwaka huu yanaangazia nafasi ya vyombo vya habari katika kuchechemua uhuru wa Habari kwa Haki za Binadamu,Maendeleo na Usalama.
"Mpaka kufikia 2035 tunatakiwa kuwa na vyombo vya habari vinavyozalisha maudhui yenye tija na kuthamini waandishi wa habari kwa ajili ya habari zenye tija kwa taifa" Dkt Rose Reuben - Mkurugenzi -TAMWA #Worldpressfreedomday#WomenInMediaTz#Vikes#IMS