Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma leo ametembelea ofisi za Bodi ya Ithibati jijini Dar es Salam na kusisitiza usimamiaji madhubuti wa utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari, nidhamu, maadili na udhibiti wa wanaofanya kazi bila Ithibati.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, akijibu hoja mbalimbali za wadau wa habari wakati wa majadiliano baada ya kuwasilisha mada kuhusu umuhimu wa ithibati kwa waandishi na watangazaji wa habari nchini.
Machumu ni miongoni mwa waandishi waliopokea vitambulisho vyao leo na ameonesha furaha yake kupata Ithibati na Kitambulisho hicho akibainisha kuwa anajisikia fahari kuwa miongoni mwa Waandishi wanaotambulika rasmi kwenye taaluma kwa mujibu wa sheria.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari-JAB Wakili Patrick Kipangula akimkabidhi Kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Presscard) Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BSM Washauri (TZ) na Mhariri Mkongwe Bakari S. Machumu, 13 Agosti, 2025.
Akizungumza mara baada ya kupokea kitambukisho chake Kibanda amesema, anajisikia fahari kuwa na Kitambulisho hicho kinachompa ari na kutembea kifua mbele akiwa ni mwanataaluma aliyekidhi vigezo ya kisheria.
#ithibatitz#ithibatikidijitali
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari-JAB Wakili Patrick Kipangula akimkabidhi Kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Presscard) Meneja Mwenza wa Kampuni ya The Media Brains na Mhariri Mkongwe Absalom Kibanda leo tarehe 12 Julai, 2025 jijini Dar es Salaam