TEMDO imetoa Mafunzo kwenye Maonesho na Mafunzo ya Biashara ya Mitambo na Mashine za Uzalishaji wa Bidhaa za Viwanda, Kilimo, Mifugo na Bidhaa zinginezo kwenye ukumbi wa SHIRECU yalio andaliwa na Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Mkulima akipata maelezo ya kina ya teknolojia ya kuchakata zao la chikichi ili kupata mafuta ya kula kutoka kwa Mtalamu Mosses Chalamila alipo tembelea banda la TEMDO katika maonesho ya Nane Nane kanda ya Kaskazini.
Mkulima wa zao la chikichi akipata maelezo ya teknolojia za kuchakata mafuta ya mawese kutoka kwa mtalamu Moses Chalamila alipo tembelea banda la TEMDO katika maonesho ya Nane Nane kanda ya Kaskazini.
TEMDO yashiriki kwenye uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (Pan African Post Uniuon - PAPU) lenye ghorofa 17. Jengo hili litazinduliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Taasi ya TEMDO imeshinda nafasi ya kwanza kwenye sekta ya Viwanda Vidogo kwenye mashindano ya Kaizen. Tuzo hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil T. Abdullah. Picha habari ni Watalamu wa TEMDO Dr. Sigisbert Mmasi na Allice Ndosi
Wakurugenzi na Maafisa Wakuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wametembelea TEMDO kwa lengo la kuangalia Maendeleo ya Teknolojia zinazo tengenezwa kama vile Mradi wa Vifaa Tiba, Mtambo wa Kuchakata zao la Muhogo, Mtambo wa kuchakata Sukari na Mkonge.
TEMDO yashiriki Maonesho ya Nane Nane kanda ya Kaskazini na Mashine za aina mbali mbali kwaajili ya kuongeza dhamani kwenye Mazao; Pia wana Vifaa Tiba kwaajili ya kusaidia hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati hapa Nchini.
Mkulima akipata maelezo ya kina ya teknolojia ya kuchakata zao la chikichi ili kupata mafuta ya kula kutoka kwa Mtalamu Mosses Chalamila alipo tembelea banda la TEMDO katika maonesho ya Nane Nane kanda ya Kaskazini.
TEMDO imeshiriki maonesho ya 29 Nane Nane 2023 na Teknolojia mbalimbali kama vile Mtambo wa kumamua na kusafisha mafuta ya Alizeti, Mtambo wa kuchakata unga wa Muhogo, Mtambo wa kuchakata siagi ya karanga, Mtambo wa kuchakata unga wa lishe, Mtambo wa kuchakata juisi ya matunda.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Notredame wame tembelea TEMDO kwaajili ya kujionea Ubunifu na Usanifu wa kazi za Kihandisi, lengo kuu la ziara ya shule hiyo ni kuwaandaa Wanafunzi wapende masomo ya Sayansi.
Uongozi na Watumishi wa TEMDO wanapenda kumpongeza Mjumbe wa Bodi Dkt. Liliane Joseph Pasape kwa kupandishwa cheo kutoka Mhadhiri Mwandamizi " Senior Lecturer" kuwa Profesa Mshiriki "Associate Professor" katika Taasisi ya Nelson Mandela. "Hongera sana Prof. Pasape".
Mwenyeketi wa Bodi ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) Mhandisi Dkt. Richard Masika (Kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO Mhandisi Prof. Frederick Kahimba Wametembelea Banda la TEMDO katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara (DITF)
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO Eng. Prof. Frederick C Kahimba alipo tembelea maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF)
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe akipata maelezo ya Tafiti na Bunifu zilizo buniwa na Taasisi ya TEMDO katika maonesho 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF)
Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji akipata Taarifa ya Maendeleo ya Mtambo wa Kuchakata Sukari kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO Eng. Prof. Frederick C. Kahimba. Prof. alipata pia fursa ya kuelezea Mafanikio ya Mradi wa Vifaa Tiba.