Hali kadhalika kujifunza unasihi wa afya ya akili uliofanyika kwenye Serikali ya Mtaa Sinza na pia shughuli zilizofanyika kwenye Ofisi ya TEWWY. Vikao hivi huviita Linking & Learning.
Kwenye program yetu ya shule ya Sekondari a Mashujaa washiriki huwa ni Mwakilishi mmoja wa walimu, wanafunzi wawili ambao ni Mabalozi wa Afya ya Akili hapo shuleni, akina mama Wanasihi wawili na timu ya TEWWY.
“Katika kutekeleza programs zetu na wadau, TEWWY ina utaratibu wa kufanya vikao ili kupeana taarifa za utekelezaji angalau kila baada ya miezi miwili. Mathalani, katika program ya shule tunajifunza kilichofanyika kuhusu afya ya akili shuleni kutoka kwa walimu na wanafunzi.
@TEWWYWisdom inawatakia Watanzania wote Noel yenye furaha na mwaka mpya wa matumaini na mafanikio 2024 tukijua kuwa Hakuna Afya Bila Afya ya Akili na kwamba, Kwa Pamoja tuna Nguvu ya Kuhamasishana na Kushinda! #HappyHolidays#SeasonsGreetings#HappyNewYear
Watu wanaofanya mazoezi mara kwa mara wana afya ya Akili iliyo bora zaidi na wana ustawi wa kihisia na viwango vya chini vya ugonjwa wa Akili;
Siyo lazima mazoezi yawe ya nguvu, yenye mpangilio maalum au yale yanayochukua muda mrefu ili kupata faida;
Zoezi lolote ni bora kuliko kukaa bila kufanya zoezi lolote. Wataalamu wanapendekeza kuwa, watu wazima lazima wajitahidi kufanya mazoezi zaidi karibia kila siku,
tuzingatie kufanya mazoezi, tusidharau. Mazoezi ni kwa afya zetu wenyewe, hususani, afya zetu za akili. Tuzilinde
- Zungumza matatizo yako na mtu unayemuamini;
- Usijitenge, shirikiana na jamii inayokuzunguka;
- Tenga muda wa kufurahisha mwili;
- Shiriki shughuli za kijamii;
- Tenga muda wa kupumzika
Afya ya Akili ni hali ya utimilifu wa kifikra, kihisia, kisaikilojia na kijamii ambayo huonekana kwa namna tunavyotenda, tunavyofikiri na tunavyohisi.
Ili kuweza kuwa na hali hiyo, zingatia haya:
- Fanya mazoezi na michezo;
- Kula vizuri;
- Pata usingizi wa kutosha;
c) vyakula vingine, kafeini na pombe vinaweza vikaingiliana na madawa yanayotumika kutibu matatizo ya afya ya Akili
Hivyo yatupasa tuwe waangalifu, daima yatupasa tuangalie nini tunakula na nini tunakunywa. Afya njema ya mwili na afya ya Akili ni muhimu kuzingatiwa.
Sikiliza,
Ni muhimu kwa kila mtu kula mlo kamili, kunywa maji mengi na kuwa mwangalifu na kiasi cha pombe na kafeine unayotumia. Kwa mfano watu wenye matatizo ya afya ya akili, angalizo hili ni la muhimu zaidi kwa sababu:
a) kula na kunywa kiafya kunaweza kukaboresha baadhi ya dalili za matatizo ya Afya ya Akili;
b) ulaji na unywaji mbaya usiozingatia afya unaweza ukafanya dalili mbaya za Afya ya Akili zikawa mbaya zaidi;