Tanzania Interfaith Partnership (TIP) is a consortium of national faith Organizations that have become partners in the effort to mitigate the impact of HIV/AIDS
Katika picha mbalimbali hapo ni viongozi wa dini na wataalam kutoka TIP wakiwa katika kikao kazi kupitia vitini vya masuala ya maji, usafi wa mazingira na usafi binafsi. Kikao hicho kimemalizika leo mjini Morogoro
Shirika la Tanzania Interfaith Partnership (TIP) kwa kushirikiana na shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa mataifa (UNESCO) leo wamezindua rasmi mwongozo wa elimu kuhusu afya ya uzazi na haki kwa vijana katika sherehe fupi zilizofanyika leo jijini Dar es salaam.
Timu za soka za TIP za walimu wa shule za msingi na timu ya vijana wa digitali kutoka halmashauri ya wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza jana walitoka sare kwa kufungana mabao matatu kwa matatu katika mechi ya kirafiki iliyofanyika jana katika uwanja wa Nyehunge Buchosa.
Wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kwa kushirikiana na shirika la Tanzania Interfaith Partnership (TIP) jana walifanya uzinduzi wa sera ya nyongeza ya ushirikishwaji majukumu katika kupinga ukatili wa kijinsia na ukatili kwa watoto.
MINISTRY OF HEALTH is inviting you to a scheduled Zoom meeting.
Topic: Launching of Gender Based Violence and Violence Against Children (GBV&VAC) Task sharing Policy Guidelines Addendum For Health Sector Services in Tanzania
Join Zoom Meeting
https://t.co/eXIvOI43v6
Zoezi la upimaji VVU katika wilaya zote ambazo TIP imefanya kazi lilijumuisha kazi za kuweka vifaa katika vituo vya upimaji vilivyoko kwenye nyumba za ibada na safari za visiwani ambako huduma nyingi za afya hazifikiki.
Siku ya leo TIP imekamilisha ziara ya kukabidhi miradi kwa kufanya zoezi hili katika ngazi ya mkoa kwa viongozi wa serikali na wa kidini. Hapo ni picha mbalimbali za mawasilisho na ripoti.
Shughuli ya TIP kuaga na kukabidhi mradi kwa halmashauri na viongozi wa dini imeendelea tena ambapo halmashauri ya wilaya ya mwisho ilikuwa ni Kwimba.
Pichani ni matukio tofauti wakati wa makabidhiano hayo
Shughuli za kukabidhi mradi wa BORESHA FCI katika wilaya ya Buchosa.
Ya kwanza na ya pili ni picha ya pamoja. Ya tatu ni mratibu wa UKIMWI wa halmashauri ya wilaya Chacha na ya nne ni makabidhiano ya ripoti ya miaka miwili kwa wawakilishi wa serikali na kwa viongozi wa dini.
Baadhi ya vijana wa TIP kutoka halmashauri ya wilaya ya Buchosa wanaoshiriki kampeni za kupitia mitandao ya kijamii kuhamasisha upimaji VVU kwa wanaume na watoto na kupinga ukatili wa kijinsia wakiwa katika picha ya pamoja jana.
Vijana wa TIP kutoka wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza, ambao wanashiriki kampeni ya upimaji VVU na kupinga ukatili wa kijinsia hasa wa kingono kwa watoto, jana waliandaa hafla maalum kwa ajili ya kuelimishana kuhusu masuala ya afya ya uzazi ikiwemo VVU na stadi nyingine za maisha
Vijana kutoka wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza wamo katika mafunzo yanayoendeshwa na TIP kuhusiana na Afya ya Uzazi na Stadi za maisha.
Pichani ni mratibu mwandamizi wa ufundi kutoka TIP Shukuru Mohammed akiendesha moja ya vipindi vya mafunzo hayo leo jijini Mwanza.
Governments across the world including Tanzania have committed to end child marriage by 2030 through the Sustainable Development Goals (SDGs). Around 650 million women and girls alive today were married as children.
#ZuiaUkatiliKwaWototo@agpahi@UnitedNationsTZ
Mwili wa aliyewahi kuwa katibu mkuu waTEC Padri Raymond Sabba umeagwa leo jijini Dar es salaam tayari kwa safari ya kwenda Kigoma ambako mazishi yake yatafanyika. Padri Sabba alifariki tarehe tatu 3/8/21 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, 🙏🏿