🔴🔴 *TAWA YAANDIKA HISTORIA AFRIKA, SELOUS NA MPANGA-KIPENGERE ZATWAA TUZO ZA WORLD TRAVEL AWARDS 2026*
Na Beatus Maganja, Zanzibar
TANZANIA imeandika historia mpya katika ramani ya utalii barani Afrika baada ya Hifadhi ya Selous na Hifadhi ya Mpanga-Kipengere, zinazosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), kuibuka washindi katika tuzo za World Travel Awards 2026, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Mamlaka hiyo kuingiza maeneo yake katika mashindano hayo makubwa ya utalii.
Ushindi huo wa kihistoria ulitangazwa wakati wa hafla ya 33 ya World Travel Awards iliyofanyika Agosti 28, 2026 katika Hoteli ya Diamonds Bijoux, Bwejuu, Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar na kuifanya TAWA kuanza safari yake katika tuzo hizo kwa mafanikio makubwa baada ya kuingiza maeneo matatu katika kategori mbalimbali na mawili kati yake kuibuka washindi.
Maeneo hayo ni Hifadhi ya Selous, Hifadhi ya Mpanga-Kipengere pamoja na Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara ambayo yaliingia katika ushindani dhidi ya baadhi ya vivutio vinavyotambulika zaidi katika sekta ya utalii barani Afrika.
Katika kategori ya Africa’s Leading Tourist Attraction 2026, Selous, Mpanga-Kipengere na Kilwa Kisiwani zilichuana na baadhi ya vivutio maarufu zaidi barani Afrika vikiwemo Pyramids of Giza nchini Misri, Table Mountain, Robben Island na V&A Waterfront nchini Afrika Kusini, Okavango Delta nchini Botswana na Lake Malawi.
Kutoka Tanzania, ushindani huo ulihusisha pia Mount Kilimanjaro, Ngorongoro Conservation Area, Amani Nature Forest Reserve na Pugu Hills Forest Reserve. Katika ushindani huo mkubwa, Hifadhi ya Selous iliibuka mshindi, ikiweka historia kwa TAWA katika ushiriki wake wa kwanza kwenye tuzo hizo.
Kwa upande wake, Hifadhi ya Mpanga-Kipengere nayo iliandika historia baada ya kuibuka mshindi katika kategori ya Africa’s Leading Honeymoon Destination 2026 ikichuana na Marrakech nchini Morocco, Mozambican Islands, Okavango Delta nchini Botswana, Red Sea Riviera nchini Misri, Volcanoes National Park nchini Rwanda pamoja na Kitulo National Park ya Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hizo, Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Semfuko, aliwashukuru Watanzania kwa kuvipigia kura vivutio hivyo na kuchangia ushindi huo huku akieleza kuwa mafanikio hayo yametokana na ubunifu, bidii na kujituma kwa Bodi, Menejimenti na watumishi wa TAWA katika kuhakikisha maeneo yanayosimamiwa na Mamlaka yanaendelea kuboreshwa na kuwa na mvuto zaidi kwa shughuli za utalii.
“Siri kubwa ya ushindi huu ni ubunifu wa vijana wangu wote, kuanzia Bodi mpaka wafanyakazi wote kujituma. Lakini kubwa zaidi ni bidii wanayoifanya katika kuhakikisha kwamba maeneo yetu yanakuwa mazuri kwa ajili ya utalii,” alisema Semfuko.
Semfuko alisema ushindi huo unaongeza nguvu katika dhamira ya TAWA ya kuendeleza utalii wa ndani na kufungua zaidi maeneo yanayosimamiwa na Mamlaka kwa Watanzania na wageni kutoka nje ya nchi.
“Tulimuahidi Mheshimiwa Rais kwamba TAWA tutakuwa vinara wa utalii wa ndani. TAWA tunataka kufanya makubwa Zanzibar... mtaona kishindo cha mwaka kesho,” alisema.
Naye Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Mlage Y. Kabange, mbali na kuwapongeza Watanzania waliovipigia kura vivutio hivyo, alisema Selous na Mpanga-Kipengere ni sehemu tu ya hazina kubwa ya vivutio vinavyosimamiwa na Mamlaka katika maeneo mbalimbali nchini.
Kabange alisema TAWA inaendelea kuboresha miundombinu katika maeneo yake ili kuongeza mvuto, kuwezesha wageni kuyafikia kwa urahisi zaidi na kuendelea kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa kwa watalii.
“Tuna maeneo mengi zaidi. Tunaendelea kuboresha miundombinu yake ili yaweze kuvutia wageni zaidi. Tunawaahidi Watanzania kwamba tutaendelea kutoa huduma bora zaidi katika maeneo yetu,” alisema Kabange.
Ushindi wa Selous na Mpanga-Kipengere unaifanya Agosti 28, 2026 kuwa siku muhimu katika historia ya TAWA.
#worldtravelawards2026
#selousgamereserve
#mpangakipengeregamereserve
#honeymoondestination
#Tanzania
*ZANZIBAR
Agosti 14, 2026*
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Tamasha la Kizimkazi limekuwa sehemu muhimu ya kuchochea maendeleo ya Kizimkazi na Zanzibar kwa ujumla, kwa kuwa limeendelea kufungua fursa mbalimbali za uwekezaji, biashara na maendeleo ya wananchi.
Rais Samia amesema hayo wakati akifunga tamasha la 10 la Kizimkazi ambapo amefafanuwa kuwa , tamasha hilo limekuwa likiibua miradi ya maendeleo na kuwavutia wawekezaji pamoja na wageni kutoka ndani na nje ya Zanzibar, akieleza kuwa miradi mbalimbali iliyozinduliwa kupitia tamasha hilo inaakisi malengo ya kuunganisha shangwe, fursa na maendeleo kwa wananchi.
Amesema viongozi wanapaswa kuhakikisha fursa zinazopatikana kupitia tamasha hilo zinawafikia wananchi na kuwa na manufaa ya muda mrefu, ikiwemo kuboresha huduma za msingi kama maji, barabara na miundombinu mingine muhimu.
Rais Samia ameongeza kila mwaka tamasha hilo limekuwa likionyesha mabadiliko katika sekta mbalimbali, hivyo kuwahimiza wawekezaji na watu wenye nia ya kutumia fursa zilizopo kuendelea kuja Kizimkazi na Zanzibar kwa ujumla kuwekeza.
Aidha, Dkt. Samia ameitaka jamii, hususan vijana, kuendelea kulinda amani na utulivu uliopo nchini, akisisitiza kuwa amani ni chachu kubwa ya maendeleo na msingi wa wananchi kutumia fursa za kiuchumi na kijamii.
Rais Samia pia amewashukuru kamati ya maandalizi ya Tamasha la Kizimkazi pamoja na wazawa wa eneo hilo kwa ushirikiano waliouonesha katika kuwapokea na kuwahudumia wageni wakati wote wa tamasha.
Sambamba na hilo amewapongeza wadau na wadhamini walioshiriki katika kufanikisha tamasha hilo, pamoja na viongozi walioweka misingi ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa upande wake, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuunga mkono maono ya Tamasha la Kizimkazi katika kutangaza na kuenzi mila, silka na utamaduni wa Zanzibar.
Dkt. Mwinyi amesema taasisi za Serikali, wafanyabiashara, wajasiriamali na wadau wengine wamekuwa sehemu muhimu ya kufanikisha tamasha hilo, huku wazawa wakishiriki na kunufaika na fursa zinazotokana na shughuli mbalimbali zinazofanyika wakati wa tamasha.
Amesema Serikali itahakikisha tamasha hilo linatunzwa na kuendelezwa ipasavyo, sambamba na kuhakikisha miundombinu inayojengwa kupitia shughuli hizo inadumu na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa Tamasha la Kizimkazi linaendelea kuwa chachu ya maendeleo si kwa Kizimkazi pekee, bali pia Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, kutokana na uwezo wake wa kuunganisha watu, fursa za biashara, utalii na uwekezaji.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hamida Mussa Khamis, amesema Tamasha la Kizimkazi limekuwa chachu ya maendeleo na limeibua fursa kwa wananchi katika sekta mbalimbali, ikiwemo afya, elimu, ajira, biashara na utalii.
Hamida amesema tamasha hilo lililofikia awamu ya 10 limeendelea kuwaunganisha wananchi na fursa mbalimbali za kiuchumi. Amesema wafanyabiashara 129 walisajiliwa kushiriki tamasha hilo, huku zaidi ya wafanyabiashara wadogo 200 wakinufaika na shughuli za kibiashara.
Amesema vijana wamepata fursa za ajira kupitia sekta ya utalii, wakati wavuvi nao wameendelea kunufaika na fursa zinazotokana na uwezeshaji wa shughuli za uvuvi.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema tamasha hilo pia limeimarisha umoja na ushirikiano kati ya wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara, hivyo kuendelea kuwa jukwaa muhimu la kuunganisha watu, utamaduni na fursa za maendeleo.
Kwa upande wake, Haroun Ali Suleiman amesema jitihada hizo ni miongoni mwa matokeo ya uongozi wa Awamu ya Nane katika kuendeleza Kizimkazi na kuhakikisha wananchi wanapata fursa zinazotokana na shughuli za maendeleo na uwekezaji.
Tamasha la Kizimkazi 2026 limeendelea kuwa jukwaa la kuibua fursa za kiuchumi, kutangaza utalii, kuenzi utamaduni na kuchochea uwekezaji, huku viongozi wakisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu na kutumia fursa zinazopatikana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Semfuko amewakaribisha wananchi wote kutembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.
Aidha, Mej. Jen (Mst) Semfuko ameongeza kuwa TAWA imeendelea kuboresha Bustani ya Wanyamapori kwa kuleta Wanyamapori wapya kama vile Tembo na Twiga na amehaidi kufanyika kwa maboresho makubwa kwenye Bustani ya Wanyamapori kuelekea mashindano ya AFCON.
#TALIINASABASABA
#DITF50
#AFCON2027
Mtayarishaji wa Tamthilia Maarufu Nchini inayojulikana kama Kombolela, Abdul Juma Usanga amewakaribisha wananchi wote wa viunga vya Dar es Salaam kutembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii hususan Bustani ya Wanyamapori.
Sambamba na hayo, TAWA inawakaribisha wananchi wote kutembelea Banda lake lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ili wapate maelezo kuhusu mambo mbalimbali yakiwemo:
📍 Shughuli za Utalii na Uhifadhi zinazofanywa na TAWA pamoja na fursa za Uwekezaji zinazopatikana katika maeneo mbalimbali yaliyo chini ya usimamizi wa TAWA
📍Fursa ya Kujionea Wanyamapori Hai kupitia bustani ya wanyamapori iliyopo ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa Shilingi za kitanzania 3,000 (Wakubwa) na 1,000 (Watoto)
📍 Elimu kuhusu Wanyamapori na mazingira yao.
📍OFA Maalum ya Ziara ya kutembelea Hifadhi ya Pande iliyopo Jijini Dar es Salaam, kwa gharama ya shilingi za kitanzania 35,000. Safari hii inaanzia katika viwanja vya Sabasaba.
📍Fursa ya kupata nyamachoma safi iliyoandaliwa kwa ustadi na utaalamu.
*BODI YA WAKURUGENZI TAWA YAKUTANA NA MKUU WA MKOA WA TABORA*
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inayoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Mej.Jen (Mst) Hamis Semfuko imekutana na kufanya mazungumzo na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Chacha.
Akizungumza katika kikao hiko kilichofanyika Juni 14,2026, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA, Mej.Jen ( Mst) Semfuko amesema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano baina ya TAWA na Uongozi wa Mkoa wa Tabora katika uhifadhi ya rasilimali wanyamapori katika maeneo yanayosimamiwa na TAWA ndani ya Mkoa wa Tabora ikiwemo Mapori ya Akiba ya Igombe na Luganzo Tongwe pamoja na Bustani ya Wanyamapori Tabora.
Sambamba na masuala ya uhifadhi, Semfuko ameongeza kuwa TAWA inatarajia kufanya uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya kitalii katika Bustani ya Wanyamapori Tabora ambayo inatarajia kuleta manufaa ndani ya Mkoa wa Tabora ikiwemo kuongeza fursa za ajira kwa wananchi.
Kadhalika, Mej.Jen (Mst) Semfuko amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa mchango wake katika kuhamasisha wananchi kuzingatia sheria za uhifadhi na kushiriki katika juhudi za kupambana na ujangili. Aidha, ameongeza kuwa TAWA itaendelea kushirikiana na Uongozi wa Mkoa, katika utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu usimamizi wa maeneo ya hifadhi pamoja na kuimarisha mapambano dhidi ya ujangili kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikali.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Chacha, ameishukuru Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA kwa kutembelea Mkoa huo na kufanya kikao hicho muhimu.
Aidha, ameongeza kuwa Uongozi wa Mkoa utaendelea kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa masuala yote yaliyowasilishwa ili kuimarisha shughuli za uhifadhi ili kuhakikisha rasilimali za wanyamapori zinatunzwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kikao hiko kilihudhuriwa pia na Wakuu wa Wilaya za Kaliua, Sikonge, Igunga, Urambo pamoja na Nzega.
🌹 *Je, ni tofauti gani nyingine unazozijua kati ya CHUI na DUMA?*
🌹 Weka maoni yako hapo chini utujuze tofauti unazoziifahamu
🌹 Kwa “take-take” kama hizi, usikose kuendelea kufuatilia kurasa zetu rasmi:
🧅*Instagram:* tawa_tanzania
🧅*Facebook:* Tanzania Wildlife Management Authority
🌹 Yajayo yanafurahisha zaidi...kaa nasi ujifunze, uburudike na ugundue mambo mengi ya ajabu kuhusu wanyamapori wetu!
🌹 Did you know that Swagaswaga Game Reserve in Dodoma is home to the magnificent Roan Antelope — one of Africa’s most stunning and rare antelope species?
���� Come and experience the beauty of these majestic animals in their natural habitat and discover the wild charm of Swagaswaga Game Reserve.
🌹 Your unforgettable wildlife adventure awaits in Dodoma, Tanzania
It was an honour having you at Makuyuni Wildlife Park @Caamil8 Wananchi @YoungAfricansSC na wadau wote karibuni sana Makuyuni Wildlife Park!
@VisitMakuyuni
*MEJ. JEN (MST) SEMFUKO AWAVISHA VYEO VYA KIJESHI MAKAMISHNA WA UHIFADHI 13*
Na. Joyce Ndunguru, Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mej.Jen (Mst) Hamis Semfuko amewavisha vyeo vya kijeshi Makamishna wa Uhifadhi (13) katika hafla ya Kijeshi iliyofanyika Februari 21, 2026, katika Ofisi za TAWA Makao Makuu, Mkoani Morogoro.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mej.Jen (Mst) Semfuko aliwapongeza Makamishna kwa kuaminiwa na Bodi ya Wakurugenzi na kuteuliwa nafasi hizo katika maeneo mbalimbali ya usimamizi.
“Ninawapongeza Makamishna wote 13 waliotunikiwa na kuvishwa vyeo, ni imani ya Bodi kuwa mnastahili vyeo hivyo, hongereni sana,” alisema Mej.Jen (Mst) Semfuko.
Aidha, pamoja na pongezi hizo, Semfuko aliwaelekeza Makamishna waliovishwa vyeo kwenda kutekeleza maelekezo ya Serikali na maono ya Bodi ya nne ya Wakurugenzi ya TAWA ya kuhakikisha TAWA inapaa katika viwango vyote vya utendaji kazi ikiwemo; ushirikishaji wa jamii, usimamizi wa kazi za uhifadhi, kuendeleza Utalii, kuongeza uwekezaji na ukusanyaji wa mapato.
“Tunataka tuone TAWA inapaa juu zaidi na nyinyi ndio moja ya vichocheo vya kufanya hivyo,” alisema Semfuko.
Kadhalika, Mej.Jen (Mst) Semfuko aliwataka Makamishna wa uhifadhi kwenda kufanya kazi kwa kushirikiana na Maafisa na Askari walio chini yao kwa kuzingatia miongozo iliyopo huku wakizingatia ubunifu, weledi, sheria na utu.
Makamishna wa Uhifadhi waliovishwa vyeo ni pamoja na Makamishna Wasaidizi Waandamizi (7) ambao ni Privatus Kasisi, Wilbright Munuo, Khadija Malongo, Mark Chuwa, Vicky Kamata, Omary Msangi na Orest Njau.
Pia, Makamishna Wasaidizi (6) ambao ni Alphonce Mung’ong’o, Jackson Msaki, Suleiman Keraryo, Jovine Nachihangu, George Makheya na Rajabu Hochi.