The official account of the Embassy of Tanzania in Addis, Ethiopia. Also accredited to Djibouti, Yemen, the African Union & UN-Economic Commission for Africa.
Mr. Frank G. Mwega, Minister Plenipotentiary at the Embassy of the United Republic of Tanzania in Addis Ababa, today visited the Royal Norwegian Embassy in Addis Ababa on behalf of H. E. Ambassador Innocent E. Shiyo to convey Tanzania's condolences following the passing of His Majesty King Harald V of Norway.
Mr. Mwega signed the Book of Condolences and conveyed, on behalf of the Government and people of the United Republic of Tanzania, heartfelt condolences to the Royal Family, the Government, and the people of the Kingdom of Norway during this period of mourning.
Tanzania stands in solidarity with the people of Norway and extends its deepest sympathies to all those mourning the loss of His Majesty.
May His Majesty's soul rest in eternal peace. 🇹🇿🇳🇴
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe, leo Agosti 24, 2026 amewasili jijini Addis Ababa, Ethiopia kuungana na ujumbe wa Tanzania unaoongozwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Florence Samizi, katika Kikao cha 76 cha Kamati ya Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani (WHO), kinachofanyika Agosti 25–28, 2026.
Dkt. Magembe amepokelewa jijini Addis Ababa na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Innocent Shiyo pamoja na viongozi na watendaji wengine wa Tanzania waliopo nchini humo.
Katika ziara hiyo, Dkt. Magembe pia atashiriki katika mikutano mbalimbali ya pembezoni mwa mkutano huo pamoja na shughuli nyingine zinazohusiana na masuala ya afya na ushirikiano wa kimataifa kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu mbalimbali za kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo, unakuja wakati ambapo nchi inaendelea kutoa mchango muhimu katika ajenda ya afya ya bara la Afrika, ikiwemo katika eneo la afya ya mama, mtoto na afya ya uzazi ambayo inaendana na uteuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Kinara wa Umoja wa Afrika (AU) wa Afya ya Mama na Mtoto, nafasi inayodhihirisha dhamira na mchango wa Tanzania katika kuendeleza afya ya wanawake na watoto Barani Afrika.
TANZANIA YASHIRIKI KIKAO CHA 76 CHA KAMATI YA KANDA YA WHO KWA AJILI YA AFRIKA, ADDIS ABABA, ETHIOPIA
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashiriki katika Kikao cha 76 cha Kamati ya Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani -WHO) (76th Session of the WHO Regional Committee for Africa – AFR/RC76), kinachofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia, kuanzia tarehe 25 hadi 28 Agosti 2026.
Kikao hicho cha ngazi ya juu kinawakutanisha Mawaziri wa Afya na viongozi wakuu wa Serikali kutoka Nchi Wanachama 47 za Kanda ya Afrika, kwa ajili ya kujadili na kupitisha sera, mikakati na mipango ya kikanda inayolenga kuimarisha afya na ustawi wa wananchi barani Afrika.
Ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Mhe. Dkt. Florence George Samizi (Mb.), Naibu Waziri wa Afya, ambaye amewasili Addis Ababa akimwakilisha Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb.), Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Kikao hicho.
Ujumbe huo umepokelewa katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Addis Ababa na Mhe. Innocent Shiyo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ethiopia.
Kikao hiki ni chombo cha ngazi ya juu cha WHO katika Kanda ya Afrika, na ni jukwaa muhimu kwa Nchi Wanachama kutathmini kwa pamoja vipaumbele vya afya vya kikanda, kupitia utekelezaji wa ahadi na maamuzi yaliyokubaliwa, pamoja na kutoa mwelekeo wa kimkakati kuhusu changamoto za afya zinazoikabili Afrika.
Katika kikao hicho, Nchi Wanachama zinatarajiwa kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uimarishaji wa mifumo ya afya, kinga na udhibiti wa magonjwa, afya ya mama na mtoto, usalama wa afya, utayari na mwitikio dhidi ya dharura za kiafya, ugharamiaji wa huduma za afya, pamoja na maeneo mengine ya kipaumbele yenye umuhimu katika kufikia huduma bora za afya kwa wote na kuboresha hali ya afya barani Afrika.
Tanzania inatarajiwa kushiriki kikamilifu katika mijadala hiyo na kuchangia katika majadiliano ya sera za afya za kikanda, huku ikitoa uzoefu, vipaumbele na mafanikio ya nchi katika kuimarisha mfumo wa afya. Ushiriki huo pia unatoa fursa kwa Tanzania kubadilishana uzoefu na mbinu bora na Nchi Wanachama nyingine, pamoja na kuchangia katika kuandaa na kuimarisha hatua za pamoja za Afrika katika kukabiliana na changamoto za afya zinazolikabili bara. Afya ya mama na mtoto ni miongoni mwa vipaumbele vya Tanzania, ambayo inaendelea kuimarisha hatua za kupunguza vifo na kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora na kwa wakati kwa wanawake na watoto.
Kikao hicho pia kinatoa fursa kwa Tanzania kuendeleza ushiriki wake katika mipango ya afya ya kikanda na kimataifa, ikiwemo kuimarisha ushirikiano na ubia pamoja na kuhamasisha rasilimali kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele vya afya vya kitaifa na kikanda. Kupitia ushiriki wake, Tanzania itaendelea kuunga mkono na kutetea mifumo na mikakati inayoongozwa na Afrika katika kukabiliana na changamoto za afya zinazoikabili bara la Afrika.
Ushiriki wa Ujumbe wa Tanzania katika AFR/RC76 unaonesha dhamira endelevu ya Serikali ya kuimarisha mfumo wa afya nchini na kuchangia katika juhudi za pamoja za kuboresha afya na ustawi wa wananchi katika Kanda ya Afrika. Aidha, unathibitisha dhamira ya Tanzania ya kuendelea kushirikiana na WHO, nchi za Afrika na washirika wa maendeleo katika kujenga na kuimarisha mifumo ya afya yenye usawa, imara, inayoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali na endelevu, ili kuhakikisha hakuna anayesahaulika.
Ratiba ya Mhe. Dkt. Florence George Samizi (Mb.), Naibu Waziri wa Afya, imeanza kwa kushiriki katika Matembezi ya “Walk the Talk” kuelekea Mkutano wa AFR/RC76. Matembezi hayo yana ujumbe wa kuhimiza viongozi na wananchi kutafsiri kwa vitendo ahadi na sera za afya kwa kuzingatia dhana ya “Afya kwa Wote”, huku yakisisitiza umuhimu wa kuzuia magonjwa, kuimarisha maisha yenye afya na kujenga Afrika yenye afya na ustawi kwa wote.
TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA 13 WA SHIRIKISHO LA SEKTA YA AFYA AFRIKA MASHARIKI (THE 13TH EAST AFRICAN HEALTHCARE FEDERATION (EAHF) CONFERENCE)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya anayeshughulikia Dawa na Vifaa Tiba, Bw. Emmanuel Daud Tayari, anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliowasili Addis Ababa, Ethiopia, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 13 wa Shirikisho la Sekta ya Afya Afrika Mashariki (East African Healthcare Federation – EAHF), unaofanyika tarehe 21–23 Agosti 2026 Addis Ababa, Ethiopia, akimwakilisha Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa. Ujumbe wa Tanzania umepokelewa katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Innocent Shiyo.
Mkutano huo wenye kaulimbiu “Ustahimilivu: Kujenga Uchumi wa Afya wa Afrika Mashariki” (Resilience: Building the East African Health Economy) unalenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika sekta ya afya kwa kujadili na kuweka mikakati ya pamoja katika maeneo muhimu, yakiwemo uzalishaji wa dawa na vifaa tiba barani Afrika, ubunifu wa afya ya kidijitali, upanuzi na uboreshaji wa utoaji wa huduma za afya, uimarishaji wa mifumo ya fedha kwa ajili ya afya, pamoja na kujenga uwezo wa wataalamu wa afya katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Mkutano huu utajadili maeneo 10 muhimu yanayolenga kujenga mfumo wa afya wa Afrika Mashariki ulio imara, jumuishi, endelevu na wenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za sasa na zijazo, ambayo ni: Mifumo ya ufadhili wa huduma za afya (Re-imagining Healthcare Financing); Afrika Mashariki kuwa kitovu cha utalii wa tiba duniani (Positioning East Africa as a Global Medical Tourism Destination); Kuendeleza na kuimarisha ubora wa huduma za afya (Advancing Healthcare Quality); mgeuzi katika huduma za afya ya msingi (Reinventing Primary Health Care); Kubadilisha huduma za afya kupitia afya ya kidijitali na Akili Unde
(Transforming Healthcare through Digital Health and Artificial Intelligence); Kujenga nguvu kazi ya afya ya baadaye kwa Afrika Mashariki (Building the Future Health Workforce for East Africa); Usalama wa afya katika dunia yenye hali ya kutotabirika (Health Security in an Uncertain World); Kuharakisha uzalishaji wa ndani kwa ajili ya usalama na mamlaka ya afya (Made in Africa: Accelerating Local Manufacturing for Health Security and Sovereignty) na Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi: Kufungua fursa za uwekezaji katika afya (Public–Private Partnership: Unlocking Investment for Health).
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashiriki kikamilifu katika majadiliano hayo, ikiwa na msisitizo katika maeneo ambayo yana umuhimu wa kimkakati kwa maendeleo ya sekta ya afya ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla na itachangia katika maeneo yafuatayo: Vision 2035: Shaping the Future of East Africa’s Health, kwa kusisitiza umuhimu wa kuwa na maono ya pamoja ya kikanda yatakayowezesha nchi za Afrika Mashariki kujenga mifumo ya afya yenye uwezo wa kutoa huduma bora, zinazopatikana kwa wakati na kwa usawa, huku ikiimarisha uwekezaji, ubunifu, uzalishaji wa ndani na ushirikiano wa kikanda katika sekta ya afya; Kuiweka Afrika Mashariki kuwa Kitovu cha Utalii wa Tiba Duniani (Positioning East Africa as a Global Medical Tourism Destination; Aidha, Tanzania itachangia katika Kuendeleza na Kuimarisha Ubora wa Huduma za Afya (Advancing Healthcare Quality), na mwisho itachangia katika Kujenga Nguvu Kazi ya Afya ya Baadaye kwa Afrika Mashariki” (Building the Future Health Workforce for East Africa), kwa kutambua kuwa wataalamu wenye ujuzi, weledi na uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia ni msingi wa mifumo imara ya afya.
H.E. Khwauli Msiska, Malawi’s new Ambassador to Ethiopia, today paid a courtesy call on H.E. Ambassador Innocent E. Shiyo, Tanzania’s Ambassador to Ethiopia and Permanent Representative to the AU and UNECA.
The two Ambassadors praised the historic ties between Tanzania and Malawi and agreed to deepen economic cooperation and political dialogue.
They committed to expanding bilateral cooperation, exploring new areas of collaboration, and cooperate closely on regional and global matters, pledging support in international fora.
The meeting concluded with a shared determination to further strengthen Tanzania-Malawi friendship and partnership.
Mheshimiwa Balozi Innocent E. Shiyo alimkaribisha Mheshimiwa Rastislav Križan, Balozi wa Jamhuri ya Slovakia nchini Ethiopia, kwa ziara ya kujitambukisha katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Addis Ababa. Hii ilikuwa ziara yake ya kwanza katika Ubalozi wa Tanzania tangu kuwasilisha Hati zake za Utambulisho mwezi Juni 2026.
Mabalozi hao walibadilishana mawazo kuhusu namna ya kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano wa pande mbili, pamoja na ushirikiano katika diplomasia ya kimataifa na masuala ya kimataifa yenye maslahi ya pamoja kati ya Tanzania na Slovakia. Mazungumzo hayo yalisisitiza umuhimu wa kuendeleza mashauriano na uratibu katika majukwaa ya kimataifa, hususan katika kukuza amani, usalama na ushirikiano wa kimataifa.
Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Balozi Križan alieleza kuhusu uamuzi wa Serikali ya Slovakia wa kufungua upya Ubalozi wake jijini Dar es Salaam. Hatua hiyo inatarajiwa kutoa msukumo zaidi katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya Tanzania na Slovakia.
Kwa upande wake, Mheshimiwa Balozi Shiyo alimtakiwa Mheshimiwa Balozi Križan na Serikali ya Slovakia kila la heri katika maandalizi na utekelezaji wa majukumu yao watakapoanza kuhudumu kama Wajumbe wa wasio wa Kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) kwa kipindi cha 2028–2029, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano na uratibu katika masuala ya amani na usalama.
The Embassy of Tanzania joins @MFAethiopia for #GreenLegacy — growing a greener Ethiopia, together.
At the invitation of @MFAEthiopia, the Embassy of Tanzania participated in a tree planting program in Bishoftu city, as part of Ethiopia’s #GreenLegacyInitiative 🌳🇪🇹
The program united MoFA staff, the diplomatic corps, local communities, and the diaspora — a powerful example of collective action for environmental sustainability and climate resilience.
In his opening remarks, the Minister of Foreign Affairs of Ethiopia, Hon. Gedion Timothewos, called it “a day of planting hope — for the future, peace, environmental sustainability, and unity.”
With 48+ billion seedlings planted since 2019, the Green Legacy Initiative is about restoring ecosystems, enhancing climate resilience, creating green jobs, and securing a livable future for the next generation.
The Embassy is proud to contribute #ClimateAction #PlantingHope #Ethiopia
*COURTESY CALL BETWEEN H.E. AMBASSADOR INNOCENT E. SHIYO AND H.E. AMBASSADOR ADYLBEK TULTEMIROV REINFORCES TANZANIA–KYRGYZ REPUBLIC RELATIONS*
H.E. Ambassador Innocent E. Shiyo, Ambassador of the United Republic of Tanzania to the Federal Democratic Republic of Ethiopia and Permanent Representative to the African Union (AU) and UNECA, today received H.E. Adylbek Tultemirov, Ambassador of the Kyrgyz Republic to the Federal Democratic Republic of Ethiopia, who paid a courtesy call at the Embassy.
The two Ambassadors held cordial and productive discussions on ways to further strengthen bilateral relations between the United Republic of Tanzania and the Kyrgyz Republic. They exchanged views on enhancing cooperation in trade, investment, agriculture, tourism, education, information and communication technology, and capacity building, while emphasizing the importance of translating the existing cordial relations into tangible partnerships that deliver mutual benefits to the peoples of both countries.
The Ambassadors also underscored the importance of strengthening political consultations, promoting exchanges of high-level visits, and fostering closer collaboration between their respective Ministries of Foreign Affairs. They reaffirmed their shared commitment to expanding bilateral cooperation and exploring new avenues of engagement in areas of common interest.
On multilateral cooperation, the two Ambassadors commended the longstanding collaboration between Tanzania and the Kyrgyz Republic within the United Nations, the African Union, and other international and multilateral fora. They reaffirmed their commitment to maintaining close consultations on regional and global issues of common interest, promoting multilateralism, *and mutual support for each other's candidatures to international organizations,* on the basis of mutual understanding and reciprocity.
During the meeting, H.E. Ambassador Shiyo, on behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, extended his sincere congratulations to the Government and the people of the Kyrgyz Republic on their election as a non-permanent member of the United Nations Security Council for the 2027–2028 term. He noted that this historic achievement marks the first time the Kyrgyz Republic will serve on the Security Council and expressed confidence that Kyrgyzstan will make *meaningful* contribution to the promotion of international peace and security during its mandate, commencing on 1 January 2027.
The meeting concluded with both sides expressing their determination to further strengthen the longstanding friendship and cooperation between the United Republic of Tanzania and the Kyrgyz Republic for the mutual benefit of their peoples.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshiriki katika Mkutano wa 49 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika (49th Ordinary Session of the Executive Council) ambao unafanyika hapa Addis Ababa, Ethiopia ambao umeanza leo tarehe 28 hadi 29 Julai 2026. Ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Said Shaib Mussa akimuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb). Mkutano huo unalenga kujadili masuala mbalimbali ya kisera, kiutawala na kifedha yanayohusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Umoja wa Afrika pamoja na maandalizi ya Mkutano wa 8 wa Uratibu wa wa Umoja wa Afrika ambao utajumuisha Kamati ya Uongozi ya Umoja wa Afrika (AU Bureau of the Assembly), Jumuiya za Kiuchumi za Kikanda (RECs) na Mifumo ya Kikanda (RMs).
Akichangia katika mkutano huo, Balozi Mussa alieleza kuwa Tanzania inaunga mkono kupitishwa kwa Bajeti ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2027, huku akisisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa fedha za umma, uwajibikaji na uandaaji wa bajeti unaozingatia matokeo ili kuhakikisha kuwa rasilimali za Umoja zinatumika kwa ufanisi mkubwa na kuleta manufaa kwa wananchi wa Afrika. Aidha, Tanzania ilitoa wito wa kuweka kipaumbele katika matumizi endelevu kama moja ya mkakati wa kupunguza utegemezi kwa wahisani na kuhakikisha kuwa ajira, upanuzi wa taasisi na utekelezaji wa programu vinaendana na uwezo wa kifedha wa Umoja wa Afrika pamoja na vipaumbele vya kimkakati na mchakato wa mageuzi ya kitaasisi unaoendelea.
Kuhusu Ripoti ya Ukaguzi, Tanzania iliunga mkono hatua zinazochukuliwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika za kuimarisha mifumo ya ukaguzi wa ndani. Aidha, ilisisitiza umuhimu wa kutekeleza kikamilifu mapendekezo ya ukaguzi, kuimarisha mifumo ya fedha, manunuzi na utoaji wa taarifa, pamoja na kuhakikisha kuwa ukiukwaji wa kanuni na taratibu za Umoja Afrika unashughulikiwa kwa wakati kupitia hatua stahiki za uwajibikaji. Tanzania ilieleza kuwa hatua hizo ni muhimu katika kulinda uadilifu, uwazi na ufanisi wa taasisi za Umoja wa Afrika.
Katika eneo la mageuzi ya kitaasisi, Tanzania ilisisitiza umuhimu wa kuendelea kutekeleza mageuzi yanayolenga kuongeza ufanisi wa taasisi za Umoja wa Afrika, kuondoa muingiliano wa majukumu na kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali zilizopo. Vilevile, ilieleza kuwa mapendekezo yote ya mageuzi yanapaswa kuambatana na tathmini ya athari zake za kifedha ili kuwezesha Nchi Wanachama kufanya maamuzi yenye tija na kuhakikisha kuwa malengo ya mageuzi yanaendana na uwezo halisi wa kifedha wa Umoja.
Aidha, Tanzania iliipongeza Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) kwa hatua kubwa ilizochukua katika kuimarisha usalama wa afya barani Afrika kupitia kuimarisha mifumo ya kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na milipuko ya magonjwa, pamoja na matumizi ya teknolojia za kidijitali katika usimamizi wa taarifa za afya. Tanzania ilitoa wito kwa Nchi Wanachama kuongeza uwekezaji wa ndani katika sekta ya afya, kuimarisha uzalishaji wa ndani wa dawa na vifaa tiba, na kujumuisha vipaumbele vya afya katika bajeti za kitaifa ili kuongeza uwezo wa bara la Afrika kujitegemea katika kukabiliana na changamoto za afya ya umma. Tanzania pia ilisisitiza kuwa itaendelea kushirikiana na kuunga mkono juhudi za Africa CDC katika kuimarisha uwezo wa Afrika wa kuzuia na kukabiliana na milipuko ya magonjwa.
Kupitia ushiriki wake katika Mkutano huo, Tanzania imeendelea kudhihirisha dhamira yake ya kujenga Umoja imara, wenye mshikamano na unaobeba kwa dhati matamanio ya wananchi wa Afrika, hususan katika kipindi hiki ambapo dunia inashuhudia mabadiliko makubwa ya siasa za kimataifa. Aidha, ushiriki huo umeimarisha nafasi ya Tanzania kama mshiriki hai katika utekelezaji wa Ajenda ya 2063 ambayo ni nguzo na mhimili muhimu wa kuongoza Bara kuelekea mustakabali wa maendeleo endelevu kufikia Afrika inayojisimamia na inayojitegemea.
Balozi Said Shaib Mussa, Naibu Katibu Mkuu, amewasili jijini Addis Ababa, nchini Ethiopia, kumwakilisha Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Mkutano wa 49 wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa Afrika (49th Executive Council) utakaofanyika Addis Ababa, Ethiopia tarehe 28 – 29 Julai, 2026.
Balozi Mussa aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa tarehe 27 Julai 2026, ambapo alipokelewa na Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia, Mhe. Balozi Melaku Bedada.
Katika kujiandaa na Mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu alikutana na Ujumbe wa Tanzania utakaoshiriki katika Mkutano huo katika Ubalozi wa Tanzania Addis Ababa.
Pamoja na mambo mengine, Mkutano wa 49 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika unatarajiwa kujadili taarifa na mapendekezo mbalimbali yaliyowasilishwa na Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu (PRC), kufanya maamuzi kuhusu masuala ya kisera, kiutawala na kifedha ya Umoja wa Afrika, pamoja na kupitia na kupitisha Bajeti ya Umoja wa Afrika kwa mwaka 2027 ili kuwezesha utekelezaji wa programu na shughuli za taasisi za Umoja huo.
Amb. Innocent Shiyo received Ms. Ndeye Rose Sarr, Chief of the UNFPA Representation Office to the AU and ECA, at the Embassy of 🇹🇿. The courtesy meeting marked Ms. Sarr’s introduction following her recent arrival in Addis Ababa and reaffirmed the commitment to cooperation.
H.E. Amb. Innocent Shiyo welcomed H.E. Amb. Ennio Maes, Amb. of the Republic of Côte d’Ivoire to Ethiopia🇪🇹, for a cordial meeting at the Embassy. The two Ambassadors exchanged views on enhancing bilateral relations and expanding cooperation b/n Tanzania🇹🇿 and Côte d’Ivoire🇨🇮.
Amb. Innocent Shiyo signed the Book of Condolences at the Embassy of the State of Qatar in 🇪🇹 following the passing of His Highness Sheikh Hamad bin Khalifa Al Thani, Father Amir of the State of Qatar. We extend our sincere condolences to the Royal Family & the people of 🇶🇦.
Today, Amb. Innocent Shiyo signed the Book of Condolences at the Embassy of Guinea in 🇪🇹 following the passing of H.E. Hadja Andrée Touré, the nation's founding First Lady.We extend our heartfelt condolences to her family and the people of 🇬🇳. May her soul rest in eternal peace.
Balozi Shiyo leo alikutana na Dkt Simone Balozi wa 🇦🇹 nchini 🇪🇹 kwa mazungumzo ya kuaga kufuatia kuhitimisha muda wa utumishi nchini 🇪🇹 na kuelekea Nairobi ambako atawakilisha Austria. Balozi Shiyo alimtakia heri na kusisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya 🇹🇿na 🇦🇹.
On the sidelines of the East African Power Pool Council of Ministers Meeting, Hon. Salome Makamba (MP), Deputy Minister for Energy, paid a courtesy call on H.E Innocent Shiyo 🇹🇿 Amb to 🇪🇹 & PR to the AU. They discussed excellent 🇹🇿-🇪🇹 bilateral relations & ongoing AU cooperation.
H.E Amb. Innocent Shiyo received H.E. Amb. Dr. Afkar Nadhim Ali Al-Farsi, who paid a courtesy call at the Embassy of the United Republic of 🇹🇿. The meeting provided an opportunity to reaffirm the longstanding diplomatic relationship b/n the Gov/t of🇹🇿 & the Sultanate of Oman 🇴🇲.