Treni mpya ya umeme inatarajiwa kuwasili nchini jumanne Machi 26 mwaka huu tayari kwa kuanza kazi mwezi Julai.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na shirika la reli nchini (TRC) #TanzaniaUpdates
Waziri wa elimu,sayansi na teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa kupitia sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 ambayo imeanza kutekelezwa January 2024, wenye taaluma ya ualimu wataanza kufanyiwa tathmini ya mitihani ili kupata ajira #TanzaniaUpdates
Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia, Prof Adolf Mkenda amesema kuwa mitaala mipya imeanza mwaka huu ikihusisha ngazi ya darasa la kwanza na la tatu, upande wa sekondari imeanzia kidato cha kwanza na kidato cha tano pamoja na vyuo vya ualimu #TanzaniaUpdates
Rais wa Senegal, MackySall amekubali kufanya mabadiliko ya tarehe ya uchaguzi mkuu kutoka Disemba 15, 2024 hadi Machi 24, 2024 kutokana na maandamano yanayotaka aheshimu muda wake wa kuondoka madarakani #TanzaniaUpdates
Kampuni ya Asas inayohusika na usambazaji wa maziwa imetunukiwa tuzo ya heshima kwa viwango na ubora kutoka Super Brand East Africa Choice. Tuzo hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam #TanzaniaUpdates
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dar es salaam (DAWASA) imetoa taarifa kwa wateja wake wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu chini kuwa kutakuwa na upungufu wa huduma za maji kuruhusu maboresho ya msingi kuanzia leo Jumanne jioni hadi Alhamis March 7, 2024
Ushirikiano wa NMB na UBX inayounganisha benki 17 kupitia mtandao wa Umoja Switch umeiwezesha benki ya NMB kuunganisha benki 17 kwenye mtandao wake wa ATM lengo likiwa kuongeza wigo wa upatikanaji wa mashine za ATM na kupunguza gharama za miamala ya ATM kwa wateja wa benki.