#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 7
Jaji anasema sisi tukizonazo kama Majaji zinaonesha colum ya kwanza tar. 10/04/2025. Na anasoma waliokuwepo siku hiyo.
Upande wa utetezi pia anawasoma waliokuwepo.
Jaji anasema au tukupe kwanza ili uendeleee. ?
LISSU anakubali.
Wameenda kuzitafuta huko ili wamleteee aweze kuendelea.
Sijui kwanini walizificha.๐
Ili tuwe fair tunaomba uzipate kwanza halafu useme unazionaje.
Lissu anasema mkinipa hizo nyaraka nitahitaji dakika 30 tu nipitie na nitakuwa na cha kusema.
Anasimama KATUGA anasema busara tumpe muda wakutosha
Leo Katuga amekuwa mtetezi wa Lissu kwa mara ya kwanza. ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Eti upande wetu tunaangalia fair hearing. Watu wanacheka. ๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Katunga anasema wao wanaiachia mahakama apate.
Jaji anasema hiyo nusu saa kwani kaomba nani? Si yeye wewe una shida gani?
Lissu ameulizwa amejibu anasema kwa kuwa leo Katuga ameamua kunipenda sana naomba nipewe lisaa limoja.
Jaji anauliza tukirudi saa 10 unahisi tunaweza kuendelea?
Lissu anasema niko tayari mimi labda nyie majaji mseme hamko tayari.
Jaji amesema tukupe lisaa limoja halafu turudi hapa.
Anamuuliza Katuga yeye anasemaje watu wanacheka sana. ๐๐๐
Katuga amesimama tunasubiri sijui atajibu nini?
Katuga amesimama haongei.
Watu humu mahakamani wanasema KATUGA piga simu uuloze kwamba LISSU aruhusiwe kukaa humu ndani ya mahakama ya lisaa limoja au akasomee lockup? ๐๐๐
Maana Mh. Lissu amesema akipewa hizo nyaraka azisomeee humu humu ndani na Mawakili wanaomsaidia research asiende kule lockup.
KATUGA amefikisha dakika kadhaa hajasema kitu.๐๐๐
Jaji anasema utapelekwa sehemu unayostahili na mawakili watakuja huko. Na saa 10:10 tutarudi hapa kwa pamoja.
Tukutane hapa saa 10 ndugu zangu.
Naomba Repost yako kwenye tweet.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 5
Mhe. Lissu anamuuliza Katuganga nani anaevunja amri ya mahakama kati ya Wakili Mkuu wa Serikali na team yake yote ambao wamewaweka wazi wote.
Kile walichoambiwa na Mahakama Kuu wasikifanye ndo wamekifanya, mwenye kosa ni nani hapo mimi au wao?
Walishawaweka hadharani wao.
Nisingejua makazi yao, makabila yao na mitaa yao. Wameleta wenyewe.
Halafu hapa wanasema wakitajwa hawatafika.๐คฃ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Majaji wanateta kidogo hapa.
Ngoja tusubiri.
Kumenuka.
Kazi ishakuwa ngumu hapa.๐
Majaji wanateta.
Kimeumana.
Jaji: anawasha kipaza sauti kinapiga kelele hakiwaki. Vurugu tupu mahakamani.
Anasema tumewasikia.
Mahakama inasema tayari kuna amri ya mahakama hii hii hiyo amri inaendelea kuwa valid kama ambavyo ilivyo.
Kwahiyo tuiheshimu tu hiyo amri maana haijatenguliwa.
Anatuomba pia tuwe watulivu hapa mahakamani.
Mhe. Lissu : Anasema sasa niendelee. Sitawasoma hao watu.
Nawaomba muangalie kwenye rekodi maelezo ya shahidi P2,3,4,5,6,7,8,9,1 na 11.
Maelezo yao yanafuatana na maelezo yote hayo yanakiuka amri ya Jaji Mtembwa kuna mahali wametoa namba za simu, mitaa kazi, familia, hadi idadi ya wake na watoto wamesema.
Amri ilisema wafiche mambo hayo.
Anasimama tena KATUGA anasema pingamizi linahusu mahakama hii haina mamlaka kusikiliza shauri hili.
Anachotuletea hapa ni kama anatoka kwenye point ya kisheria.
Naona mwenzetu anachallenge namna information inavyokuwa challenged.
Tunaweza mkamatia mbali sana tukimuacha hivi au tusimkamate kabisa.
Mahakama ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Katuga anasema tunaweza chukua siku saba au sita.
Anamkaribisha Wakili Job wa serikali anasema upande wetu turejee kwenye shauri la Mahakama ya rufaa Civil Application No 656/2021 ilisema
Pingamizi linapaswa kuwa la kisheria huyu mtu (Lissu) mkimuacha ataenda mbali sana.
Angalieni namna ya kumdhibiti, atatuacha nawaambieni waheshimiwa majaji.
Mhe Lissu : Hoja ya pingamizi lao haina msingi wowote kisheria.
Kama niliyosema jana mahakama hii haina mamlaka juu ya shauri hili on the face of records kuna irregularities.
Kwahiyo kusema kwamba hizo zinaonekana kwenye rekodi ya mahakama zisisemwe hiyo hoja haina maana yoyote.
Pia hiyo kesi waliyoitaja wangejua kesi maarufu ni Mukisa Biscuits anataja citation yote kutoka kichwani anasema hiyo kesi inasema PO ni nini?
Sasa wao wanacite kesi gani sijui hapa. Haya mambo yapo kwenye Mukisa.
Jamaa hii kichwa yake sijui ikoje. ๐คฃ๐คฃ
Ningekuwa naingiza mambo mapya lakini nazungumzia kuhusu makaratasi ambayo nimepewa jana hapa mahakamani wanayakataaje sasa?
Dr. Nshalla ameenda kuongea na Lissu kidogo wamemaliza.
Na majaji nao wanateta.
Mahakama iko kimya majaji wanateta kuna POLISI moja hapa simu yake imepiga wimbo wa BONGE LA DADA ameona sana aibu. ๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Lissu anasema sasa nimetaja sheria kuhusu namna committal proceedings inavyopaswa kufanya. Hizi rules ni zao wamezitengeneza juzi hapa wao wenyewe sio mimi.
Tusipozungumzia makosa yao ambayo hawataki nizungumzie wanataka tuzungumzie makosa ya nani? Either nazungumzia nini kama hoja yao iko sahihi maana yake yote yafutwe. Ninachosema ni kwamba toka jana nilikuwa nazungumzia nini? Basi kama ni hivyo futeni hadi niliyosema jana.
Jaji anamuuliza KATUGA kama ana rejoinder.
Katuga anasema anachokufanya yeye ni kwamba yuko aggrieved na maamuzi ya mahakama kwahiyo naomba tena Mahakama jamani Mheshimiwa imuelekeze. Tumeona hadi yamejadiliwa hadi maamuzi ya mahakama kuu. Muelekezeni kuendana na kilichopo tu tafadhali.
Naomba Wakili Mrema aongezee, anasimama na kusema tunatofautiana nae kwasababu baadhi ya mashahidi aliowasema kwamba wangekuwa ni mashahidi wake kwenye proceedings hawapo na amesema kanuni ametungiwa yeye lakini hazipo kwneye proceedings.
Huyu mtu asipodhibitiwa anaingiza mambo mengi hapa. Yanatuvuruga sisi. Hayapo kwenye makaratasi. Anachomeka sana vitu. Anasema jambo moja ukizubaa anachomeka mengine tisa. Adhibitiwe.
Part 6 itaendelea post inayofuata,
Naomba Repost yako.
@OrestJr1@Jambotv_ Nazan hapa serikali ndo iandae program za kuwafanya hawa walimu walikaa mtaani muda wawe up-to-date maana kukaa sana mtaan kunafanya kusahau mambo mengi sana!