Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke ilianzishwa mnamo mwaka 1972 kama zahanati na baadae mwaka 1980 kupandishwa hadhi kuwa kituo cha afya, kuanzia mwaka 1985 ikaanza kufanya kazi kama hospitali ya wilaya mbaka mwaka 2010 ambapo ilipandishwa hadhi na kuwa hospitali ya rufaa ya mkoa
Mheshimiwa DC Munkunda aifanya ziara yake hospitali ya rufaa mkoa wa temeke, atembelea wodi ya mama na mtoto,ashiriki katika upandaji miti kitaifa, ampongeza Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu kwa kuboresha huduma za mama na mtoto.
Serikali kupitia Wizara ya Afya kuja na mwongozo wa kuchangia gharama za matibu" asema Ummy mwalim akiwa katika wizara yake Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Temeke na mfawidhi Dr. Kimaro
Mkurugenzi Dr. Joseph Gasper Kimaro wa Hospital ya Rufaa mkoa wa Temeke awatakia wafanyakazi wote wa hospitali hio na wananchi wote kiujumla "Heri ya Christmas na mwaka mpya"🥳
Mkurugenzi wa @cdcgov Dr Rochelle P Walensky anetembelea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Temeke na kuona shughuli mbalimbali ambazo zinatolewa katika hospitali hio kwa ushirikiano wa @wizara_afyatz@cdctanzania na @mdh_tanzania katika vitengo mbalimbali kama vile CTC, TB, Methadone
Changia damu okoa maisha... njoo uungane na watanzania wenzio kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watanzania wenzetu.. jumapili 12/06/2022 saa mbili asubuhi temeke hospitali.
"Customer care" huduma kwa wateja ni kitu cha msingi sana kwenye taasisi yoyote ambayo imejikita kutoa huduma kwa jamii.. Hospitali ya mkoa wa Temeke, imeamua kuandaa mafunzo ya huduma kwa wateja kwa watumishi wake wote kutoka kila idara.... Temeke Hospitali sasa ni 🔥 🔥 🔥
Mganga mkuu hospitali ya rufaa ya mkoa wa Temeke Dr Joseph G Kimaro akiwa na viongozi wengine wa Hospitali hio kwenye kigoda cha ijumaa 27/05/2022 kusikililiza changamoto za wananchi ambao ni watumiaji wa Hospitali hio ili kutatua na kuboresha huduma.
Eng Frenk Kaduma leo tarehe 26/05/2022 akikagua miradi mbalimbali ya ujenzi ikihusisha ujenzi wa ICU ya kisasa, jengo la wagonjwa wa dharura na jengo la vipimo vya radiolojia kwa udhamini wa IMF fedha za Uviko 19
Kikao cha baraza la wafanyakazi wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Temeke kilichofanyika leo tarehe 20/05/2022 katika ukumbi wa Idd Nyundo Halmashauri Manispaa ya Temeke
Mganga mkuu wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Temeke Dr Gaspar J Kimaro amethibitisha kupokea majeruhi 25 wa mbio za mwenge waliopata ajari ya gari maeneo ya polisi chang'ombe temeke mapema leo tarehe 13 mei 2022.