Viongozi na Wanachama wa CHADEMA tunakazi ya kuhakikisha Tundu Lissu anatoka jela na amatoka haraka na salama.
Tunakazi ya kufanya kama walioifanya South Africa kwa Nelson Mandela, Václav Havel nk.
Tusilidhike Lissu kukaa ndani
Mahakama inapopoteza taswira ya kuwa taasisi huru na kuanza kuonekana kama tawi lenye mwelekeo wa kisiasa, athari zake huwa pana na za muda mrefu. Imani ya wananchi kwa mfumo wa haki hupungua, na msingi wa utawala wa sheria unadhoofika. Hivyo, uhuru na uadilifu wa mahakama ni nguzo muhimu inayopaswa kulindwa kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha haki na imani ya umma vinabaki imara.
Technology must serve people, protect rights, and create opportunities for sustainable development. The future of Africa’s digital ecosystem depends on the actions and partnerships we build today — @AD_Abinallah , CEO, TMC
#AITF2026#AfricaInnovationAndTechnologyForum#TMC
Hizo zinaweza zisiwe pesa nyingi kama unavyosema brother ila jiulize je, azimio la Bunge la Ulaya linaishia kwenye Euro milioni 156 (tsh billion 470) pekee? Maana hili jambo halijaishia hapa huu ni mwanzo tu
EU ni moja ya masoko makubwa ya bidhaa za Tanzania. Kwa mwaka mmoja tu, Tanzania huuza bidhaa za thamani ya zaidi ya TSh trilioni 2.8 katika soko la Ulaya. Pia EU imekuwa mshirika muhimu katika uwekezaji, teknolojia, elimu na miradi ya maendeleo
Kwa hiyo mjadala haupaswi kusema "tumepoteza bilioni tsh 470 tu" Mjadala unapaswa kuwa taswira ya Tanzania kimataifa inaathirikaje? Je, imani ya wawekezaji inaongezeka au inapungua? Je, mahusiano ya biashara yanabaki imara?
Kwa miaka mingi, fedha za EU zimekuwa zikisaidia miradi ya afya, elimu, kilimo, nishati, maendeleo ya vijijini, uhifadhi wa mazingira na ujenzi wa uwezo wa taasisi mbalimbali nchini. Ni fedha zilizokuwa zinasaidia kupunguza mzigo ambao serikali ingeubeba yenyewe kupitia kodi au mikopo
Madhara mengine ya haraka haraka ambayo tunayapata kama taifa baada ya azimio la bunge la ulaya
📌Kupungua kwa fedha za miradi ya maendeleo
📌Kupungua kwa imani ya wawekezaji wa kimataifa
📌Kuongezeka kwa gharama za kukopa nje
📌Shinikizo kwa fedha za kigeni (foreign exchange)
📌Kuathiri ushirikiano wa teknolojia, elimu na utafiti unaofadhiliwa na taasisi za Ulaya etc
Ni kweli Tanzania iliendelea hata baada ya Denmark, UK, Finland na EU kusitisha baadhi ya misaada mwaka 2018. Lakini pia ni kweli kuwa hakuna nchi inayonufaika kwa kupoteza washirika wa maendeleo au kuingia kwenye migogoro ya kidiplomasia isiyo ya lazima
Nchi yenye uchumi wa kati haipaswi kupimwa kwa uwezo wa kupuuza ukosoaji, kama taifa tujenge taasisi imara zenye uhuru na Haki, tuvutie wawekezaji, tulinde heshima ya taifa kimataifa na kutulinde masoko yetu kimataifa