Simanzi yatanda msibani kwa Angel
Simanzi imetanda msibani kwa Angel Wariael, ambaye mwili wake umeshafikishwa nyumbani kwao Nkoasenga, Kata ya Leguruki, Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha. Mwili wake unatarajiwa kuagwa na ndugu, jamaa na marafiki kabla ya kuzikwa.Timu ya The Chanzo itakuletea matangazo ya moja kwa moja ya safari ya mwisho ya Angel. Endelea kufuatilia kurasa zetu za mitandao ya kijaamii.
Mwili wa Angel Wariael, mwenye umri wa miaka 13, aliyefariki dunia Novemba 18, 2026, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umesafirishwa kwenda nyumbani kwao, Kijiji cha Nkoasenga, Kata ya Leguruki, Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha kwa ajili ya mazishi.
Angel alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwa risasi katika matukio ya Oktoba 29, akiwa nyumbani kwao Manzese, Dar es Salaam.
Endelea kufuatilia The Chanzo kwa taarifa zaidi kuhusu safari ya mwisho ya Angel Wariael.