MHS-Massana Hospital & @ummymwalimu
Sera ya afya (personal health information Protection policy) na (cyber crime act 2015) zinalinda faragha ya mgonjwa (patient privacy & confidentiality).
Hivyo nitalinda jina la huyu mgonjwa ambaye nataka kusimulia mkasa wake kwa ufupi sana, uliotokea jana katika hospitali ya Massana, Dar es Salaam.
Jana majira ya saa tano usiku, nilipokea simu kutoka namna nisiyoitambua, ikanijulisha kwamba @TillahBlessed amepata tatizo na yupo hospitali.
Nikawailiza wapi? Wakanijibu MHS-Massana Hospital. Lakini wakasema hajapata huduma tangu wafike hapo na wamepungikiwa kiasi cha fedha.
Mmoja wa wafanyakazi wenzake na @TillahBlessed (Times FM) pia aliniandika ujumbe kunitoa hofu kwamba ni kweli dogo amepata tatizo, yupo hospital.
Nikawauliza bei gani wanadai? Jumla ya gharama za vipimo na bed rest (kabla ya huduma ni Sh72,300). Nikasema sawa. NIKALIPA bei yote niliyopewa.
Lakini nikaona pia ni vizuri nikafika hapo, nimsalimie dogo, nimefika pale MHS-Massana Hospital majira ya saa sita kuelekea saba usiku. Yupo emergency.
Nimepiga naye story pale, nikamuuliza muuguzi kwanini hamtoi huduma kwa watu kwanza kabla ya kudai fedha? Akasema ni utaratibu wao tu wa kazi.
Ok! Nikatoka reception nimchukulie @TillahBlessed juisi au kinywaji. Nikiwa dirishani, nasikia sauti ya mwanamke, analia kwa maumivu makali sana.
Nikageuka, namuona mwanamke amebebwa kwenye wheelchair, anatolewa nje (na security guards wawili), lakini analia kwa maumivu makali sana.
Mwanamke yule ana michubuko sanq mwilini, mguu umechubuka pia na umevimba, lakini anatolewa nje. Nikauliza, vipi kwani? Mbona mnatoa nje na analia?
Wale walinzi wakanijibu, tumepewa maelekezo tumsaidie kumtoa nje kwa sababu hana fedha za matibabu. Moyo wangu ulidunda kwa hasira nyingi.
Nikawauliza, “ninyi ni mazombi? Mnaelekezwa vipi? Huyu mtu ni mgonjwa, ana majeraha, mnamtoa nje? Kwamba akafie huko? Ndivyo mlivyofundishwa?”
Nikamuuliza yule mwanamke, tatizo nini? Akasema amepata ajali, akiwa anashuka kwenye daladala, dereva akaondoa gari akiwa hajashuka vizuri.
Amefikishwa MHS-Massana Hospital, anasema hakuna hata sindano au dawa ya maumivu amepata, sasa wakaamua aondolewe hapo awekwe nje.
Nikawauliza anadaiwa kiasi gani ili apate hiyo huduma ya kwanza, wale watu wa reception na malipo wakasema ni Sh39,500. Nikawalipa hiyo pesa.
Nikawaomba wauguzi wamrudishe ndani, wamsaidie kupata tiba, nitagharamia hayo matibabu yake lakini kwanza wampe huduma ya kwanza mgonjwa.
Nikawauliza, hivi ndivyo ethics za huduma za afya zilivyo hadi katika vyuo? Wanafundishwa UTU kweli? Kwao ni pesa kwanza kabla ya UTU? Ipo hivyo?
Kwamba, hata kama ni hospitali binafsi, watu hawa, hawawezi kutoa huduma kwanza (hata kwa wagonjwa wa dharura) hadi kwanza walipwe pesa zao?
Je, @ummymwalimu sera ya afya inaelekeza kwamba watoa huduma kwa wagonjwa wasiokuwa na fedha mkononi, wanatakiwa kufukuzwa?
Waziri wa afya ndiye msimamizi na sera ya afya. Nafikiri ni wakati wa kufanya mapitio na kutathmini sera ya afya, miongozo, sheria na viwango.
Wakati naondoka, yule muhudumu anayemuhudumia @TillahBlessed alinifuata na kuwaombea msamaha wenzake. Akasema ni changamoto tu ya kazi.
Nikamtia TENI, kwa kuwa ni mjamzito, nikamueleza huo msimbazi ajitahidi kununua matunda kwa ajili ya kula vizuri, mtoto akizaliwa apewe jina langu.
Anyways, mgonjwa yule alipata huduma, na Mungu amemsaidia, na anaendelea vizuri na leo asubuhi amenicheki kwamba anaendelea vizuri. Abarikiwe.
Brigedia Mtikila, MMM.
🚨 Pep Guardiola was wearing a Richard Mille watch at the Bernabeu, worth £1.1 million. ⌚
Only 50 were made, with Guardiola and Rafael Nadal among the owners. 🇪🇸
(Source: @MailSport)
Five of Christopher Nolan’s movies are returning to Regal Cinemas for $5:
April 10/11: ‘The Dark Knight’
April 17/18: ‘Interstellar’
April 24/25: ‘Inception’
May 1/2: ‘Insomnia’
May 8/9: ‘Dunkirk’