Naibu Waziri wa Habari,sanaa,utamaduni na michezo Juliana Shonza akiambatana na mkurugenzi wa @TuliaTrust_org ambaye ndiye Naibu Spika @TuliaAckson amekabidhi zawadi kwa washindi wa michuano ya Tulia Trust Cup yaliyokuwa yakifanyika viwanja vya Mwawindi Jijini Mbeya.
Naibu Spika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust @TuliaAckson amewatembelea Wakinamama wa soko la Darajani lililopo jijini Mbeya ili kujionea maendeleo ya ukarabati wa soko unaoendelea ikiwa ni siku kadhaa tangu apokee maombi ya ukarabati huo kupitia @TuliaTrust_org
Leo ndiyo ile siku mshindi wa Tulia Trust Street Dance competition 2020 ataondoka na kitita cha shilingi laki tano ,mshindi wa pili shilingi laki tatu na mshindi wa tatu ataondoka na shilingi laki mbili ndani ya viwanja vya shule ya msingi Mwenge jijini Mbeya. #tuliatrustnajamii
Naibu Spika @TuliaAckson kupitia Taasisi ya @TuliaTrust_org amepokea msaada wa madawati 200 kutoka shirika la TAZAMA ambayo yatasambazwa katika Shule mbalimbali jijini Mbeya baada ya taasisi hiyo kuomba ushirikiano wa TAZAMA kuwasaidia Wanafunzi wanaosoma katika mazingira magumu.
Leo tumetoa mifuko 140 ya Cement katika Shule ya Halinji na Nsalaga,Mkurugenzi wa @TuliaTrust_org ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania @TuliaAckson amewataka Wananchi wajue kutofautisha misaada inayotolewa na taasisi hiyo na mambo ya siasa.
Jumamosi hii tukutane viwanja vya Shule ya msingi Mwenge iliyopo Soweto kushuhudia finali za Tulia Trust Street Dance Competition. Kama noma na iwe noma #tuliatrustnajamii
Kikundi cha kudance WANYABI toka Must wakifungua mzunguko wa kwanza kwenye nusu fainali za Tulia Trust street Dance Competition 2020 #tuliatrustnajamii
Naibu Spika Dr.Tulia Ackson ameungana na Tulia Trust Street Dance competition 2020 hatua ya nusu fainali inaendelea kwenye viwanja vya chuo cha uhasibu TIA jijini Mbeya. #tuliatruststreetdancecompetition2020#tuliatrustnajamii
@TuliaTrust_org tumetembelea shule za Msingi nne zilipo kata ya Maendeleo,Kalobe pamoja na Itende,ndani ya Jiji la Mbeya,ikiwa ni pamoja na kuwapatia msaada wa jumla ya ndoo na sabuni ikiwa ni jitihada za taasisi kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na #COVID19
@TuliaTrust_org tumetoa msaada wa shilingi laki mbili na arobaini kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa daraja la muda mfupi linalo unganisha kata mbili ambazo ni Tembelea na Mwasanga Jijini Mbeya,daraja ambalo linajengwa kwa nguvu za wananchi. #tuliatrustnajamii
Jamii inahitaji upendo na kupewa thamani ili istawi na kuwa bora,Tulia Trust Street Dance competition 2020 tunakusihi kijana,ujari na kuthamini kipaji ulicho nacho na kukipa thamani kikufanye kuwa bora na mwenye mafanikio zaidi. #tuliatruststreetdancecompetition
Hawa ni wanafunzi toka Iyunga boys wakijaribu kusherehesha kwa kuonyesha uwezo wao wa kudance. Tunawapatia max ngapi ? #tuliatruststreetdancecompetition
Kama noma na iwe noma 🕺🏼🕺🏼🕺🏼. Tukiwa tunaendelea ndani ya viwanja vya shule ya sekondari Iyunga boys iliyopi jijini Mbeya kwenye mashindano ya Tulia Trust Street Dance competition 2020 ambapo kauli mbiu inasema kama noma na iwe noma.