On 19 December 2025, His Excellency Caesar C. Waitara, Ambassador of the United Republic of Tanzania to Namibia, received a courtesy visit from His Excellency Gabriel P. Sinimbo, Ambassador of the Republic of Namibia to Tanzania, at his office in Windhoek for an introductory meeting.
His Excellency Ambassador Sinimbo is the newly appointed Ambassador to Tanzania, who presented his Letters of Credence to Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania, on 11 December 2025.
During their discussions, the two Ambassadors exchanged views on various issues aimed at strengthening and further enhancing the long-standing historical and diplomatic relations between Tanzania and Namibia.
Tarehe 9 Septemba 2025, Mheshimiwa Caesar C. Waitara, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia alitembelewa na Mheshimiwa Javier P. Gastelurrutia, Balozi wa Hispania nchini Namibia.
Katika mazungumzo yao, Mabalozi hao walijadiliana kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu utendaji wa kazi katika eneo lao la uwakilishi, ikiwa ni pamoja na namna bora ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi zao na Namibia.
Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia tarehe 2 Septemba 2025 umepata heshima ya kutembelewa na Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,Waziri wa Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Mahitaji Maalum pamoja na Mhe. Mama Anna Mkapa, Mwenza wa Rais wa Awamu ya Tatu wa Tanzania wakiwa wameambatana na maafisa mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Lengo la ujumbe huo kutembelea Ubalozi ilikuwa ni kusalimia na kupata maelezo mafupi kuhusu utendaji kazi wa Ubalozi kutoka kwa Mhe Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia.
Aidha,ujumbe huo alipata fursa ya kutembelea jengo la Ubalozi ambalo limenunuliwa na kumilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Namibia Mhe. Caesar C.Waitara, amempokea Waziri wa Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Mahitaji Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima aliyewasili nchini humo leo tarehe 1 Septemba 2025, kushiriki Mkutano wa Wajane Afrika, unaotarajiwa kifanyika kuanzia tarehe 3 - 5 Septemba 2025, jijini Windhoek.
Mhe.Dkt.Gwajima ambaye ataongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo, ameambatana na Mhe.
Mama Anna Mkapa pamoja na wa wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
USHIRIKI WA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI NAMIBIA KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA YA ONGWEDIVA, 20 – 31 AGOSTI 2025
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia umeshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Ongwediva(Ongwediva Annual Trade Fair - OATF) yaliyofanyika kuanzia tarehe 20 hadi 31 Agosti 2025, katika mkoa wa Oshana, nchini Namibia.
Maonesho haya ya kila mwaka huwakutanisha washiriki kutoka mataifa mbalimbali kwa lengo la kuonesha na kutangaza bidhaa na huduma kutoka katika nchi zao. Ubalozi wa Tanzania umekuwa mshiriki wa kudumu katika maonesho haya kama sehemu ya mkakati wa kidiplomasia wa kiuchumi kwa ajili ya kutangaza bidhaa, huduma, pamoja na fursa za uwekezaji na biashara zinazopatikana nchini Tanzania.
Maonesho haya yalifunguliwa rasmi tarehe 24 Agosti 2025 na Mheshimiwa Dkt. Netumbo Nandi Ndaitwah, Rais wa Namibia, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Viwanda, Madini na Nishati wa Namibia, pamoja na mawaziri wengine wa serikali ya Namibia, wakuu wa mikoa,wabunge, na mabalozi kutoka nchi mbalimbali.
Kwa mwaka huu, Tanzania iliwakilishwa na wajasiriamali mbalimbali waliowasilisha bidhaa mbalimbali za asili ya Kitanzania. Aidha, Watanzania waishio Namibia (Diaspora) walishiriki kikamilifu kwa kuuza bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania, hali iliyoonesha mshikamano na ushirikiano mzuri baina ya Ubalozi na Diaspora.
Ubalozi wa Tanzania uliandaa banda maalum lililotumika kutangaza bidhaa mbalimbali za Kitanzania ikiwemo mchele, maharage, kahawa, chai, korosho, mvinyo, konyagi, pamoja na viungo kutoka Zanzibar. Moja ya vivutio vya kipekee mwaka huu lilikuwa ni maandalizi ya chakula cha jadi cha wali na maharage, ambacho kilipokelewa kwa furaha kubwa na wageni waliotembelea banda hilo.
Mwitikio kutoka kwa wananchi wa Namibia ulikuwa mkubwa, ambapo wafanyabiashara na wateja binafsi walionesha nia ya dhati ya kuanzisha ushirikiano wa kibiashara na watengenezaji wa bidhaa kutoka Tanzania. Baadhi yao waliunganishwa moja kwa moja na mfanyabiashara Mtanzania anayeendesha shughuli zake mjini Windhoek, ambaye husambaza bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania.
Ubalozi unaamini kuwa ushiriki wa mwaka huu umeendelea kuimarisha jina la Tanzania katika soko la Namibia na Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa ujumla, na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza mahitaji ya bidhaa za Kitanzania. Hii ni hatua muhimu katika kuendeleza mahusiano ya kiuchumi, kibiashara na kidiplomasia kati ya Tanzania na Namibia.
Leo tarehe 6/8/2025 ujumbe wa Maafisa Waandamizi watatu kutoka Jeshi la Wanananchi wa Tanzania (JWTZ) ukiongozwa na Brig. Gen. AK Kamuhabwa, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumbu la Tanzania umetembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Windhoek, Namibia kwa lengo la kujitambulisha.
Ujumbe huo ulionana na kufanya na mazungumzo na Mhe. Caesar C. Waitara,Balozi wa Tanzania nchini Namibia na kuelezea kuwa, lengo la ziara yao nchini Namibia ni kuimarisha uhusiano wa kijeshi na diplomasia kati ya JWTZ na Jeshi la Namibia.
BALOZI WAITARA AFUNGUA MAFUNZO YA KISWAHILI, NAMBIA.
Balozi wa Tanzania nchini Namibia Mhe.Caesar C. Waitara, amefungua mafunzo maalum ya lugha ya Kiswahili kwa ngazi ya awali jijini Windhoek, Namibia.
Akifungua mafunzo hayo Julai 25, 2025 Balozi Waitara ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya ufunguzi huo, ameeleza kuwa mafunzo hayo ni matokeo ya Kongamano la Kwanza la Kiswahili liliondaliwa na Ubalozi mwezi Aprili 2025 ambalo lilifanyika katika Chuo cha Triumphant.
Mafunzo hayo yatakayofanyika kwa kipindi cha wiki 15, yatatolewa kwa njia ya mtandao kuanzi tarehe 29 Julai 2025, katika Chuo cha Triumphant kilichopo Windhoek, Namibia kwa kushirikiana na Baraza la Kiswahili la Tanzania (BAKITA).
Aidha, katika hotuba yake, Mhe. Balozi Waitara aliwapongeza wanafunzi wa chuo hicho kwa kuamua kujifunza lugha hiyo kwa sababu pamoja na masuala mengine, itawezesha kuwasiliana kirahisi na raia zaidi wa milioni 200 wa mataifa mengine ambao wanazungumza lugha hiyo umuhimu.
Hadi hivi sasa idadi ya wanafunzi ambao wameshajiandikisha kwa ajili ya mafunzo hayo ni 70 wakiwemo Balozi wa Namibia nchini Nigeria, Balozi wa Namibia nchini Jamhuri ya Watu wa Congo pamoja na Konseli Mkuu wa Namibia aliyopo Angola.
Balozi Waitara aliendelea kuwasisitia wanafunzi hao kuhusu umuhimu wa lugha hiyo kama utambulisho wa Mwafrika, kuleta umoja na kusaidia katika mawasiliano na uendeshaji wa biashara.
Vilevile, lugha hiyo itaongeza wigo wa uelewa wa wanafunzi katika masuala mbalimbali ikiwemo biashara, utamaduni, utalii na diplomasia.
Mbali na hayo Mhe. Balozi Waitara aliahidi kuwa Ubalozi wa Tanzania utaendelea kushirikiana na Triumphant College, BAKITA, na wadau wengine katika kubidhaisha lugha ya Kiswahili nchini Namibia.
Tukio hilo lilifanyika kwa njia ya Hybrid ambapo kwa upande wa Namibia lilihudhuriwa na Prof Geoffrey Kiangi,Makamu Mkuu wa Chuo cha Triumphant, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia pamoja na wanafuzi wa Kiswahili.
Kwa njia ya mtandao, tukio hilo lilihudhuriwa na Waheshimiwa Mabalozi wa Namibia wanaowakilisha Namibia nchini Nigeria pamoja na Jamhuri wa Watu wa Congo pamoja na Bi.Consolata Mushi,Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Tanzania.
Leo tarehe 16/07/2025 Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia amesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria nchini Namibia kufuatia kifo cha Mhe. Muhammadu Buhari, aliyekuwa Rais wa Nigeria.
Mhe. Balozi amejumuika na Mabalozi wa nchi nyingine wanaoziwakilisha nchi zao nchini Namibia kuomboleza msiba huo.
Leo tarehe 15/5/2025,
Mheshimiwa Ceaser Chacha Waitara, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia amemwakilisha Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso (Mb), Waziri wa Maji katika Mkutano wa 12 wa Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (Zambezi Watercourse Commission-ZAMCOM) uliofanyika tarehe 15 Mei 2025 jijini Windhoek, Namibia.
Katika mkutano huo wa ZAMCOM unaojumuisha nchi nane za Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Msumbiji, Namibia, Zambia na Zimbabwe, Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso (Mb) amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa ZAMCOM katika kipindi cha mwaka 2025/2026.
Leo tarehe 7/5/2025, Mhe. Caesar C.Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia ametembelewa katika ofisi za Ubalozi na Mhe. Sam Shafiishuna Nujoma, Gavana wa Mkoa wa Khomas, jijini Windhoek, Namibia
Lengo la kukutana lilikua ni kuangalia maeneo ambayo jiji la Windhoek linaweza kushirikiana na miji ya Dodoma na Zanzibar.
Ifahamike kuwa jiji la Windhoek ambalo lipo katika Mkoa wa Khomas ndiyo mji Mkuu wa Namibia na umepiga hatua katika maendeleo ya miundombinu na mipango miji ukilinganisha na miji mingine nchini Namibia.
Mazungumzo yao yalilenga katika kuanzisha mashirikiano ya kimiji kati ya jiji la Windhoek na miji ya Dodoma na Zanzibar.
Leo tarehe 24 Aprili 2025 Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia amekutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi za Ubalozi na baadhi ya watoa mada katika Kongamano linalohusu mchango wa Lugha ya Kiswahili katika harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika hususan Namibia. Kongamano hilo litafanyika tarehe 25 Aprili 2025 jijini Windhoek.
Watoa mada hao walifika Ubalozini ni Balozi Lt.Gen.(Rtd) Abdulahrahman Shimbo,aliyekuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Balozi wa Tanzania nchini China pamoja na Balozi Brig Gen.(Rtd) Francis Mndolwa,aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Balozi wa Tanzania nchini Burundi.
Aidha, watoa mada wengine kutoka Tanzania ambao watakuwepo katika Kongamano hilo ni Bi. Consolata Mushi,Katibu Mtendaji wa BAKITA ambaye amwakilisha Mhe. Prof. Aidan Mwaluko Kabudi (MP), Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Eliah Victor, Mkurugenzi wa Vipindi wa TBC ambaye anamuakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TBC.
Leo tarehe 24 Aprili 2025Mhe Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania chini Namibia amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Frans Kapofi (Mb), Waziri wa Ulinzi na Masuala ya Wapigania Uhuru ( Ministry of Defense and Veteran Affairs) wa Namibia katika Ofisi ya Wizara hiyo.
Lengo la mkutano huo ilikuwa ni;
Mosi,kumpa hongera Mhe. Kapofi kwa kuaminiwa na kuteuliwa tena na Mamlaka kushika nafasi hiyo.
Pili,kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Ulinzi kati ya Tanzania na Namibia ambapo pande zote mbili zilikubalina umuhimu wa kuendeleza ushirikiano huo.
Leo tarehe 22 Aprili, 2025 ujumbe wa Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ukiongozwa na Col.Hamis Almas Lussuna, pamoja na Maj.Jela Joseph Bega na Maj.Biswaro Charles Malima kwa pamoja wamepata fursa ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia na kusalimiana na Mheshimiwa Caesar Chacha Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia.
Ujumbe huo utakuwepo nchini Namibia kuanzia tarehe 20 hadi 26 Aprili 2025 kwa ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu na Chuo kikuu cha Namibia Kitivo cha Sayansi ya Kijeshi.
Ifahamike kuwa, uhusiano wa Kijeshi katika ya Namibia na Tanzania ni ya muda mrefu na yenye manufaa kwa nchi zote mbili.
STATEMENT OF CONDOLENCE
H.E. @SuluhuSamia, President of the United Republic of Tanzania, has expressed her heartfelt condolences following the passing of His Holiness Pope Francis:
“I am deeply saddened by the news of the passing of the leader of the Catholic Church worldwide, Pope Francis.
Throughout his 12 years as the leader of the global Catholic Church, Pope Francis lived his life as a teacher and leader who inspired, taught, and championed the well-being and development of people, as well as the promotion of peace.
On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt condolences to all Catholic faithful in the country and across the world.
May Almighty God rest his soul in eternal peace in heaven.
Amen.”
#RIPPopeFrancis #TanzaniaMourns #CatholicChurch #Peace #Diplomacy
Balozi wa Tanzania nchini Namibia Mhe. Caesar C. Waitara amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Biashara wa Namibia Mhe. Balozi Selma Ashipala-Musavyi (Mb) jijini Windhoek.
Balozi Waitara amempongeza Waziri huyo kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara hiyo pamoja na kumhakikishia kuendeleza na kudumisha uhusiano wa kihistoria na wa kindugu uliopo kati ya Tanzania na Namibia kwa maslahi ya pande zote mbili. @UbaloziNamibia
Leo tarehe 11/04/2025 Mhe. Caesar C. Waitara Balozi wa Tanzania nchini Namibia amekutana na Mhe. Selma Ashipala-Musavyi(Mb), Waziri wa Uhusinao wa Kimataifa na Viwanda wa Namibia.
Lengo la kukutana nae ilikua ni kumsalimia na kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Waziri wa Wizara hiyo pamoja na kumhakikishia kuendeleza na kudumisha uhusiano wa kihistoria na wakindugu uliopo kati ya Tanzania na Namibia.
Leo tarehe 10/04/2025 Mhe. Caesar C. Waitara, Balozi wa Tanzania nchini Namibia ametembelewa na waliokuwa wapigania Uhuru wa Namibia.
Ujumbe huo umeongozwa na Ndugu Eddy Hamada, ambaye ni mpigania Uhuru mstaafu na aliambatana na Bw. John Kayo.
Lengo la ugeni huo lilikuwa ni kujadili Mchango wa Tanzania uliotoa kwa Serikali ya Namibia wakati wa harakati za kupigania uhuru.
Ifahamike kuwa, Tanzania ilitoa mafunzo ya kijeshi kwa jeshi la Namibia pamoja na mafunzo mengineyo kama vile utabibu, ualimu na Lugha ya Kiswahili.