Pitch iko mbali sana aiseee πββοΈπββοΈ
Kwani lini Tz mashindano ya Riadha yashawahi fanyika humu ndani?
I mean Riadha kweli watu wanaanzia uwanjani!
Maana sio kwa Running Lane hii
Hii mbegu itupiwe jicho la kipekee na wakulima wa mpunga inapacha sana inazaa sana, mbegu ni RIC3(TXD 307).
Mashamba haya hayatumii mbolea kabisa, na wastani wa mavuno gunia 20-30 kwa ekari.
Hili shamba liko kilosa, Kijiji cha Ngaite.
Huu mwaka jipe assignment achana na masuala ya mademu demu, achana na masuala sijui ya nyeto nyeto, punguza kucheza ma game game na mitungi punguza kunywa mkali afu acha kuhonga honga.
Walahi nakuhakikishia mwaka 2027 unapopinduka hutakosa hata milioni mbili ya akibaπ Naapia π€
Ukihisi umekata tamaa tafuta nyimbo ya Paul Clement - Mwokozi.
Kuna verse kaimba hivi
"Najua una nguvu waweza nibeba,Mwanadamu atachoka ataniangusha"
"Mwanadamu hugeuka wakati wowote,Ila kwako uhakika huwezi nitupa"
Powerfull Messageπ
Enzi zile krismass ilikuwa big deal sana, Linapikwa pilau jingi sana na viungo vyeusi tii kama mkaa soda ni za watu wazima, watoto wanatengenezewa chemi cola kipakiti kimoja maji ndoo kubwa,πhapo mtoto hatumwi dukani pilau linapikwa musoma harufu mpaka tarime.
Kijana mwenzangu kuna siku UTAFANIKIWA mbele ya macho ya watu wote ambao walikukatia tamaa, hawakukuamini, waliokunyima nafasi na fursa, waliosema hauwezi na wale wote waliosema haustahili. Endelea kupambana na kumtegemea MUNGU, ushindi wako mkubwa unakuja.
Kwa wale mnaopenda kusali Zaburi. Unaweza kuanza na Zaburi 51 ya toba, kisha Zaburi 35 ya kuomba kupiganiwa halafu Zaburi 91 ya ulinzi na baraka, malizia na 23 ya wingi na baraka. ππ»