Mwambieni HILIDA NEWTON anitoe kabatini sidhani kama nimewahi zinguana nae yule dada 💔
Nina upendo mkubwa sana na waty wanao pambania harakati za nchi hii kwahyo nampenda sana Newton mfikishieni huu ujumbe.
Ahsante
‼️ALERT‼️
Usiku huu kikosi cha wauaji wa KMKM kutoka Zanzibar tayari wameingia Dar na kesho wamepanga kuwavalisha sare za Polisi.
Maandamano ya 7/7 yamempanikisha Nduli Idd Amin mama na genge lake ndo maana wanahangaika sana.
Sisi tumesema Maandamano yetu ni ya amani, vurugu labda walete wao.
#77Tunatoka #7UP #FreeTanganyika #FreeTanzania
Bango langu linasomeka,
“Haki zetu si zawadi za serikali ni msingi wa utu wetu. Tunaheshimu amani, lakini hatutakubali haki zetu zitupwe pembeni”
Maandamano yangu yataanza muda si mrefu 🔥🔥🔥🔥🔥
Mpaka sasa Genz wamefanikiwa kwa asilimia 80% Nadhani tunaweza kufanikiwa zaidi tukisha ingia barabarani,
Soon hata hii mitandao itazimwa, tusilale kulala tuwaachie mafisadi wano lalia noti zetu, twendeni barabarani hatuna kitu cha kuogopa✊🏽
Siku ambayo wafanyabiashara walitakiwa kutangaza biashara zao kitaifa na kimataifa
Ipo kimyaaaaa!
Ahsanteni sana Genz kwa huu ushindi na baada ya hapa tunakutana 8/8 hakuna kupoa, si wanasema walichaguliwa na wananchi?
JESHI LA POLISI @tanpol hawa vijana ni magaidi baadae leo mnawachekea kwasababu wapo sisiyemu lakini kuna siku watafanya uhalifu bila kujali itikadi,
Na pengine hawa ndio wanaendelea kufanya uhalifu baadae mtaanza kusema al-shabab wametokea wapi kumbe nyie ndo mlikuwa mnawalea chukueni tahadhari mapema,
Tukutane 7/7 kukomboa nchi ✊🏽
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 229
Anasimama Mhe. Lissu.
Anasema baada ya kusikiliza hoja za Wakili wa mleta maombi naomba nianze kwa kunukuu maneno ambayo Mahakama hii iliyasema kwenye kesi ya Commissioner General of TRA Criminal case namba 62/2022 pale ambapo maombi ya mdaawa yamezuiliwa na sheria, hawezi kufanya drafting ya kuhadaa Mahakama.
Wanasema uamuzi ulifanyika bila wao kusikilizwa, mgogoro ulianza 19 February 2026 ukurasa 391 wa record, Ugomvi ambao umetuleta hapa ulianza siku Tano kabla ya maamuzi ya Mahakama.
Wakili wa Serikali mkuu Renatus Mkude alisema "waheshimiwa Majaji tuko tayari kuendelea na mashahidi 3 lakini kabla ya kuendelea tuna notice of additional substance of evidence, ambayo imejazwa electronically siku ya Jana"
Katika ukurasa wa 392 Mahakama ikaamua kuwa tuendelee na mashaidi kwanza baadae tutarudi kwenye hoja za notice.
February 20, 2026 ukiangalia ukurasa wa 405-419 utayaona maneno niliyoyasema.
Mahakama ikaamua tumesikiliza sehemu zote kesi hii anahairishwa hadi jumatatu ilikuwa 23 February 2026 kuanzia ukurasa 420 unaonesha hayo.
Mkude akasema wako tayari kuendelea na Katuga akafanya submission in chief pg 421, 423 Katuga akajibu PO, nikafanya rijoinder, pg 428 kuna ruling of the court.
Baada ya submission ya Renatus, submission in chief ya Katuga, rejoinder yangu na reexamination in chief ndipo Mahakama ilitoa uamuzi.
Kwa record hiyo yote nguvu ya kusema hawakusikilizwa wanaitoa wapi?
Kwasababu ya maombi haya leo ni siku ya 139 kesi haiendelei kwa sababu ya uongo wao kwamba hawakusikilizwa.
Haki ya kusikilizwa ni haki ya kikatiba ni kweli sasa kwa ushaidi huu wanawezaje wakasema hawakusikilizwa?
Mmemsikia Wakili Katuga akisema Mahakama ilikosea ilipaswa iangalie reasonablity ya hiyo notice, ipokee ushaidi, iangalie competence kisha iamue.
This is an appeal under 6.3 wanayoitaja, it's only clever drafting inayolenga kuiadaa Mahakama.
Iangalie TRA vs New Musoma textile industry kwenye orodha yangu ni kesi namba 7 hawaruhusiwi kuleta malalamiko kuhusiana na hiyo notice kwenye Mahakama hii. Kifungu 6.3 cha AJA mamlaka ya Mahakama hii siyo hiyo wanayoiomba wao.
Ukurasa wa 21 unaonesha mjadala mpana wa ninachokisema sasa na inamaliza huu mjadala, hamuwezi kuanza kuangalia hiki kilicholetwa ni kitu gani mnapaswa kutazama je huu uamuzi ni legal.
Wanasema hawakusikilizwa mnaangalia kwenye record, Je ni kweli hawa watu hawakusikilizwa, hamuendi kwenye huu usikilizwaji ulikuwaje, Mahakama hii haiangalii mambo superficial.
Waheshimiwa Majaji mleta maombi alisikilizwa hivyo ruling ya mahakama ni legal, imeandikwa na Majaji wenye mamlaka baada ya kusikiliza pande zote hata kama hauwafurahishi wanapaswa kukubaliana nao.
Waheshimiwa Majaji waleta maombi hawana hoja yeyote ya maana on the basis of this record. Section 308 ya CPA imetajwa kwa lengo la kuwaalika mtengue kilichoamuliwa na Mahakama kuu nawaombeni msiende huko.
Nitasema kwa kifupi sana juu ya section 308 ya CPA na nini Mahakama ilisema inakataa kuongezwa kwa ushahidi mpya inadeal na Shaidi mpya tu.
Inazungumzia ni katika mazingira gani shaidi ambaye hakutajwa kwenye commital proceedings anaweza kuongeza kwenye trial, mleta maombi hapa analeta ushahidi mpya wa shaidi ambaye ametajwa kwenye commital na siyo shaidi mpya kama Sheria inavyotaka.
Anaendelea Mhe. Lissu
Kwenye uamuzi huu hakuna sehemu ambayo Mahakama imesema ushaidi huo haufai bali imesema ni ushahidi mpya na haufai kisheria.
Hii clever drafting in order to avoid the legal power, kama wanataka kupinga uamuzi huo wasubiri kesi iishe kisha wakapinge uamuzi huo.
Part 230 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Imetoka kwa reporter wetu @HildaNewton21
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 230
Anaendelea Mhe. Lissu.
Waheshimiwa Majaji naomba nimalizie kwa kusema yafuatayo, maombi haya yameletwa kwa lengo moja tu kurefusha mashauri na kuchelewesha kesi ya msingi ili mjibu maombi aendelee kukaa Ukonga gerezani.
Leo ni siku ya 139 kesi haifanyiki na mimi nakaa Gerezani I'm completely innocent but I'm in prison kwa mwaka mmoja na miezi mitatu.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania article 59.b.4 inazungumzia mamlaka ya DPP kutokuchekewesha muenendo wa Mahakama.
Kuzuia Mahakama kuu kuendelea na kesi kwa siku 139 kwa kuleta maombi ambayo wanayajua hayana msingi wowote, kama hii ni kutenda haki then inabidi tutafute tafsiri nyingine ya neno kutenda haki.
Mamlaka ya DPP ni kuwezesha uamuzi wa haki, wa haraka na usiokuwa wa gharama kubwa.
Niko Mahabusu muda wote huo je hiyo ni haki? DPP na Mawakili wake wamepuuza mamlaka ya kikatiba ya DPP kwa maneno yao wenyewe walishabakiza shahidi mmoja lakini haijaendelea kwa siku 139 kwa sababu ya maombi haya.
Mhe. Lissu anasema ombi langu siyo tu Mahakama hii iyakatae maombi hayo siyo tu hilo, maombi yangu Mahakama ya rufani ina mamlaka ya kutoa amri ambazo zingetolewa na Mahakama kuu.
Kwa kutumia kifungu cha 367 cha kutaka mleta maombi anilipe fidia kwa kunifanye nikae gerezani kwa siku 139 bila kesi kuendelea kwa sababu ya maombi yake.
Yakataeni haya maombi na muamuru DPP anlilipe fidia kwa usumbufu wote alionifanyia.
Mhe. Lissu anasema ni hayo tu Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya rufani.
Anasimama Wakili wa Serikali Katuga.
Anasema tumeleta maombi yetu na tumeiomba Mahakama hii tukufu kwamba tumenyimwa haki ya kusikilizwa kwenye huo ushaidi tunaoomba uongezwe, ulikataliwa kabla ya kufika katika hiyo mahakama.
Mjibu maombi ameialika Mahakama hii kwenye proceedings kuanzia pg 391 akizungumzia submission ya uhalali wa notice yetu, tulipata nafasi ya kusikilizwa kuhusiana na notice yetu siyo nafasi ya kusikilizwa kuhusiana na huo ushahidi.
Hatueleweki harafu tunaambiwa tumefanya clever drafting, ushahidi umekataliwa kabla ya kuingizwa, tulisikilizwa kwenye notice tu.
Mjibu maombi anaposema tulipewa haki ya kusikilizwa hakutuelewa kwenye angle gani. Kuirejesha Mahakama hii katika kifungu cha 308 anasema ni kuomba rufaa kwa Mahakama hii sisi tulikuwa tunaonesha walichokifanya na kilichotakiwa kufanyika.
Katunga anaendelea kusema
Sisi hatujaleta maombi haya kuchelewesha kesi tumekuja hapa kuiomba Mahakama iwese kutafsiri Sheria. Kifungu cha 367 kinatumika pale Mahakama inapokuwa imesikiliza kesi na kuona kwamba kesi ni ya kutengenezwa.
Kwa mujibu wa Sheria tunasema maombi yetu ni ya muhimu tunaomba yakubaliwe na yatazamwe na kuita hizo proceedings kuangalia kile ambacho tunakilalamikia.
Jaji anasema basi baada ya kusikiliza pingamizi la awali pamoja na maombi haya tutakwenda kuamua kwanza kuhusu pingamizi la awali kama tutakuwa tumekubali basi itaishia hapo kama pingamizi litakataliwa basi tutaendelea.
Tutawajulisha tarehe ya uamuzi.
Inapigwa Court ya kinyonge ni kama jamaa mchana umepita kama upepo.
Nawatakia Ijumaa njema.
Julai 7, 2026 tukutune barabarani, usihau kubena bango lako lenye ujumbe wa madai yetu ya msingi.
Naomba Repost yako.
Imetoka kwa reporter wetu @HildaNewton21