#UMOJATVupdates: Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) Taifa, (MNEC) Ndugu @NdeleMwaselela akinunua samaki kwa wajasiriamali wa Soko la Makongolosi wilayani Chunya alipokwenda kukagua utekelezaji wa maagizo yake.
MNEC anayewakilisha Mkoa wa Mbeya Ndugu @NdeleMwaselela akimkabidhi Diwani wa Kata ya Matundasi Wilayani Chunya mkoani Mbeya, Kimo Choga fedha kwaajiri ya ununuzi wa matofali 1000 ya kujengea Darasa 1 kwenye shule mpya ya sekondari ya Masache inayojengwa katika Kijiji cha Itumbi.
#UMOJATVupdates: (MNEC) Ndugu @NdeleMwaselela Aipongeza Wilaya ya chunya Kwa utekelezaji wa Maagizo ya Mh Rais Dkt @SuluhuSamia akisema wametekeleza Kwa vitendo, MNEC yupo Ziarani kikazi kwaajiri ya kukijenga Chama na kufuatilia utekelezaji wa Maagizo ya Mh Rais Wilayani Chunya.
#UMOJATVupdates: (MNEC) @NdeleMwaselela Amekutana Na kuzungumza na makundi mbali mbali ya Wanachama wa CCM wilayani Chunya ambapo pamoja na mambo Mengine anatarajia Kusikiliza na Kutatua Kero zao kupitia Ziara yake Maalum inayoendelea Wilayani Humo Iliyoanza Jana Sept 2.2024.
#UMOJATVupdates: (MNEC) @NdeleMwaselela Akizungumza na wanachama wa Chama Cha CCM pamoja na wakazi wa wilaya ya chunya Katika mkutano wa Hadhara wakati akiendelea na Ziara Maalum ya kukijenga Chama Cha mapinduzi (CCM) wilayani Humo Iliyoanza Jana Tarehe 2 Sept 2024.
#UMOJATVupdates: Mjumbe Wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Kutoka Mkoa wa Mbeya, (MNEC) @NdeleMwaselela Akisaini Kitabu Cha wageni mara Baada ya kuwasili Katika Ofisi za CCM wilayani Chunya Kwaajiri ya Ziara ya kukijenga Chama Inayorindima Kwa Siku Tatu za kishindo wilayani humo.
#UMOJATVupdates: MNEC @NdeleMwaselela Amegawa majiko ya gesi Kwa mama lishe wa Mbeya mjini wakati wa kilele Cha Tamasha la TULIA Cooking Festival 2024 Jijini Mbeya, Katika Hatua yakukabiliana na Uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya Mkaa na Kuni Kwa kiasi kikubwa.
#UMOJATVupdates: (MNEC) Ndugu @NdeleMwaselela Akifurahi jambo Na Naibu waziri wa Nishati Mh Judith Kapinga Pamoja na Spika wa Bunge La Tanzania na (Mb) wa Mbeya Dkt @TuliaAckson Katika Tamasha la TULIA Cooking Festival lililofanyika Katika uwanja wa Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya.
#UMOJATVupdates: (MNEC) ndugu @NdeleMwaselela Akiwa ameongozana na Waziri wa Nishati Mh Judith Kapinga ambaye alialikwa kama mgeni rasmi Katika Kilele Cha Tamasha la TULIA Cooking Festival 2024 Pamoja na Mama Sophia Mwakagenda Mbunge wa Viti Maalum-(CHADEMA) Mkoani Mbeya.
#UMOJATVupdates: Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Ndugu @NdeleMwaselela amempongeza Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt @TuliaAckson kwa kuwapatia Mitungi ya gesi Mama Ntilie 1,000 katika Jimbo hilo pamoja na mavazi rasmi yakuvaa wakati wa na kuhudumia wateja wao.
(MNEC) Ndugu, @NdeleMwaselela ameongoza kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mbeya na Viongozi wa CCM wilaya zote kupokea Mwenge wa Uhuru unaoanza mbio zake mkoa wa mbeya katika wilaya zote mwenge wa uhuru umepokelewa Kambi katoto wilayani chunya Kutoka Mkoa wa Tabora Tarehe 24.08.2024.
#UMOJATVtz: Kheri ya Siku ya Jumapili Njema ya Leo, Tarehe 25.08.2024 Kwenu nyote Wanafunzi, Walimu, wazazi na walezi wa watoto wetu wa Shule ya Paradise Missions Pre & primary school Kutoka Kwa Mkurugenzi wa Shule yetu, (MNEC) Ndugu @NdeleMwaselela.
#UMOJATVupdates: Mjumbe Wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Kutoka Mkoa wa Mbeya (MNEC) Ndugu @NdeleMwaselela ameungana na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya kuupokea Mwenge wa Uhuru kijiji cha Kambikatoto, wilaya ya Chunya kutoka Mkoani Tabora 23.08.2024.
#DKTSAMIAmbeyaDCmshikamanoCUP2024
Rasmi Kivumbi Ni Kesho 09.8.2024 Kuanzia Saa Nane Mchana, Uwanja wa 44KJ(jeshini).
Mashindano Haya Yamedhaminiwa na (MNEC) @NdeleMwaselela Pamoja na Uongozi Mzima wa Shule ya Paradise Missions Pre & Primary School Iliyopo Mbalizi Jijini Mbeya.
#UMOJATVupdates: Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Ndugu Patrick Mwalunenge, Mjumbe Wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Kutoka Mkoa wa Mbeya, (MNEC) @NdeleMwaselela Wakipeana mkono na Waziri wa TAMISEMI Mh Mohamed Mchengerwa Leo Mara Baada ya Kutembelea Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.
#UMOJATVupdates: Mh Waziri Mchengerwa Amefika Mkoani Mbeya Kushuhudia Utiaji Saini wa mikataba ya Ujenzi wa Soko jipya la Sokomatola, Barabara za Mitaa Pamoja na Ujenzi wa Stendi ya Kisasa ya Mabasi ya Mkoa Katika uwanja wa ndege wa zamani (OldAirport) Kupitia Mradi wa TACTIC.
#UMOTVupdates: Mjumbe Wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, (MNEC) @NdeleMwaselela Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Viongozi mbali mbali wa CCM Mkoa wa Mbeya na Waziri wa TAMISEMI Mh Mohamed Mchengerwa pindi alipofika Mkoani Hapa na Kutembelea Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya July 27,2024.
#UMOJATVtz: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh @SuluhuSamia na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mh Umaro Sissoco EmbalΓ³, wakati wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Muongozo wa Ushirikiano baina ya Nchi mbili, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.
#UMOJATVtz: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco EmbalΓ³ Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024.