#SupaBreakFast ya kesho tarehe 14 Mei, 2026 asubuhi kuanzia saa 1:00 asubuhi Kiongozi wa Chama Ndugu, @SemuDorothy atakuwa mgeni kwenye kipindi hicho.
Usipange kukosa!
OUT OF TIME, OUT OF TOUCH, OUT OF IDEAS! Ndipo ma-CCM walipofikia. Mnawezaje kubeba agenda ya kuwashambulia na kuwatukana vijana wa #GenZ kwamba hawana adabu, wamepotoka na hawana uzalendo? Mnajua kuwa #GenZ ni asilimia 30 ya Watanzania wote? Mmeshapitwa na wakati. Mtaondoka tu!
"Ripoti inawalinda wahusika wa mauaji kwa kukwepa uwajibikaji na inavisafisha vyombo vya ulinzi na usalama vilivyohusika badala ya kuviwajibisha. Hata ukitumia takwimu za Tume yenyewe kuwa watu Zaidi ya 518 wameuawa (takwimu ambazo hata hivyo zinatia shaka kubwa usahihi wake), haiingii akilini kwa nini Tume imeshindwa kutumia takwimu hizo kutoa wito wa vyombo vya ulinzi na usalama kuwajibika." - @ACTwazalendo
"Ripoti ya Tume ya Chande ilikusudiwa kufunga ukurasa wa maumivu. Badala yake,
imefichua mgogoro mkubwa zaidi wa kitaifa. Tanzania sasa inakabiliwa na chaguo moja
kati ya mawili;-
➢ Njia ya ukweli, uwajibikaji na haki; au
➢ Njia ya kutokuwajibika, ukandamizaji na utawala wa nguvu.
ACT Wazalendo inasimama imara upande wa ukweli, haki, utawala wa katiba na
ushindani wa kisiasa wa amani. Maisha ya Watanzania 518 waliopotea, wale 245 ambao
hawajulikani walipo (na inawezekana idadi ni kubwa zaidi), pamoja na mustakabali wa
taifa letu, vinadai hatua madhubuti zaidi kuchukuliwa. Hili linahitaji kufumuliwa kwa
mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi yetu ikiwemo mwelekeo mpya wa kikatiba
(constitutional order), weledi wa vyombo vya dola na utumishi wa umma kwa ujumla
wake." - @ACTwazalendo
#TANZANIA: LISSU SI MHAINI LAKINI ANAMAKOSA YA KUPIGANIA RASILIMALI ZA NCHI HII, KUPINGA UTEKAJI - ADO
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu leo Mei 05, 2026 akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kilwa Kusini katika maadhimisho Siku ya ACT Wazalendo amesema Tundu Lissu si mhaini lakini amesema kuwa ana makosa ya kupinga utekaji, kupigania rasilimali za nchi ya Tanzania, kupigania Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi.
"Tundu Lissu si mhaini lakini ana makosa matatu. Kosa la kwanza kupigania rasimali za nchi hii, kosa la pili kupinga utekaji na kosa la tatu kupigania Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi."
"Nilisema Dodoma kwa yeyote anayedhani kuwa anaweza kuwazima Watanzania kwa risasi na kuwateka nyara; anapoteza muda wake. Watawala wanataka tukae kimya; nasi tuko tayari kwa lolote lile ili Tanzania ikombolewe!" - Ado Shaibu, Mbunge na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo
@ACTwazalendo Tunatoa wito wa kujiuzulu na kuwajibishwa
wafuatao;
1. Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa,
2. Mkuu wa Jeshi la Polisi,
3. Msajili wa Vyama vya Siasa,
4. Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.
5. Wakuu wa Mikoa iliyohusika na mauaji ya wananchi wawajibishwe;
6. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam - Albert Chalamila
7. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya - Beno Malisa
8. Mkuu wa Mkoa wa Songwe - Jabiri Omar Makame
9. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza - Said Mtanda
10. Mkuu wa Mkoa wa Geita - Martine Shigella
11. Mkuu wa Mkoa wa Arusha - Amos Makalla
12. Mkuu wa Mkoa wa Iringa - Kheri James
13. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma - Rosemary Senyamule
14. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga - Mboni Mhita
15. Mkuu wa Mkoa wa Mara - Kanali, Evance Alfred
➢ Wakuu wa Wilaya za Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo, Mbeya, Mbeya
Vijijini, Kyela, Mbozi, Momba, Nyamagana, Ilemela, Geita, Arumeru,
Arusha, Iringa, Dodoma, Kahama, Musoma, Tarime, Bunda, na Songea
ambazo zilishamiri kwa matukio ya mauaji wawajibishwe
Msimamo rasmi wa @ACTwazalendo kuhusu Ripoti ya Jaji Chande kuhusu mauaji ya Oktoba 2025. Ni MAJONZI makubwa kwa Taifa na lazima hatua za uwajibikaji zichukuliwe haraka