…uliyofanyika kwa njia ya Mtandao, leo tarehe 29 Juni 2026, Makamu wa Rais akiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa.
Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa
(SADC Organ Troika) kuhusu hali ya usalama nchini Madagascar na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akitoa salamu za rambirambi mara baada ya Ibada ya kumuombea marehemu Bi. Suzana Ngolo Magufuli ambaye ni Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, iliyofanyika Viwanja vya Kilimani Wilayani Chato.
Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Bi. Suzana Ngolo Magufuli ambaye ni Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, mara baada ya Ibada iliyofanyika Kilimani Wilayani Chato leo tar 29 Mei 2026.
Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Viongozi pamoja na familia, wakishuhudia mwili wa marehemu Bi. Suzana Ngolo Magufuli ambaye ni Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, ukishushwa kaburini wakati wa mazishi yaliyofanyika Kilimani.
Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili katika Viwanja vya Kilimani Wilayani Chato, ambapo anaungana na waombolezaji mbalimbali kushiriki Ibada ya kumuaga Bi. Suzana Magufuli ambaye ni Mama wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Waandishi wa Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) unaofanyika katika Ukumbi wa Ngurdoto Mkoani Arusha.
Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akipokea tuzo iliyotolewa na Chama cha Waandishi wa Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Chama hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika Ukumbi wa Ngurdoto Mkoani Arusha kufungua Mkutano Mkuu wa 13 wa Kitaaluma wa Waandishi Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA).
Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo tarehe 20 Mei 2026 amewasili mkoani Arusha kwa shughuli za Kikazi. Mhe. Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Waandishi Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA) utakaofanyika kesho tarehe 21 Mei 2026.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemtembelea na kumjulia hali, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Samwel Malecela katika makazi yake Kilimani Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma kushiriki Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa Pili wa Anglikana Dayosisi ya Ruvuma na Marehemu Askofu Stanford Shauri, Ibada inayofanyika Liuli Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma
Muungano wetu ni wa kipekee na wa kihistoria ambapo unachagizwa na matukio ya furaha na umoja ikiwemo michezo.
Miaka 62 ya Muungano wetu ni ushuhuda wa amani, umoja na mshikamano wa kweli.
*Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi*
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ninaungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuipongeza Klabu ya Simba kwa ushindi na kutwaa Ubingwa wa Kombe la Muungano 2026.
Hongera kwa wachezaji, benchi la ufundi na kwa timu zote zilizoshiriki mashindano haya.
Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasili katika Ukumbi wa Mabele mkoani Dodoma, ambapo ni mgeni rasmi katika kilele cha Tuzo kwa wanawake waliofanya vizuri katika sekta mbalimbali maarufu Malkia wa Nguvu kanda ya kati, zinazoandaliwa na Clouds Media Group.