Mpango wa kuuliwa kwa watoto kipindi Cha Yesu Ni sababu Shetani alijua aliyezaliwa Ni Nani,vivyo hivyo kipindi Cha Musa. Sio wote Ila kuna watu tuliyopitia tunayopitia na tutakayopitia Ni sababu shetani ANAJUA sisi TUTAKUA Nani, haina maana haitatokea Ila haijawahi kuwa rahisi.
BWANA AKUWEKE KWENYE NAFASI YAKO LEO NA KUKUPONYA NA MAGONJWA YOTE.
Zaburi 18:19
Akanitoa akanipeleka panapo nafasi,
Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote;...
1 Kor 13:4-7 SUV
1 Petro 2:12
Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.