#WASHINGTON:BUNGE LA MAREKANI LAIDHINISHA MUSWADA WA KUTATHIMINI UPYA UHUSIANO NA TANZANIA NA MAREKANI
Kamati ya Mahusiano ya Kigeni yabunge la Marekani imeidhinisha miswada mitano ya sera za mambo ya nje, ikiwemo muswada unaotaka kufanyika kwa tathmini ya kina ya uhusiano kati ya Marekani na Tanzania kufuatia kile wabunge wa Marekani wanachokitaja kuwa kuongezeka kwa vurugu za kisiasa na kudorora kwa demokrasia nchini humo.
Mjumbe Mkuu wa Upinzani katika kamati hiyo, Seneta Jeanne Shaheen wa chama cha Democratic, amesema uungwaji mkono wa pande mbili za kisiasa kwa miswada hiyo unaonesha dhamira ya kuimarisha usalama wa taifa la Marekani na kuendeleza ushawishi wake duniani.
Muswada unaohusu Tanzania, uliowasilishwa kwa ushirikiano na Seneta Ted Cruz wa chama cha Republican, unaitaka serikali ya Marekani kufanya tathmini ya kina ya mahusiano ya nchi hizo mbili.
Aidha, utaitaka Washington kuchunguza kwa karibu uhusiano unaozidi kuimarika kati ya Tanzania na mataifa ya China na Urusi, pamoja na athari zake kwa maslahi ya Marekani katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Mbali na Tanzania, kamati hiyo pia imeidhinisha muswada wa kusaidia nchi washirika kupata teknolojia za kidijitali za Marekani kwa lengo la kupunguza utegemezi wa teknolojia za China.
Wabunge hao pia wamepitisha sheria inayolenga kuongeza uwazi katika matumizi ya fedha za walipa kodi wa Marekani zinazotumika kufadhili misaada ya kigeni, hasa bidhaa za chakula na vifaa vya uzazi wa mpango vinavyotolewa kwa nchi mbalimbali.
TYK
Kwa nini Mungu anatuonya tusiyapende ya dunia? Aiumbe dunia yy, atuweke humo halafu anasema tusi-enjoy 😂 jitahidi usome hadi kwenye HITIMISHO.
1 Yohana 2:15
Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
Si kwa sababu anataka tuwe na maisha ya kukosa raha. Ni kwa sababu anajua moyo wa binadamu:
Kitu chochote unacho “kishikilia sana” kitakuwa mungu wako. Na Mungu anataka awe yeye wa kwanza, kwa sababu ndiye anayeweza kukutosheleza kweli. Vitu vya dunia havitosheki
kamwe.
"Ya ulimwengu” hupofusha. Unapokwama sana kwenye mali, sifa, starehe, huwezi tena kuona Mungu wala kuhurumia watu. Ndio maana Yesu alisema ni vigumu tajiri kuingia Ufalme wa Mungu - si kwa sababu pesa ni mbaya, bali kwa sababu pesa inamfunga moyo.
“Ya ulimwengu” ni yepi haswa?
Bibilia inafanua wazi katika 1 Yohana 2:16:
“Mambo yote yaliyomo ulimwenguni, yaani: tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, hayatokani na Baba, bali yanatokana na ulimwengu.”
Tafsiri yake ya haraka:
Tamaa ya mwili: Starehe unazotafuta kwa njia mbaya. Sio kula ni sawa, bali kula kupita kiasi hadi uumize mwili wako. Sio mapenzi ni mabaya, bali kutumia mwili wa mtu kama kitu tu.
Tamaa ya macho: Choyo, wivu, kuhitaji kila kitu unachoona kwa mtu mwingine. Kujenga furaha yako kwa kumiliki zaidi na zaidi.
Kiburi cha uzima: Kujivuna, kujiona bora kuliko wengine, kutafuta sifa za watu zaidi ya sifa za Mungu.
Je, ni “starehe zako zinazoumiza watu wengine”?
Ndiyo, mara nyingi ndivyo ilivyo. Lakini si kila starehe. Tofauti iko hapa:
Sio mbaya kufurahi, kucheka, kula chakula kizuri, kupenda vitu vizuri. Tatizo linatokea pale starehe hiyo inakuwa:
Njia ya kujaza pengo la ndani ambalo ni Mungu tu anayeweza kujaza.
Inakuumiza wewe au inawaumiza watu wengine - kwa mfano: ulevi, udanganyifu kwa ajili ya pesa, ngono nje ya ndoa, kujivuna hadi kudhalilisha wengine.
Mungu hataki akuvue furaha. Anataka akupe furaha kubwa zaidi ambayo haiishi na haiumizi mtu.
HITIMISHO
Twaweza sema kuwa mambo ya dunia ni kitu chochote ambacho ww unakifanya kwa raha na starehe zako lakini kinakwaza, kinaumiza, kinajeruhi wengine aidha kwa nafsi au mwili
Chukulia mfano, uzinzi/uasherati. Lazima kuna upande unapata shida kutokana na tendo hilo. Huko kuna kutelekeza mimba,....
Kwa hiyo ndugu zangu, tuifurahie dunia bila kuumiza wengine
CIAO
Hizi ni kauli tunazopenda kuzisema pale mambo yanapokuwa sawa,
Tukiwa vizuri kiafya, kiuchumi....
Lakini maisha yakibadilika na matatizo yakatukumba, ndipo tunamrudia tena Mungu kwa unyenyekevu mkubwa.
Ukitaka kuamini hilo, muulize Feruzi🙏
Ni kwamba binadamu hubadilika, lakini Mungu hubaki kuwa yule yule.
TYK
Ukiyasoma maandiko yangu ya hivi karibuni utagundua kuwa ninahimiza sana kuhusu IMANI, KUMWAMINI KRISTO
Binafsi nimejishtukia na nikatafakari na kupata jibu kuwa huo ndio wito wangu. Hiyo ndiyo ile karama ambayo Kristo alinikubalia kama ambavyo niliandika katika kile kitabu changu cha USHUHUDA. Ushuhuda sehemu ya pili utafuata ndani ya miezi mitatu ijayo
Unajua ili kupata kumshuhudia Kristo ni lazima awe amekufanyia jambo la tofauti? Na pia ni lazima uwe umesimama naye ndio maana akafanya? Kaa mkao wa kuupata ushuhuda wangu sehemu ya pili ambao ni mwendelezo wa ile sehemu ya kwanza
Wengine wanahubiri kuhusu ndoa na mahusiano, masuala ya uchumi, masuala ya kijamii...... ambao ndio wengi
Binafsi naamini IMANI ndiyo kila kitu kwetu WAKRISTO. Imani isiyokuwa na mashaka
Shida kubwa tuliyonayo ni kuwa na imani haba, imani yenye mashaka. Tunasali, tunaomba lakini hatuamini kama tunachoomba tutapata, tunakuwa na mashaka. KRISTO HAPENDI KABISA
Ukiwa na IMANI THABITI utapata vyote, vya hapa duniani na vya mbinguni. Yesu mwenyewe anatuambia 'ukiamini na kutii tutakula mema ya nchi'
Mm najitahidi kufanya hivyo na kweli nakula mema ya nchi. Ww unayefahamu hali yangu waweza shangaa. Nakula mema gani mm? 😂
Kwangu mm mema ya nchi, cha kwanza kabisa ni kuwa na AMANI, ile itokayo kwa Kristo (unaijua? 😂). Maisha yana changamoto nyingi ambazo mara nyingi hutupelekea kukosa amani
Sasa mm nikiwa kwenye hali hizo za kukosa amani huwa nasema na Kristo na yy mara moja hunirejeshea amani. Huo kwangu ni utajiri mkubwa sana, utajiri namba moja
Kwa hiyo rafiki yangu, mwamini Kristo PASI NA MASHAKA ule mema ya nchi kama mm, na baadaye tukutane mbinguni 😂
CIAO
We wish to our brother a deserved life to live like others until.....
Jamani,
Kwa nn watu wanakuwa wagumu hivi kuelewa? Issue siyo Lissu wanayemuona
LISSU ni 'ideology' kwa WaTz.
Ma-Lissu ni wengi, mamilioni
Zaidi sana,
Wapinzani ni WaTz, wana haki na nchi yao.
KUKESHA WAKIWAZA NAMNA GANI YA KUWANYIMA WATANZANIA MAISHA YAO HALALI HUO NI UHARAMIA
ALERT: Maisha ya Lissu yako hatarini. Samia na Mwanae Abdul wanafanya mchakato wa kumuua Lissu kwa sumu. Lengo lao ni kumlisha sumu, na kisha kumuachia huru. Baada ya muda ataenda nje kutibiwa na atapatikana na ugonjwa usiotibika. Hii ni taarifa toka ndani ya mfumo
UKWELI ULIOFICHIKA KATIKA SAFARI YA KWENDA EMMAU
Matumaini yalivunjika. Mwokozi alikuwa akitembea kwa miguu.
Wanafunzi wawili waliondoka Yerusalemu wakiwa na huzuni kubwa, wakitafakari tena na tena kifo cha msalabani cha Kristu. Walikuwa walikuwa na huzuni yao wenyewe, wasiweze kutambua kwamba ufufuko ule walioshindwa kuamini ulikuwa unatembea nao wakati huo kama mgeni.
Upofu na Matarajio Yaliyopotea
Wanafunzi walivunjika moyo kabisa kwa sababu Yesu hakufanana na mpango wao wa kibinadamu wala matarajio yao ya kisiasa kuhusu Masihi.
Mara nyingi tunakosa kuona uwepo wa Mungu katika maisha yetu kwa sababu tunahangaika sana na kulia kwamba Mungu hakujibu maombi yetu vile tulivyotaka atujibu
Utimilifu wa Maandiko
Kabla Yesu hajafichua utambulisho wake wa kimwili, alitumia masaa akifungua maandiko kutoka kwa Musa hadi kwa Manabii. Hii inaonyesha kwamba Mungu anataka imani yetu ijengwe imara katika ukweli wa milele wa Neno lake kuliko katika uzoefu wa kihisia unaopita haraka.
Kufichuliwa kwenye kuvunjika Moyo
Macho ya wanafunzi hayakufunguliwa kwa hoja kubwa ya kitheolojia, bali katika tendo la kawaida na la ukaribu la Yesu kuvunja mkate mezani.
Mara nyingi katika nyakati zetu za unyenyekevu, ushirika, na uvunjifu ndipo Bwana hufanya uwepo wake uonekane dhahiri kwetu.
“Wakaambiana, ‘Je, mioyo yetu haikuwa ikiwaka ndani mwetu alipokuwa akisema nasi njiani na kutufungulia Maandiko?’”
UKWELI ULIOFICHIKA
Yesu hakuachi kwa sababu tu unapambana na mashaka, hofu, mkanganyiko, au moyo mzito. Hata unapokuwa unaondoka mahali pa ahadi ukiwa umeshindwa kabisa, yuko tayari kukufuata, kutembea njia yako ya upweke pamoja nawe, na kujenga upya imani yako kwa uvumilivu toka ndani.
Je, umeshughulika sana kurudia kukumbuka masikitiko yako ya zamani hivi kwamba unamkosa kabisa Mwokozi anayetembea pembeni yako katika huzuni yako?
Nami naendelea kuhimiza mikataba ya rasilimali iwekwe wazi kwa mujibu wa sheria. Si ajabu ni mizuri lakini sasa asemavyo Mhe Mpina kwanini kificho? Unaliletaje taifa pamoja bila kujenga TRUST? KUAMINIANA?
FUNDISHO - KISA CHA NABII YONA
Yona hatimaye alitambua kwamba yeye ndiye sababu ya machafuko yaliyokuwa yakizunguka chombo. Katika wakati ule, alikoma kulaumu hali na alikubali ukweli.
(Ukweli uliopelekea yy kutupwa baharini. Na alijua akisema kweli atatupwa baharini. Lakini yy alisema. Unaweza kuona haikuwa kitu chepesi)
Mabadiliko mara nyingi huanza tunapokoma kutafuta visingizio na tunapokiri kwa uaminifu maeneo tuliyokuwa tukipinga mapenzi ya Mungu.
Mungu yule yule aliyemfuatilia Yona bado anatufualia na sisi leo. Neema yake inafikia mpaka katika dhoruba, kushindwa, kukata tamaa, na njia potofu. Anapoita, utii daima ni salama kuliko kukimbia, na kujisalimisha daima ni bora kuliko kupinga.
Ikiwa Mungu anaruhusu dhoruba katika maisha yako sasa hivi, usikate tamaa. Mawimbi yanaweza kuwa makali, lakini kusudi lake ni kubwa zaidi. Kile kinachoonekana kama kurudi nyuma kinaweza kuwa mwanzo wa urejesho wako. Mtumaini yeye katika dhoruba, mtii katika kutokuwa na uhakika, na umwone akigeuza changamoto yako kubwa zaidi kuwa ushuhuda wa uaminifu wake.
Papa Leo amekuwa kiongozi wa kwanza wa Kanisa Katoliki duniani kuhutubia Bunge la Spain. Pia ameingia uwanja wa Santiago Bernabeu wa Madrid kukutana na waumini tena ametembelea wasio na makazi. Leo yupo Barcelona, pia ataenda visiwa vya Canary kuwaona wahamiaji wasio na vibali
West Ham are really trying to delay Mateus Fernandes’ move to Man United with crazy prices just to make us back down?
Brentford and Mbeumo did the same thing 😂
West Ham are really trying to delay Mateus Fernandes’ move to Man United with crazy prices just to make us back down?
Brentford and Mbeumo did the same thing 😂