ACP Mushana Lugola Mujema.
Huyu ni mkuu wa POLISI JAMII, Mkoa wa Kipolisi Ilala, askari wa Cheo chake hatukutegemea anaweza kumpiga rungu Katibu Mwenezi wa BAVICHA.
HUYU anatakiwa kuwa wa mfano,
Ashitakiwe kwa jina lake, Tukamate Mshahara wake.
Msimamo wa CHADEMA Unatolewa na Vikao vya Maamuzi Kikatiba, Hizi ni Sanaa za Jeshi la Polisi.
Amani ya Kweli ni Kujua Hatma za DAMU za Vijana Wenzetu na Hatma ya Mwenyekiti Wetu Kuwa Huru.
Pia Tunatambua Haki ya Maandamano Kikatiba.
By Victor Baleke- Mwenyekiti BAVICHA KANDA
Karatasi Huchanika, Lakini Sauti ya Umma ni Jiwe. Ukijaribu Kuirusha kwenye Pipa la Taka, Utavunja Pipa Lako Mwenyewe na Kelele Kali za Pipa.
Hauwezi Kuifuta CHADEMA Kwa Kalumu ya TSH 500/= ya Sisty L. Nyahoza.
CHADEMA Ina Makaburi, Walemavu, Yatima NK na Sio Majengo na Magari.
Tanesco Toeni UFAFANUZI,
Kwanini Mteja Anafungiwa Mita Mwezi wa Tatu 2026(Mteja Mpya), Akinunua Umeme Mnamdai Kodi ya Pango Kutoka Mwezi wa Saba 2025 ?
Tena Bila Taarifa Yoyote Kwa Watanzania.
Kodi Gani Inadaiwa Kabla ya Uwekezaji na Huduma Kutolewa ?
OCD Ashusha Bendera za CHADEMA Leo.
Anaitwa Christopher Msonsa, Ni OCD Wilaya ya Kipolisi Mbalizi.
Huyu Anatakiwa Awemfano, Afundishe Kuheshimu Haki za Kisiasa kwa OCDs Nchi Nzima, Apelekwe Mahakamani Akaeleze Mamlaka Ametoa Wapi.
Wanataka Maridhiano kwa Matendo ya Aina Hii.
Miaka 65 ya Uhuru π π .
Mkoa Ambao Ndio Mkubwa Kibiashara na Taswira ya Nchi Pia, Sikutegemea Mkuu wa Mkoa Wake Anaweza Kutoa Tamko la Namna Hii.
Serikali Imezidiwa Uwezo na Viwanda Vinavyotengeneza Maji DSM ?
Real ?
Najiweka Kwenye Nafasi za Marehemu,
Niwe Ardhini Kwa Kudai Haki.
Halafu Wewe Unaenisoma Unaenda Kuridhiana na Walioniuwa Nikitete Madai Yangu Mimi na WEWE.
ππππ
#NOMaridhiano
Mtunza Hazina wa @BawachaTaifa Mkoa wa Rukwa, Amekamatwa na Kupewa Kesi ya UHAINI.
#NOMARIDHIANO
Tunaridhiana Na Nani Ikiwa Watu Wetu Wanaonewa Kwa kesi za Uongo.
One Thing I've Learned From Raila Odinga Is This
" Become What You What! Or Die Trying, Don't Ever Give Up, As Long as Your Alive, The Only Time To Give Up, Is When You Leave This World
He Ran For The Presidential and Didn't Win, But He Never Stopped Trying"
Victor Baleke - CDM
Mwenyekiti BAVICHA Lupemba, Mh Abedinego Sanga, Jana Usiku Ametekwa Akiwa Kijiji Kwao Matambwe (Lupembe).
Ametekwa Na Watu Wenye Silaha Waliojitambulisha Ni Polisi.
Pia Wameendelea Kutumia Simu Yake, Kumchatisha Mjumbe Wa CC Rose Mayemba Kuhusu Maandamano.
Na Victor Baleke .
Amenijuza Wakili Mathias Paul Mlimi kwamba wapo watu watatu wanaojiita ni wateja wanahitaji huduma ya uwakili wananitafuta mimi. Wamekiri kwake kuwa wana namba zangu lakini wanatamani kazi yao niifanye nae. Ameniambia hajawaelewa na anawasiwasi nao. Nimezipokea taarifa hizo.
#BreakingNews Jeshi la Polisi limezingira ofisi za @TanganyikaLaw na kufunga barabara zote za kuelekea katika ofisi hiyo na kuzuia watu kufika eneo hilo, ambapo tulikusudia kuadhimisha #ChademaMashujaaDay kuwakumbuka wahanga wa kupigania haki na demokrasia nchini.
Leo Nimeshiriki Siku ya Mashujaa Kwa Kumtembelea Kamanda Remi Swalo, UYOLE - MBEYA.
Kamanda Remi, Alikatwa na Panga Kichwani Akiwa Wakala wa CHADEMA, Hali Iliyompelekea Ulemavu wa Kudumu wa Kutosikia na Kuongea Tena.
Wahandishi Hawa Wanachelesha Sana Mabadiliko Nchi Hii, Mizaha Mingi, Haulizi Maswali Magumu !!!
Wakipata Majina Wanageuka Wafanya Biashara.
Tuoneshe Misimamo Mikali Dhidi ya Waandishi Kanjanja.
#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 1
Mahakama imeamuru kuwa committal itasomwa yote bila kurushwa live.
Wakili wa Serikali Katuga anaendelea kusoma kwa sasa.
Maajabu yaliyotokea ni kwamba mawakili wa serikali waliomba maelezo ya mashahidi wa siri yasirushwe live.
Lakini cha ajbu mahakama imesema maelezo ya mashahidi wote yafichwe na yasiwe live.
Kifupi mahakama imetoa uamuzi ambao hata serikali haijaomba. Imefunga kila kitu na kesi kuzimwa.
Katuga anaendelea, amemkumbusha Mtuhumiwa Shitaka lake na kumkabidhi taarifa ya mashitaka.
Anasema Jamhuri itakuwa na mashaidi 30 na vielelezo vya myaraka 9.
Maelezo yataanza kusomwa na Thawabu Isa wakili wa serikali.
Anasimama na kuanza kusema SSP Kangio, atakuwa shahidi wa kwanza. Ameapa kusema ukweli na maelezo yake ni kama ifuayavyo.
Nimeajiriwa 2003 polisi na mikoa mbalimbali ninefanya. Nimekuwa na vyeo tofauti na sasa ni mrakibu wa polisi kanda ya Dar es salaam. Nafanya majukumu ya kusimamia askari katika majukumu ya kiupelelezi.
04/04/2025 nikiwa ofisi afande Kaaya anayefanya Doria mtandaoni nilimtaka anipe picha mjongeo kuhusu maudhui yakiyokuwa yanatoa taarifa yenye uchochexi.
Maudhui hayo ni mapolisi wanakuja na mabegi ya kura feki kwenye vituo. Jambo ambalo ni uongo. Majukumu yetu ni ulinzi na sio kuiba kura.
Pia maelezo yaliyokuwepo ni kuhusu majaji ni MACCM hivyo wanafanya kazi kwa mujibu wa CCM. Na sio kweli kwamba majaji wanafanya kazi kuwaonea wapinzani. Na hivyo taarifa hii ni uongo na yalilenga kuleta chuki.
Pia alisema kuenguliwa kwa wapinzani ni mkakati wa serikali hivyo zilikuwa ni uongo na kutengeneza chuki dhidi ya Rais.
Na msimamo wetu ni wa uasi. Ni kweli ni msimamo wa uasi kwani tunaenda kukinukisha na huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli.
Katika picha mjongeo hiyo mzungumzaji alikuwa ni LISSU. Na aliyokuwa anafanya yalikuwa na nia ya kuitishia serikali ili ayapate yeye na wafuasi wake.
Niliamuru Insp. Kaaya aanze kufanya uchunguzi wa jalada hilo na taarifa hiyo ndio akafungua kesi na kuanza uchunguzi. Na akaanza kujaza PF500
Baada ya kutoa maelekezo kutafuta mjengeo iliyoerekodiwa eneo husika nilitoa taarifa kwa mabosss wangu na kuhusu kile alichosema TUNDU LISSU mtandaoni. Niliripoti kwa afande DCI akasema tuendeleee
Nilimtafuta kiongozi wa JAMBO TV anipe video ile na baadae akasema video anayo P ambae kasafrir. Hivyo nikatoa taarifa kwa maboss kuwa video tutaipata kwa P ambayo yuko Dodoma.
DCP NG'ANZI nilimpa taarifa kuwa tutaipata kwa kijana wa Jambo TV ambae yuko Dodoma.
Haya ni maelezo ya George ambae ni kaimu mkuu wa upepelezi kanda ya Dar es salaam. Yansomwa maelezo yake hapa mahakamani.
Nikaeleza lifunguliwe kosa la uhaini kwasababu aliesema TUNDU lisuu hayo maneno yake, yeye ni Askari ambae ana cheti cha Kujenga taifa kutoka jeshi la JKT hivyo alikuwa na wajibu wa kulinda amani ndani ya Taifa letu. Kusema maneno kama hayo ni kosa kisheria.
Hayo ndio maelezo yangu yote. Yameisha maelezo ya George na anasemaa anayo maelezo ya nyongeza Ya huyo SSP George akasema pia nilikabidhiwa TUNDU LISSU akitokea RUVUMA.
Nilimpokea Lissu na wakati nafanya mahojiano walikuja mawakili wake pia Tulienda kwenye ofisi yenye utulivu na nikamuonya kuwa anatuhumiwa kosa la uhaini. Na kumpa haki zake za msingi.
Huyu George ni msaidizi wa Mafwele. Anasemaa Lissu aligoma kutoa maelezo yoyote.
ASP. John. Ni shaidi wa pili ambae ni mkazi wa Temeke. Amekula kiapo na ushaidi wake ukaanza kuandikwa.
Nimeajiriwa 2005 na nina elimu ya computer na mfanyakazi wa polisi. Nimesoma vyuo ikiwemo Chuo Cha Polisi kurasini.
Nafanya kazi kwa DPP dawati la Doria mtandaoni. Na huwa napeleleza makosa yanayofanywa mitandaoni.
Huyu sasa ni shaidi wa pili baada ya yule wa kwanza ambae ni George.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Retweet yako.