"Ili kufanikisha elimu ya gredi ya kumi ,walimu wakuu na washikadau wote wanahitaji kuzingatia agizo la rais la kuwapokea wanafunzi wa gredi ya kumi bila vikwazo."
Omboko Milemba, mwenyekiti wa kitaifa chama cha KUPPET.
UKOSEFU WA USALAMA VIHIGA:
Maafisa wa usalama na ujesusi kaunti ya Vihiga waanzisha msako dhidi ya watu wasiojulikana waliovamia afisa mmoja wa polisi mlinda lango katika mejengo ya Bunge la kaunti ya Vihiga usiku wa kuamkia leo na kutoweka na bunduki wakimwacha na majeraha.
Wikendi ya maafa:
Wanaume wawili wamefariki hii leo, mmoja ajitikia kitanzi katika eneo la Chambiti,mwengine afariki katika kisima mjini Mbale huku mwanaume mwengine mhudumu wa Bodaboda alkuawa na watu wasiojulikana katika eneo la Chavakali usiku wa kuamkia leo.
Charles Otiende ndiye katibu mkuu mpya wa chama cha kutetea maslahi ya walimu wa shule za upili na vyuo anuwahi (KUPPET) tawi la Vihiga baada ya kuvuna ushindi wa kura 1704 kwenye uchaguzi wa chama hicho kaunti ya Vihiga.
Askofu mkuu wa Kanisa la African Divine Church (ADC) akiwaongoza waumini wa dhebebu hilo katika ibaada ya kufungua mwaka kwenye makao makuu ya dhebebu hilo katika eneo la Boyani, kaunti ndogo ya Hamisi.
Wafanyikazi wa serikali ya kaunti ya Vihiga kwenye kambi ya mazoezi katika vitengo mbali mbali wakijiandaa kushiriki mashindano baina ya wafanyikazi wa serikali za kaunti ( KICOSCA) yatakayoanza Jumatatu katika kaunti ya Siaya. Kaunti ya Vihiga itashiriki katika vitengo 24.
Kongole kwa waziri wa vijana na michezo kaunti ya Vihiga Dkt Ruth Agesa kwa kutawazwa kuwa waziri bora katika idara hiyo kanda ya magharibi na kumaliza wa pili kitaifa , kwenye hafla iliofanyika wikendi hii jijini Mombasa.
Katibu wa shule za upili katika chama cha kutetea maslahi ya walimu wa shule za upili na vyuo anuwahi (KUPPET) tawi la Vihiga Charles Otiende aitaka serikali kuongeza mkataba wa matibabu na Bima ya afya ya walimu ya Minet kwa muda wa mwaka mmoja zaidi ,mbadala na kuhamia (SHA).
Jopo la uteuzi la kuwapiga msasa wanachama wapya wanne katika bodi ya kutoa huduma katika kaunti ya Vihiga wakiongozwa na mwenyekiti Nicholas Simani ( wapili kushoto) katika makao makuu ya kaunti baada ya kuapishwa kwao.
Mwakilishi wa kike kaunti ya Vihiga Beatrice Adagala amekashifu matamshi ya gavana wa kaunti ya Nyeri Mutahi Kahiga akimtaka kujiuzulu kufuatia matamshi ambayo yaliashiria kufurahia kifo cha aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga.
Aliyekuwa mbunge wa Makadara Fred Omido na mwenyeki wa baraza la wazee kaunti ya Vihiga ambaye amekuwa mwadani wa mwendazake Raila Odinga akiomboleza kifo cha rafiki yake wa dhati.
Wakaazi wa kaunti ya Vihiga wazindua rasmi vikao vya Bunge la Mwananchi kaunti ya Vihiga katika eneo la makutano ya Chavakali, wakilenga vikao vya kila juma vitkavyohusisha wananchi kutoa maoni yao kuhusu uwajibikaji wa viongozi mbali mbali eneo hili na kitaifa.
Faith Kipyegon aishindia Kenya dhahabu ya tatu kwenye mbio za 1500m huku Dorcas Ewoi akipata fedha katika mashindano ya riadha ya dunia yanayoendelea kule Tokyo, Japan.
#worldathelticschamps
Video kwa hisani ya supersport
"Kaunti ya Vihiga ndio inakuwa kaunti ya kwanza kutia saini mkataba wa makubaliano ya kuimarisha mpango na mamlaka ya afya ya jamii(SHA) kwa wafanyikazi,"Dkt. Mercy Mwangangi, afisa mkuu mtendaji wa mamlaka ya SHA.