The Women's Legal Aid Centre stands in solidarity with Tanzanian women & children by providing legal aid services & a wide-ranging mix of public programming.
Tunampongeza Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Cuthbert Sendiga kwa kusimamia haki ya Mama aliyepokonywa vitu usiku kisa wizi wa mumewe na kuamuru arudishiwe vitu vyake.
Haki za Wanawake ni Haki za Binadamu.
@queen_sendiga
Tunashiriki wiki ya sheria wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera. Mwanasheria Felicia Isimula akitoa msaada wa sheria
# Msaada wa sheria ni Haki ya Binadamu
# Wiki ya sheria 2024
@Sheria_Katiba
Tumeshiriki Mkutano wa Kitaifa wa wadau utekelezaji wa uboreshaji wa Usalama wa Milki za Ardhi uliofanyika Dodoma.
Kauli Mbiu: Usawa wa Kijinsia katika umiliki wa ardhi kwa ustawi wa Jamii.
@wizara_ya_ardhi
@ofisi_ya_rais_tamisemi
WLAC imetoa mafunzo ya sheria ya ndoa na mirathi katika kongamano la wajane lililoandaliwa na kanisa la Elim New Covenant Church Tanzania. "Thamani ya Mwanamke mjane katika ngazi ya jamii na taifa"
WLAC imeshiriki katika mazungumzo na waandishi wa habari kupitia Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia (MKUKI) chini ya uratibu wa @wildaf na @maendeleoyajamiitz katika mazungumzo na waandishi wa habari kuhusu siku 16 za uanaharakati dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Elimika kisheria kupitia machapisho. Fahamu masuala ya kisheria kupitia vitabu ambavyo vimeandikwa kwa lugha nyepesi na kuweza kuongeza uelewa wa masuala ya Kisheria.
Sheria ya ardhi imebainisha haki sawa kwa mwanamke na mwanaume kumiliki ardhi. Changamoto inayozikabili jamii nyingi ni mfumo kandamizi unaowanyima fursa wanawake kumiliki na kunufaika na ardhi.
Ardhi ni Mali kwa pamoja tujenge jamii inayolinda haki za umiliki wa ardhi.