@MabalaMakengeza Huyo Thiery Henry na mzee Wenger nao wachunguzwe...wakiingia uwanjani tu Arsenal na Ufaransa wanapoteza na majeruhi juu..Sasa mchezaji anachezea Arsenal na na ni mfaransa na Wenger yupo uwanjani..ππππ
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Fiston Mayele, anatarajiwa kujiunga na Klabu ya Al Ahli Tripoli ya Libya baada ya kufikia makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Dola Milioni tano za Marekani (Shilingi za Tanzania Bilioni 13.15).
Mayele, aliyekuwa akiichezea Pyramids FC ya Misri, anatarajiwa kuwa mmoja wa usajili mkubwa wa Al Ahli Tripoli katika dirisha hili la usajili, huku klabu hiyo ikiendelea kuimarisha Kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.
Ripoti mbalimbali zinaeleza kuwa pande zote zimekubaliana kuhusu masharti ya mkataba, na kinachosubiriwa ni kukamilika kwa taratibu za mwisho kabla ya kutangazwa rasmi kwa uhamisho huo.
#KitengeSports