Kombe la Mataifa ya Afrika. Kila mtu katika Premier League, Bundesliga, Ligue 1 na ligi za Uturuki analalamika.
โWale jamaa wametoa milioni 20 kila mmoja, ada za uhamisho na kila kitu. Kombe la Mataifa ya Afrika. Hakuna kitu zaidi ya vuvuzela. Viwanja ni vibovu, vimekauka.
Mwamuzi wa kati wa mchezo namba 220 wa ligi kuu ya NBC Tanzania bara kati ya Simba SC dhidi ya Singida Black Stars (1-0), Hery Sasii amefungiwa miezi sita (6) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema Sheria 17 za mpira wa miguu.#WestUPDATES
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amepiga marufuku mechi za Tottenham kuonyeshwa nchini humo.
Korea Kaskazini hairuhusu mchezo wowote unaohusisha wachezaji kutoka nchi jirani ya Korea Kusini kuonyeshwa.
Ni kutokana na mgogoro wa Kidiplomasia baina ya Mataifa hayo mawili.
Serikali ya DR Congo imeiandikia barua NBA, ikiiomba kuacha kudhamini ligi ya mpira wa kikapu , Afrika ambayo huusisha taasisi za Rwanda.
Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Therese Wagner, amesema kuwa NBA itashusha hadhi na kupoteza kuaminiwa kama itaendelea kujihusisha na Rwanda.
โDhidi ya Simba, Dodoma, KenGold ni baadhi ya michezo ambayo Yanga walionekana wakinufaika na waamuzi, mbona Ally Kamwe hakuzungumzia? Kwa hiyo kuna namna Ally Kamwe na mashabiki wa Yanga wameanza kupata presha baada ya Simba kuonekana wana ubora msimu huu.โ______Geoff Lea.
"Jonathan ni mchezaji mzuri sana, jambo la kwanza tunalopaswa kufanya, bila shaka, ni kumfikisha kwenye kiwango cha utimamu wa mwili tunachotaka. Kwa sababu si tu kuhusu utimamu wa mwili, bali pia kuhakikisha kwamba hapati majeraha"Saed Ramovic Kocha Mkuu wa Yanga.#WestUPDATES
Marc Guehi anaweza kuadhibiwa na chama cha soka nchini Uingereza (FA) kwa kuandika 'I Love Jesus' kwenye kitambaa cha unahodha alichokivaa kitambaa hicho kilichokuwa kina rangi za kampeni ya kutetea mapenzi ya jinsia moja beki huyo akaandika maneno hayo kwa juu ya kitambaa hicho
Baada ya kuweka kambani chuma 2 kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Damac huko Saudia Cristiano Ronaldo kafikisha magoli 915 ikiwa ni safari ya kuelekea magoli 1000 aliyosema anataka kufikisha kabla ya kustaafu soka.#WestUPDATES
Baada ya taarifa ya kukamatwa kwake siku ya Ijumaa kutoka mauzo ya kazi za rapa Lil Durk yamepanda kwa asilimia 28 kwenye vyanzo vyote vya usikilizwaji wa muziki.
Durk anashikiliwa na mamlaka za usalama nchini Marekani kwa tuhuma za kupanga njama za mauaji ya rapa Lil Pap.
Wachezaji saba wa klabu ya Chavuma Town Council ya nchini Zambia wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa kwenye ajali ya basi wakati kikosi hicho kikielekea kwenye mechi ya ligi ya daraja la tatu, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
Baada ya kuwa nje ya uwanja kwa siku 369 nyota raia wa Brazil Neymar Jr amerudi uwanjani hii kutumikia timu yake ya Al Hilal,
Neymar aliingia dakika ya 77 akichukua nafasi ya Nasser Al Dawsar mchezo ambao Al Hilal wameshinda kwa mabao 5-4 dhidi ya Al Ain.#WestUPDATES
Kwa mara ya kwanza, Mshindi wa Ballon dโOr 2024 hatajulishwa kabla ya sherehe na Kandanda ya Ufaransa! Hii inamaanisha kuwa mshindi hatajua kuwa ameshinda hadi bahasha ifunguliwe wakati wa utoaji wa tuzo Oktoba 28. #WestUPDATES
Kocha Eric Ten Hag alipewa michezo 2 kutetea kibarua chake akishindwa uamuzi mgumu utachukuliwa na tayari michezo yake miwili kamaliza kwa sare mbili.
FC Porto 3-3 Manchester United
Aston Villa 0-0 Manchester United
Bado 80% ya bodi ya Man United inamuungaa mkono Ten Hag.
FA imemfungia mechi 8 na faini ya ยฃ15,000 [ Tsh Milioni 53] mchezaji wa Preston North End ,Milutin Osmajiฤ kwa kosa la kumngโata beki wa Liverpool anayechezea Blackburn kwa mkopo kwenye mchezo wa EFL Championship mwezi uliopita.#WestUPDATES
Annie Kilner ambaye ni mke wa beki wa kulia wa Manchester City , Kyle Walker anadai fidia ya pauni milioni 15 sawa na Bilioni 54,428,016,000 kwa pesa za Tanzania kama fidia ya yeye kukubali kuendelea kubaki kwenye ndoa baada ya mume wake kuzaa watoto wawili nje ya ndoa.
Beki wa kulia wa Manchester City Kyle Walker amenaswa tena akikojoa kwenye moja ya ukuta wa eneo la wazi wakati anatoka kwenye baa ya Manchester usiku wa Jumamosi , kitendo hiko kinahatarisha mlinzi huyo kutozwa faini ya pauni 150 ambayo ni sawa na Tsh 544,000.#WestUPDATES
Klabu ya AmaZulu ya South Africa wameachana na kocha mkuu Pablo Franco Martin pamoja na Msaidizi wake Aitor van den Brule ameondoka katika klabu hiyo baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha mwanzo wa msimu wa ligi kuu ya South Africa.
FULL TIME-CAF SUPER CUP
Al Ahly 1-1 Zamalek
Penalt
(3-4)
-Zamalek wababeba ubingwa wa CAF Super Cup
-Al Ahly wanapoteza Caf Super Cup mara ya 2 mfululizo msimu uliopita alipigika chuma 1-0 mbele ya USM Algier
Klabu ya Al Ahli Tripoli ya Libya imemtimua kocha mkuu Chokri Khatoui baada ya kushindwa kuiongoza timu hiyo kufuzu katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumapili dhidi ya vigogo wa Tanzania, Simba SC.#WestUPDATES